Mada yako ingekuwa ya msaada sana kwetu wasomaji wako,ungetueleza pia ni watu wangapi wamepimwa kwa siku, na kati ya hao waliopimwa ni wangapi wamepatikana na ugonjwa. Hiyo ingeleta maana zaidi.
Hata hivyo naungana nawe kwamba hata kama ungetoa namba hizo huenda (kwa sababu sijui), bado namba zetu za wagonjwa zingekuwa ni pungufu zaidi ya wao.
Na kama ungekuwa mdadisi mzuri (sio lazima uwe mwanasayansi), ungekwenda mbele kidogo na kujiuliza sababu ya matokeo ha ni nini hasa?
Najua kwa jinsi ulivyowasilisha mada yako, majibu yako yangekuwa kati ya haya ninayopendekeza hapa chini:
- umahiri wa viongozi wetu kwa kuweka mipango imara ya kuzuia huo ugonjwa..
- sisi Mungu anatupenda sana, hasa baada ya kuhimizwa na kiongozi wetu kusali kwa siku tatu
- sisi watu wetu hawafi kwa wingi kwa sababu huduma za afya zetu ni imara zaidi kuliko za kwao
- viongozi wetu wamegundua 'nyungu' na wakatuhimiza. Ni kinga imara kwa huu ugonjwa
- n.k, n.k.
Kwa hiyo, kutokana na yote haya ingekuwa ni upuuzi na kupoteza muda kusikiliza ngonjera za wataalam, hata wa hapa kwetu, na wale wa kimataifa kama WHO, na kufuata taratibu walizokuwa wanatushauri tuzifuate.
Sasa basi, kwa vile imethibitika kwamba sisi COVID-19 haitutishi kwa lolote, hata uchumi wetu hautaathirika kwa lolote, kwa maana sababu kubwa ya kuchukua hatua tulizochukua zilikua ni mapambano ya kuulinda uchumi wetu.
Ninayo mengi ya kuungana mkono na wewe, lakini ngoja tuachie hapa kwa sasa; huku nikijipiga kifua kwa furaha ya kuwaonyesha wazungu (bila shaka mabeberu), umahiri wetu mpya.