Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: Korea Kusini

Kasi ya maambukizi inazidi kuongezeka nchini humo huku visa vipya 70 vikiripotiwa.

Mpaka hivi sasa, Korea Kusini imekwisharipoti visa takribani 833 na vifo saba (7).
 
mbona idadi ya wafu ndogo sana. kumbe kawaida tu
 
Kawaida tu,inazidiwa Hadi na kipindupindu banah..
mbona idadi ya wafu ndogo sana. kumbe kawaida tu
nyi nanyi fateni uzi kwa mtililiko mpk chini muone
toka nipate akili sijawai ona ugonjwa wa mlipuko unaosambaa kwa kasi km huu na kuua watu wengi kwa muda mchache hivi halafu mpk ss mataifa hayajui yafanyaje
yaani
hayajui jinsi gani ya kuzuia kusambaa
hayajui hata mataifa mengne yameupata vp
hawajui tiba yake
hawajui kinga yake
na hawajui lini watapata kinga /dawa

halafu mnasema eti kawaida tu wakati hayo mafua ya ndege hayafui dafu kwa ugonjwa huu hata EBOLA cha mtoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We ndo be smart
Sio kila kitu unahisi utakavyo
Jamaa kakuelezea kimakini sana ila huelewi, shida ni ww

Sent using Jamii Forums mobile app
Kaeleza nini ? Hebu dadavua , kwamba kitoweo mtumie tokea miaka ya 30 huko kije kilete madhara 2020 ?? Almost miaka 100 ??? And you are buying into that idea ???

Alafu sio mtu mmoja n taifa, mfano wake ungekua na maana kama angeathirika mtu mmoja tu , taifa Hilo Hilo waathirika Zaid ya watu 70000, in space of two months, kwann wasidhurike muda woooote huo ?? Be smart like your smartphone bro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ni wazo lako , na kama wamepata ugonjwa ambao hawakui kuupata , hata huo utakua man made , Mungu haumbi tena , alishamaliza , kiumbe kipya kinachokuja chenye uhai n mikono ya binadamu... Mengine hua n genetic modified yaweze kua lethal zaid

Sent using Jamii Forums mobile app
 
vipi mbona unatokwa povu mkuu, we tulia uugue corona, na inakuja
 
Mkuu tusizunguke sana katika jambo ili..
Nini msimamo wako juu ya chanzo cha ugonjwa huu?, ni silaha za kibaiolojia ama ni moja ya janga la asili tu kama yalivyo mengine?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Si janga la asili , labda nikuulize , Kwani Mungu bado anaendelea na uumbaji ??

Hawa wadudu ni mikono ya binadamu, wanafanya genetic modifications wanayaachia , shida inakua kama hivi.... Kuna kitabu kama nikikumbuka nitakileta hapa..kinahusu Mossad..shirika la kijasus la Israel.. virusi vya Ebola walikua navyo kabla hata havijawahi reportiwa popote dunia kama vimeleta maafa , na hata hapa naamini Wana magonjwa mengine mengi tu deadly na lethal kuliko hata huu..ni swala la muda tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ebola inachinja acha utani , sema huu unasambaa kama umeme

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Iran imeripoti visa vipya vinne (4) pamoja na vifo vipya vinne (4). Jumla, visa 47 pamoja na vifo 12 vimeripotiwa hadi sasa huku vyanzo vingine vikidai kuwa idadi ni kubwa zaidi.
 
NEWS ALERT: Iranian lawmaker claims at least 50 people have died of coronavirus in the city of Qom; the official death toll stands at 12. [ILNA]

The lawmaker added that he has urged the minister of health to quarantine the city. ILNA reports that, last night alone, 7 people in Qom died of coronavirus.
 
UPDATE: Italia

Visa vipya 38 vya COVID-19 vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 193 nchi nzima huku wanne (4) wakipoteza maisha hadi sasa kutokana na virusi hivyo.
 
UPDATE: Bahrain imeripoti kisa cha kwanza cha COVID-19 nchini humo. Kisa hicho kikiwa ni raia wake aliyerejea nchini humo akitokea nchini Iran.

Wizara ya afya nchini humo imetangaza kuwa, wale wote wenye dalili za homa, kukohoa na kushindwa kupumua vizuri, kuhakikisha wanajitenga na wengine na kisha kupiga simu namba ya dharura (444).
 
Ebola inachinja acha utani , sema huu unasambaa kama umeme

Sent using Jamii Forums mobile app
mi nafikiri huu ugonjwa pia unaweza kuwa ni wa mda tu kama magonjwa mengine ya mlipuko, tatizo dunia ya sasa media ndo zinafanya mambo yanakuzwa. bila media tatizo lingeisha kimya kimya, mbona epidemics zinatokea miaka mingi na kuisha zenyewe. yani pia ni mabadiliko ya hali ya hewa, kuna baadhi ya bacteria na virus huwa wanaishi kwenye viipindi tofauti vya hali ya hewa, hali ya hewa ya kipindi hicho ikiisha na vyenyewe vina potea. nahisi pia ndo maana hii kitu haionekani africa kwa sababu ya hali ya hewa iko tofauti. tropical na equitor kuna joto sana, flue virus hawapendi kuishi kwenye joto.
 
UPDATE: Korea Kusini imeripoti kifo kipya nchini humo kinachohusishwa na COVID-19. Mpaka sasa, idadi ya waliokufa kutokana na virusi vya COVID-19 nchini humo imefikia 8.
 
ila pia nahisi kwa waafrika tulivo less protected, wale jamaa wameisha utest huu ugonjwa kwa waafrika kitambo na wameona waafrika hawaugui, na siamini kama ni kweli huu ugonjwa haujawahi kujaribishwa huku, wachina ni wajanja sana na wako fasta fasta sana katika kutrace tatizo, so kumuambukiza mtu mweusi ili waone reaction ni option ambayo lazima waifanye kwa siri bila kukwambia
 
Trump alisema mpaka mwezi April utakua umeisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Muingiliano ulipo kati ya Africa na China , waafrica wanao enda huko kibiashara n wengi Sana , mpaka sasa tuko salama , Hilo eneo lenyewe la Huwan..waafrica wako kibao ila mpaka sasa wako salama wote , huenda ukatupita pembeni huu ugonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…