Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: Iran

Mmoja wa wajumbe wa baraza la washauri wa kiongozi wa nchi hiyo Ayatollah Khamenei ameripotiwa kufariki dunia mnamo Jumatatu kutokana na virusi vya Corona.

Mohammad Mirmohammadi, 76, amepoteza maisha katika hospitali ya Masih Daneshvari mjini Tehran alipokuwa akipatiwa matibabu, shirika la habari la nchi hiyo IRNA limeripoti.

 
Nchini Iran mambo yawezekana ni mabaya kuliko wanayotuambia.
Mbunge wa kule Qom alisema kuwa washazika watu 50 serikali ikakanusha ila hadi sasa imefika Ikulu na vifo vyakimbia sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mpaka sasa hakuna hata mweusi kuugua Corona duniani kote kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
Immunity za waafrika ziko more resistant zaidi ya races zingine Leo Ni miezi kadhaa imepita watu zaidi ya 3000 wamefariki ila hakuna mmatumbi hata mmoja.

Mwafrika hafi kwa mafua, Corona virus Ni mafua tu ambayo Ni kiboko ya wazungu na waasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ugonjwa utafikia watu weusi ru ni swala la muda

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama Kuna watu Wana deep connection na Asia Basi ni Africa kutokana na biashara na uchumi Ila Hadi leo hakuna taarifa yeyote rasmi ya mwaafrika kufa kwa haya mafua.

Hubei Ni mji wenye waafrika wengi kuliko sehemu yeyote ya China na ndio chimbuko la huu Ugonjwa lakini Hadi muda huu hakuna aliefariki na aliepata misukosuko kidogo Ni janki wa Cameroon ambae yeye alipewa paracetamol pekee afu punde akapewa discharge arudi nyumbani.

Mafua haya hayamuuwi mwafrika labda Kinga zake ziwe chini saaana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
🌚🌚🌚🌚🌚🌚🌚🌚🌚🌚🌚


☝☝☝never die with flu
 
Iran hali ni mbaya sana, kama inafikia hatua hadi viongozi wakubwa kufa kwa huu ugonjwa ujue hali ni mbaya.
Vipi kwa wananchi wa kawaida?
Nashawishika kusema hivi virusi vya Corona ni hatari zaidi ya tunavyosikia.
 
UPDATE: Uhispania

Visa vipya 36 vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 120 huku wagonjwa watano (5) wakiripotiwa kuwa katika hali ya umahututi.

Mpaka sasa wagonjwa wawili (2) wameripotiwa kupata ahueni.
 
UPDATE: Uhispania

Visa vipya 36 vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 120 huku wagonjwa watano (5) wakiripotiwa kuwa katika hali ya umahututi.

Mpaka sasa wagonjwa wawili (2) wameripotiwa kupata ahueni.
Ila white people akili zao wanazijua wenyewe hapo hata LA liga haijasimamishwa








😷😷😷😷😷😷😷😷😷😷
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…