Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: Wizara ya afya ya China imeripoti visa vipya 96 nchini humo sanjari na vifo vipya 28 nchi nzima huku visa 74 kati ya hivyo vikiripotiwa Hubei pekee.
 
UPDATE: Mainland China
  • 80,651 confirmed cases so far
  • 3,070 deaths so far
  • 5,489 in serious condition
  • 55,404 recoveries
 
UPDATE: Korea Kusini imeripoti visa vipya 174 pamoja na vifo vipya viwili (2) nchini humo na kufikisha jumla ya visa 6,767 pamoja na vifo 44 nchi nzima.
 
UPDATE: South Korea
  • 6,767 confirmed cases so far
  • 44 deaths so far
  • 52 in serious/critical condition
  • 108 recoveries
 
UPDATE: Norway imeripoti visa vipya 26 nchini humo na kufikisha jumla ya visa 127 nchi nzima.

Hadi hivi sasa, Norway haijaripoti kifo chochote kinachohusishwa na COVID-19 nchini humo.
 
UPDATE: Ujerumani

Visa vipya 31 vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 670 ambapo wagonjwa wapatao wawili (2), wako katika hali mbaya zaidi huku wengine 17 wakiripotiwa kupata ahueni.

Mpaka sasa, Ujerumani haijaripoti kifo chochote kile kinachohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.
 
UPDATE: Uhispania

Visa vipya 28 vimeripotiwa nchini Uhispania na kufikisha jumla ya visa 402 huku wagonjwa wapatao saba (7) wakiwa katika hali mbaya zaidi na wengine wawili (2) wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo nchini humo vinavyohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) imefikia tano (5) hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Barani Afrika

Visa viwili (2) vya kwanza vimeripotiwa nchini Cameroon.

Visa viwili vya Cameroon ni raia wa kigeni kutoka nchini Ufaransa.
 
UPDATE: Iran

Visa vipya 1,234 pamoja na vifo vipya 16 vimeripotiwa nchini Iran hivyo kufikisha jumla ya visa 4,747 huku wagonjwa wapatao 913 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo imefikia 124 hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Visa vya kwanza vya COVID-19
  • Kisa cha kwanza (1) kimeripotiwa nchini Bhutan
  • Kisa cha kwanza (1) kimeripotiwa nchini Serbia
  • Kisa cha kwanza (1) kimeripotiwa jijini Vatican
  • Kisa cha kwanza (1) kimeripotiwa nchini Colombia
 
UPDATE: Italia

Visa vya COVID-19 vipatavyo 4,636 vimekwisha ripotiwa nchini Italia hadi sasa ambapo wagonjwa wapatao 462 wako katika hali mbaya zaidi huku wengine 523 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo imefikia 197 hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Marekani

Idadi ya visa vyote nchini Marekani imefikia 329 hadi sasa ambapo wagonjwa wapatao nane (8) wako katika hali mbaya zaidi huku wengine tisa (9) wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo imefikia 16 hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Japan

Idadi ya visa vyote nchini humo imefikia 350 hadi sasa huku wagonjwa wapatao 29 wakiwa katika hali mbaya zaidi na wengine 10 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) vilivyothibitika nchini Japan imefikia sita (6) hadi hivi sasa.
 
thnkx kwa kutufumbua macho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…