NEWS ALERT: Safari za ndege zasitishwa
Uingereza: Shirika la ndege la Uingereza, British Airways, limesitisha safari zake za Italia baada ya nchi hiyo kuwekwa kizuizini hadi mwezi Aprili ili kukabiliana na virusi vya Corona.
Israel: Shirika la ndege la Wizz Air limesitisha safari zake kati ya Israel na Italia ikiwa ni hatua ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ili kukabiliana na virusi vya Corona
Denmark: Waziri mkuu wa nchi hiyo Mette Frederiksen ametangaza kusitishwa kwa safari za ndege kuingia nchini humo kutoka katika mataifa yaliyoathirika zaidi kama vile Italia, Iran na Korea Kusini.
Uhispania: Serikali imetangaza kusitishwa kwa safari za ndege za moja kwa moja kutokea nchini Italia kwa muda wa wiki mbili ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona.
Ureno: Serikali imetangaza kusitishwa kwa safari za ndege za abiria za kwenda na kutokea Italia kwa muda wa siku 14 kuanzia Jumatano ikiwa ni hatua mojawapo ya kuzuia kuenea zaidi kwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.
Canada: Shirika la ndege la nchi hiyo, Air Canada, limesitisha safari zote za kwenda na kutokea Italia hadi mwezi Mei kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.