Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Sisi tunapokea tu, wajehuku sisi niwakarimu tunaubinadamu.
NEWS ALERT: Safari za ndege zasitishwa

Uingereza:
Shirika la ndege la Uingereza, British Airways, limesitisha safari zake za Italia baada ya nchi hiyo kuwekwa kizuizini hadi mwezi Aprili ili kukabiliana na virusi vya Corona.

Israel: Shirika la ndege la Wizz Air limesitisha safari zake kati ya Israel na Italia ikiwa ni hatua ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ili kukabiliana na virusi vya Corona

Denmark: Waziri mkuu wa nchi hiyo Mette Frederiksen ametangaza kusitishwa kwa safari za ndege kuingia nchini humo kutoka katika mataifa yaliyoathirika zaidi kama vile Italia, Iran na Korea Kusini.

Uhispania: Serikali imetangaza kusitishwa kwa safari za ndege za moja kwa moja kutokea nchini Italia kwa muda wa wiki mbili ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

Ureno: Serikali imetangaza kusitishwa kwa safari za ndege za abiria za kwenda na kutokea Italia kwa muda wa siku 14 kuanzia Jumatano ikiwa ni hatua mojawapo ya kuzuia kuenea zaidi kwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

Canada: Shirika la ndege la nchi hiyo, Air Canada, limesitisha safari zote za kwenda na kutokea Italia hadi mwezi Mei kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa waongo
Ukipiga mahesab ni uongo kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hebu pitia hizi graph kiongozi.....
Screenshot_2020-03-10-22-58-25-353_com.android.chrome.jpeg
Screenshot_2020-03-10-22-58-13-538_com.android.chrome.jpeg
Screenshot_2020-03-10-22-58-00-675_com.android.chrome.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
MPYA: Korea Kusini imethibitisha visa vipya 242 sanjari na vifo vipya sita (6) nchini humo.

Hadi hivi sasa nchini Korea Kusini;
  • Visa 7,755 vimethibitishwa
  • Vifo 60 vimethibitishwa
  • 36 wako katika hali mbaya zaidi
  • 288 wamepata ahueni

hivi korea kusini na russia hili janga limewapita kushoto ama ndio wanasiasa wanaruhusu kutolewa kwa habari wanazozitaka wao tu?
 
UPDATE: China

Visa vipya 15 pamoja na vifo vipya 11 vimeripotiwa na Wizara ya afya ya nchi hiyo hivyo kufikisha jumla ya visa 80,793.

Wagonjwa wapatao 4,257 wako katika hali mbaya zaidi huku idadi ya waliopata ahueni ikifikia 62,793.

Idadi ya vifo nchini humo vinavyohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) imefikia 3,169 hadi hivi sasa.
 
Back
Top Bottom