Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

duh..itali inaitaji msaada watu wanapukutika huko balaa.
 
UPDATE: Wizara ya afya ya China imeripoti visa vipya 20 sanjari na vifo vipya saba (7) huku visa vitano (5) na vifo sita (6) kati ya hivyo vikitokea Hubei pekee.
 
UPDATE: Korea Kusini imeripoti visa vipya vipya 110 pamoja na kifo kipya kimoja (1).

Mpaka hivi sasa nchini humo;
  • Visa 7,979 vimethibitishwa nchi nzima
  • Vifo 67 nchi nzima
  • Wagonjwa 36 wako mahututi
  • Wagonjwa 510 wamepata ahueni
 
UPDATE: Ujerumani

Visa vipya 233 pamoja na kifo kipya (1) kimeripotiwa nchini humo.

Mpaka kufikia sasa, jumla ya visa 2,745 vimeripotiwa nchi nzima ambapo wagonjwa 25 wameripotiwa kupata ahueni huku wengine wawili (2) wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Ujerumani imekwisha ripoti vifo sita (6) nchini humo hadi sasa vinavyohusishwa na virusi vya Corona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…