FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
- Thread starter
- #801
Ni kweli, watu wenye umri mkubwa wamekuwa na kiwango kikubwa cha vifo (fatality rate) na hilo ni kutokana na sababu mbalimbali isitoshe watu wenye umri mdogo sana pia wametajwa kati ya watu walioko hatarini zaidi.halafu mkuu nikifatilia update zako wanaokufa asilimia kubwa wengi ni umri kuanzia miaka 60 kwenda mbele au hujagundua hilo mkuu
ina maana km hvyo wazee wanashindwa kupambana nao unawaathili zaidi
Sent using Jamii Forums mobile app
Sababu nyingineyo, uwepo wa magonjwa mengineyo kwa baadhi ya makundi ya watu yanaweza kusababisha makundi hayo kuathirika zaidi na virusi vya Corona.
Pia, utofauti wa kimwili kati ya makundi ya watu kadha wa kadha kunaweza kuchochea jinsi gani mwili unavyoweza kukabiliana na aina fulani ya magonjwa. Hili linaweza kuchangia pia baadhi ya watu kuwa "Super-spreaders".
Licha ya hivyo, bado pia kuna uwezekano wa kiasilia wa makundi ya watu wenye umri tofauti tofauti kupata athari ama kupoteza maisha kutokana na virusi hivyo ila tu kuna baadhi ya makundi ya watu ambayo yanatajwa kuwa hatarini zaidi.