FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
- Thread starter
- #1,361
Nchini Nigeria, yule mgonjwa mmoja bado yuko katika uangalizi maalumu nchini humo.Vp mkuu kwa nchi za Algeria, na Nigeria kuliporipotiwa visa vya kwanza hakuna update yoyote ya either patients zaidi au recovery ya mgonjwa husika?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna taarifa ya Kamishna wa afya wa Lagos kumtembelea mgonjwa huyo ambaye ni raia wa Italia katika kituo maalumu alikowekwa lakini jambo la kustaajabisha ni kwamba, wakati kamishna huyo ameingia kituoni hapo kuonana na mgonjwa huyo na mpaka kuzungumza naye, hakuwa amevalia mavazi wala vifaa vyovyote vile vya kujikinga na maambukizi jambo lililozua sintofahamu na wasiwasi mkubwa kwa jamii na watu mbalimbali nchini humo huku wengi wakihoji kuhusiana na kitendo hicho cha kiongozi huyo kumkaribia mgonjwa bila ya vifaa vya kujikinga.
Kuhusu Algeria, yule mgonjwa mmoja amerejeshwa nchini kwake Italia na masuala mengine ya kitabibu yanaendelea huko.