Fahamu kuhusu Fao la Kukosa Ajira Tanzania (Unemployment Benefit)

Siku mkija kugundua ya kuwa mafao yenu NSSF N.K Ndiyo yanayotumika kuendesha serikali...mtakuwa mmeshachelewa...

Serikali iliamua kuinganisha hii mifuko kwa sababu hii mahsusi kabisa...

Zama zilishabadilika, ishi,fanya mambo yako yote kwa asilimia 90 ya mshahara unaoupata....hiyo asilimia 10...fanya kama sadaka...

Pia una uwezo wa kuanza kwa mwajiri wako (hr) + benki, hr akaaprove mshahara wako ukatwe 10% nyingine iwe inaingizwa fixed account kwa muda na utaratibu maalum mtakaokubaliana.(mutual Consent/agreement)

Hili pekee ndilo linaweza kumuokoa muajiriwa pindi anapofukuzwa kazi.
 
Kumbe serikali haina pesa hadi inategemea pesa zetu.....!!?

........Basi wapunguze kuvimba.
 
You're Welcome
Mkuu DOMINGO THOMAS naomba kuuliza je maternity benefits ya PSSSF yamesitishwa? Maana nimeomba tokea tarehe 13/11/2024 Hadi leo status inasomeka received by PSSSF. Nimefika kwenye ofisi zao wamesema wamepokea na zimewafikia watafanyia kazi, Ila kimya kingi Hadi leo. Naomba kufahamishwa kama lomesitishwa
 
Elimu nzuri ila hapo tu kwenye "msaada" ndo mgogoro, zile hela ni za mwanachama na si msaada na ikipita miezi 18 unalipwa kiasi ulichochangia na wanatoa hiyo 33% ya mshahara wako waliokulipa miezi 6.
Sahihi, lakini ukipata kazi nyingine mpaka ukastaafu kile kiasi ulicho lipwa hakitotolewa kwenye malipo ya kustaafu
 
Ni kwamba watu watumie mishahara yao kujiendeleza kimaisha, sio kusubiri mafao
 
Maternity benefits ipo na haijafutwa, wanacho takiwa kukuambia ni nini kinasababisha wachelewe kukulipa, Ninacho fahamu kuhusu maternity benefits ni kwamba michango 12 kabla ya kujifungua unatakiwa uwe umechangia kwa mfululizo, je umeangalia statement ya michango yako ipo mpaka mwezi wa kumi na moja.....!?
 
Sahihi, lakini ukipata kazi nyingine mpaka ukastaafu kile kiasi ulicho lipwa hakitotolewa kwenye malipo ya kustaafu
Okay ......hii ela iliniumiza aisee sintosahau yaani nilikuwa apeche alolo 2019 nikatia timu NSSF nikakutana na hii dhahama ya fao la kukosa ajira wakati mie nataka nivute yote. Mwisho wa siku ikabidi nichukue fao la kukosa ajira na nilivyomaliza nikawa napambana nilipwe zilizobaki hata kwa kujifanya mgonjwa lakini wapi, kumbuka kipindi hicho hata staffs wa NSSF hawakuwa na maelezo ya what next ukishalipwa fao la kukosa ajira miezi sita. Nimekuja kugundua kwamba baada ya miezi 18 unalipwa baada ya kusota sana ndo kuna staff akanambia maana wengine walikuwa wanarukaruka the si unajua enzi zile mzee baba Magu alikuwepo.

Nikasubiri miezi 18 nikavuta mkwanja wangu nikaacuana nao
 
Asante kwa kushare experience, pole pia
 
Hesabu ngumu zaidi ya calculus!
 
 
Nilianza kulipwa hiyo 33.3% tarehe 11/12/2024 na nililipwa amount ya miezi miwili. Niliachishwa kazi tarehe 30/09/2024. Baada ya kunilipa hiyo hela ya miezi miwili inachukua muda gani kulipa malipo ya awamu nyingine kwa miezi minne iliyosalia. Nilijua labda wangelipa tena mwisho wa mwezi wa 12 lakini mpaka sasa hivi naona kimya
 
Hapo watakuwa wamekupa ya mwezi wa 11 na 12, I guess walichelewa kuchakata maana kama uliondoka kazini tarehe 30 Sept maana yake huwa inachukua mwezi process yote kukamilika....hivyo kifuatapo hapo utakuwa unalipwa mwezi mmoja mmoja mpaka hiyo miezi 6 iishe
 
Ila PSSSF wao hawafanyi hivyo hawalipi kila mwezi wanakulipa mzigo wote wa miezi 6 kwa pamoja. Kitu nachoona ni kizuri pia.
 
Mkuu DOMINGO THOMAS sorry miezi 18 wanahesabu baada ya kulipwa hiyo 33 ya miezi 6 au inakuaje?
Kwanzia upoteze ajira
Wanahesabu miezi 18 baada ya tarehe ya mwisho kumaliza kulipwa fao la kukosa ajira (mie walihesabu yaani ukifika tu counter anaangalia mwisho ulilipwa lini alafu ana count miezi 18 baada ya kumaliza kulipwa kisha anakupa maelekezo ya kuandika barua pamoja na kuchukua kiapo mahakamani / mwanasheria kudhibitisha huna ajira)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…