Fahamu kuhusu kuanzisha biashara ya Mobile Money (M-Pesa, Tigopesa)

Fahamu kuhusu kuanzisha biashara ya Mobile Money (M-Pesa, Tigopesa)

Hii biashara ni nzur sana ukiwa sehemu nzuri yenye watu wengi,ukiwa na mtaji hata wa mil1 ukizungusha vzr huwezi kukosa laki4 na kuendelea kwa mwezi cha msingi uwe na wateja tuu,ishu sio mtaji mkubwa unaweza ukawa na mtaji mkubwa lkn sehemu uliopo haina wateja wengi utaishia kupata laki1.
 
Na hapo kwenye luku faida yake ikoje?
Hii biashara cha msingi ni location nzuri,ambayo ina movement ya watu, ukiwa na uwezo wa kuhudumia watu si chini ya 50 kwa siku una uhakika wa kupata commision kwa line moja,mfano tigo si chini ya 800000. Upande wa luku nayo ni hivi hivo,ukifanya miamala mingi ya kuuza units mwisho wa mwezi commision inakuwa kubwa
 
Hii biashara iko vizuri sana, mimi mwenyewe ndo kazi yangu, aisee iko vizuri mno,.
 
Hii biashara kumbe ni yakipuuz hiv unacheza na pesa ming kumbe faida kidogo? Nilkuwa naifanyia mpango nianze hebu waliopo kwenye biashara hii endeleen kutujuza
Mi naisi wengi tulikua na ii mipango nilikua nafikiri those mawakala wanapata profit ya kutosha ndomana kila hatua mbili wakala kumbeeeee loooooh
 
shida ya hii biashara pia ni mabukula,nishashuhudia washkaji wangu kama wa3 wakimalizwa mitaji yao na mabukula,yaani mtu anaweka milioni 2 kny account yake,anampa wakala hzo pesa,kesho yake asubuhi hazikuti hizo hela na transaction imeshafanyika,sa si uhanith huu
 
biashara ya uwakala wq tigo pesa, mpesa, airtell money nk inahitaji mtaji wa kiasi gani?
faida yake ikoje katika kila uwakala kwa mfano tigo pesa pekee kwa mwezi inaweza kuwa na faida gani?
 
mada nzuri,ingawa ishawahi jadiliwa hapa jf.lakini kwa kuwa kila zama zina mambo yake ngoja waje wadau wa biashara hizo ili watoe mwanga.
 
Sidhani kama hapo ni kujiajiri. Nionavyo mimi ni kwamba umeajiriwa na Zain (ZAP), Vodafone (M-PESA) na Tigo (TIGO-PESA)
Huyo ni mtu mwenye biashara huru km vile kuuza duka, pale unapo weka bidhaa za baharesa, je hapo umeajiriwa na bahresa?
Muajiriwa ni mtu ambae anapangiwa muda wa kufanyakazi pamoja na malipo, hapo upo huru kufungua na kufunga ofisi yako muda uutakao. Ndg kujiajiri haimaanishi kuanzisha biashara yako pekeyako bila ya mwingiliano na wafanyabiashara wengine.
 
Heshima kwenu,
1. M PESA
2. Tigo pesa
3. Airtel money
4. CRDB fahari huduma
5. Kifaa cha max malipo kwa ajili ya luku etc


jamani ndugu yenu nafikiria kuanzisha hii biashara ya u-wakala wa m-pesa. Mwenye details kidogo kuhusu hii biashara anijuza hasa nataka kufahamu kuhusu;
1. Kiwango cha chini cha mtaji unao hitajika
2. Jinsi faida inavyopatikana
3. Jinsi ya kujisajiri (hili nadhani sio issue sana naweza kwenda kwa voda wenyewe) itanirahisishia zaidi
nawasilisha
======================================================,Mimi ni wakala wa M-Pesa kitambo sana sijawahi tapeliwa,inalipa sana kama tu goli lako lipo sehemu yenye mchanyiko wa watu wengi na kama unaielewa vizuri biashara hiyo.Unahitaji kuwa na laini,TIN na eneo la kufanyia biashara
kumsajili mteja ni Tsh 500/- kamishen
mteja aliyesajiliwa akiweka pesa kwa mara ya kwanza unapata tsh 2000 kamisheni akituma pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh 300/- hadi tsh 5000/- inategemeana ametuma kiasi gani
akitoa pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh500/- hadi tsh 5000/- inategemeana katoa shilingi ngapi
akinunua airtime kwako unapata karibia 10% kamisheni ya airtime aliyonunua
akinunua Luku unapata kamisheni kadhaa
Biashara hii ili ufanikiwe zaidi unaweza kuichanganya na biashara nyingine kama kuuza luku, na vinywaji baridi kama soda na juisi ambavyo havihitaji mtaji mkubwa au kama una biashara yako tayari halafu ukaongezea hii biashara kama ziada

Yaani kwa kijana wa kitanzania wa kawaida akiwa serious inaweza akatolewa na biashara hii kwa ufupi ZAP,M-pesa na Tigo Pesa kama una magoli matatu au maanne kipato cha mwezi ni net 2m, yanini kuajiliwa sasa?
================


Faida yake inategemea yafuatayo:

Ufanisi wako (via Operator) wa kazi;
Kama service ni nzuri hasa in unavyowasikiliza na kuwashughulikia wateja, hii inahusisha mhudumu wako kua haraka na kujua huduma zote.
Mfano: mteja anaweza asijue jinsi ya kutumia akaunti yaM-pesa, hapo ina maana Mhudumu awe mpole amsaidie.

uwe na mtaji wa kutosha ili kuhakikisha mteja akija kutoa au kutuma pesa anapata
hii itasaidia kuptopoteza miamala kwa kukosa pesa na pia itamfanya mteja awe anaiamini sehemu yako hata siku nyingine kuja kwenye banda lako,

  1. Hakikisha jioni unafunga mahesabu pesa yako mkononi na kwenye laini. Kama jumla ilikuwa milioni mbili asubuhi jioni inatakiwa iwe hio hio milioni mbili
  2. Unapata pesa ya commission mwisho wa mwezi. Kama mtaji wako ni Million 5 kwa siku na inazunguka ipasavo na hio sehemu ina shughuli nyingi, kamisheni inaweza fikia hata milioni moja au zaidi
  3. Changamoto

  4. Kama sehemu haina mzunguko wa pesa wa kutosha unaweza kupoteza muda wako, wateja wapo wa kutosha ni nadra kupata hasara. More inakua out of mistakes kama kutuma pesa mahala ambako sio husika kwa bahati mbaya.
  5. Unaweza ukatuma pesa kwa mtu mwingine ambaye sio mteja kwa bahati mbaya, japo pesa hii unaweza kupiga simu kwa vodacom halafu wakarudisha muhamala huo mara nyingine unaweza usiupate kama uliyemtumia atakuwa haraka kwenda kutoa
  6. Noti feki kama kuna wateja wanaweza wakakuletea mabunda ya pesa huku wakiwa wamechanganya na mabunda ya noti feki, kabalaya kuweka pesa kwenye droo yako hakikisha unaziangalia, kama unafanya hadi usiku nunua tube light ili kuwe na mwanga wa kutosha kugundua noti feki.
  7. Kuna vikwazo pia katika biashara hii, na kubwa likiwa ni suala zima la usalama kuna vibaka au majambazi wanaweza wakakutegea ukiwa unatoka wakakukaba, ni bora kuwa na sefu lako imara, kwenye fremu yako pia kunatakiwa kuwe na grili imara kuzunguka dirisha na mlango
Nilikuwa naitafuta sana kujua
 
Daah napata kigugumizi aisee maana majibu yanachanganya kwelikweli
 
Back
Top Bottom