Mimi naifanya biashara hii hapa Dsm, mahitaji ya kupata laini za kazi TIN NO, LESENI YA BIASHARA NA ENEO LA KUFANYIA HIYO BIASGARA pamoja na mtaji.Ili uweze kufanya kazi bila kurudisha wateja wengi kwa kutokuwa na salio unanatakiwa uwe na mtaji usiopungua milioni mbili, na hapa mzunguko wa hela utauona na utaweza kupata kamisheni kubwa.
Mfano kama unafanyia kazi eneo kama kimara mwisho au mbezi mwisho au eneo lingine lenye mzunguko mkubwa wa watu hukosi kamisheni kuanzia laki nne hadi nane kwa mwezi. ANGALIZO, UNATAKIWA UFANYE MIAMALA MINGI ILE KAMISHENI IWE KUBWA KIUJUMLA.
CHANGAMOTO KUBWA KWA SASA Ni kupata line ktk haya makampuni mawili yaani tigo na voda, nakuhakikishia utapeleka document zako pale utasubiri hata mwaka na laini bado hujapata, sanasana utaambiwa utoe laki tatu hadi tano na vishoka wa kule akakutafutie laini zile ambazo wanazifungia kwa mawakala wanaoshindwa kazi
Mimi nina laini moja ya MPESA NAIUZA SH350,000/= Kama unahitaji.
Biashara ni nzuri sana, Faida mojawapo ni urahisi katika uendeshaji usiokuwa na longolongo nyingi kwa mfano, biashara hii hata kama unamuachia majukumu msaidizi ama mfanyakazi, huumii sana kichwa kwani hesabu zake zinajulikana na isitoshe,
miamala yote hurekodiwa kiteknolojia na kampuni husika ambapo huwa rahisi
mwisho wa mwezi au kipindi cha biashara kuja kupewa kamisheni ya miamala iliyofanyika.
Hakuibii mtu hapa. Uzuri mwingine wa biashara hii ya uwakala wa makampuni ya simu ni kwamba, jioni baada ya kufunga kazi mjasiriamali unafahamu mara moja faida
uliyopata katika siku husika kulingana na idadi ya watu na kiasi cha miamala
waliyofanya. Husumbuani na mteja kwenye bei kwani bei zinakuwa zimeshapangwa tayari na makampuni, na hamna shida ya wateja kwani mahitaji ya huduma za kipesa ni mengi na mawakala bado ni wachache nchini.
Kuna vikwazo pia katika biashara hii, na kubwa likiwa ni suala zima la usalama. Ili
kuanzisha biashara hii mahali fulani yafaa kwanza suala la usalama wa pesa na
wewe utakayekaa hapo litiliwe kipaumbele cha kwanza kabisa. Ikiwa ni duka au kibanda basi ni sharti uhakikishe, unajengea grilkuzunguka dirisha na milango ili kuhakikisha hapawi kivutio kwa wezi na majambazi wenye silaha.