Fahamu kuhusu kuanzisha biashara ya Mobile Money (M-Pesa, Tigopesa)

Fahamu kuhusu kuanzisha biashara ya Mobile Money (M-Pesa, Tigopesa)

Nimekuwa najiuliza sana kwanini sasa huduma ya kupiga simu sio muhimu sana kwa makampuni ya simu za mkononi kama vodacom, leo nimekutana na kijana mmoja anayefanya kazi kibanda cha mpesa.

Katika mazungumzo nikamuuliza mgawo wa kipato ambacho mtoa au mfanya biashara wa mpesa hupata kutokana na aina ya huduma na kiwango cha ghalama ambazo vodacom hupata. Huyu ndugu akaniambia mteja akija kutoa 100000 voda hukata 2000 kama gharama ya huduma lakini mwisho wa mwezi vodacom hugawia 800 mtoa huduma ambaye pesa ni zake.

Nikajiuliza maswali kadhaa je kwanini uwiano uko hivi? Lengo la vodacom kunyonya watu kiasi hiki ni nini? Au nalo hili halijulikani kwa wapanga sera na viongozi?

Naomba anayefahamu kwa kina kuhusu hiki atujuze pia akiweza kwa airmoney na tigo pesa
 
Faida kwa mimi mtumiaji:
- Sipangi foleni tena benki au ATM kwa ajili ya kuchukua sh 500,000
- Sipangi foleni ya kununua LUKU au DSTv tena.
- Naweza kulipia bidhaa mbalimbali bila kulazimika kutembea na cash
- Naweza kupokea/kutumia pesa kwa ndugu jamaa na marafiki kwa urahisi zaidi

Hasara:
- Wizi (ukizubaa, unapigwa bao)
- Mizinga na michango imezidi hata kwa watu ambo physically wapo mbali
 
[TABLE="width: 595"]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Transaction[/TD]
[TD="colspan: 3"]Agent commission model (ex VAT)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]From [/TD]
[TD]To[/TD]
[TD]Deposit commission[/TD]
[TD]Withdraw commission[/TD]
[TD]Total commission[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 1,000[/TD]
[TD] 9,999[/TD]
[TD] 200[/TD]
[TD] 300[/TD]
[TD] 500[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 10,000[/TD]
[TD] 19,999[/TD]
[TD] 200[/TD]
[TD] 400[/TD]
[TD] 600[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 20,000[/TD]
[TD] 49,999[/TD]
[TD] 300[/TD]
[TD] 400[/TD]
[TD] 700[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 50,000[/TD]
[TD] 99,999[/TD]
[TD] 400[/TD]
[TD] 600[/TD]
[TD] 1,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 100,000[/TD]
[TD] 199,999[/TD]
[TD] 600[/TD]
[TD] 800[/TD]
[TD] 1,400[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 200,000[/TD]
[TD] 299,999[/TD]
[TD] 800[/TD]
[TD] 1,300[/TD]
[TD] 2,100[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 300,000[/TD]
[TD] 399,999[/TD]
[TD] 1,000[/TD]
[TD] 1,800[/TD]
[TD] 2,800[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 400,000[/TD]
[TD] 500,000[/TD]
[TD] 1,000[/TD]
[TD] 2,500[/TD]
[TD] 3,500[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Registration[/TD]
[TD="colspan: 4"] Tshs 500 once off[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Hayo ndio mapato ya wakala anaye deposit na anaye withdraw. Hapo vodacom wameshatoa sehemu yao. Hii commission inakusanywa unalipwa kwenye simu yako ya head office kila mwisho wa mwezi. Kama upo chini ya wakala mkuu unakatwa 20% anapewa yeye.
 
Faida yake inategemeana na transaction ulizofanya kwa mwezi husika(wenyewe wanaita commission).wanahesabia transaction za kutoa pesa pia za kuweka,zinajumlishwa af wanapga 20%voda,20%wakala wako mkuuand 60%zako.hope umenixoma
 
In short iko hivi,ukiwa unauwezo wa kufanya transaction za watu 50 kwa si zenye wastani wa elfu 60,000/= iwe kutoa au kuweka,kwa mwezi utapata 800,000/= hapo bado za kusajili n.k

Hizo ulizoambia kwamb ktk 2000 Wanakata 800 logic ni kwamba wao ndio wanao lipa kodi,wewe huusiki na kodi yoyote serikali ktk huduma hiyo.

Hivi ndivyo nafahau wengine wanaweza kujazia nyama kidogo
 
Habari zenu wana JF,
mimi bado ni mwanafunzi ila natamani kujijengea msingi wa kuwekeza katika sehemu
mbalimbali kwa kuanza na kidogo nilichonacho.Kuna maeneo ya kwetu hayana huduma ya M-Pesa na nadhani
inaweza ikawa sehemu ya kuanzia endapo nitapata msaada wa kujua ni vitu gani natakiwa kutimiza ili kuwa agent wa M-Pesa.
Natanguliza shukrani kwa kaka/dada zangu wa JF.
 
Mtaji wa kuanzia milioni moja au zaidi...


Wanaitaji pia leseni ya biashara, sijaelewa hii leseni inatolewa na TRA au manispaa?
Naomba ufafanuzi.

Pia nimeambiwa na tigo Pesa kuwa hawapokei tena maombi ya kuwa wakala mpaka October,

Kama kuna mdau wa tigo atujuze isije ikawa ni uongo wa afisa wa tigo niliyeongea nae
 
Sidhani kama hapo ni kujiajiri. Nionavyo mimi ni kwamba umeajiriwa na Zain (ZAP), Vodafone (M-PESA) na Tigo (TIGO-PESA)

Kwa maana hiyo, mkulima ameajiriwa na mlaji, mwenye duka ameajiriwa na wenye bidhaa, seremala ameajiriwa na mteja wake nk. Hivyo msamiati wa kujiajiri hauna maana..
 
Kwa wale wanao taka kufanya biashara ya mpesa please mni pm kwa ajili ya maelekezo zaidi ila kwa awali lazima uwe na

1. TIN number
2. Leseni ya biashara yoyote
3. Kitambulisho chako

Mtaji ni kuanzia laki tano na kuendelea.

Ni bure utapata ilimladi uwe na vigezo tu

Karibuni kwa maswali zaidi
 
...Ni Bure, sasa mambo ya kuku-pm kwanza ya nini? Nadhani utakuwa umefanya jambo jema sana kama utaweka kila kitu wazi halafu mtu aangalie hayo maelekezo na kujipima ndipo akutafute!

Hii pia itakusaidia hata wewe kutojaza In-Box yako kwa maswali ambayo majibu yake ungeweza kuyaweka tu hapa wengi tukafaidika. Ni mawazo yangu tu.
 
Asante mdau kwa taarifa, binafsi nina mpango wa kuanzisha huduma/uwakala wa m-pesa
 
Habari zenu wanaJF. Natumaini wote mko poa. Nimepata wazo la kujiajiri kwa kuwa wakala wa M-PESA na hivyo ningependa kujua ni jinsi gani ntaweza kufaidika kwa hii biashara? Yeyote mwenye mchango wa kimawazo nipevuke anijibu please.
 
Bidii yako ndio faida yako. Unapouza zaidi na kuwa na wateja wengi zaidi ndo faidi inakuwa kubwa zaidi. Tahadhari lakini multiple deposit na direct deposit zitakunyima faida kubwa.

Nimekuwa wakala wa kujitegemea chini ya Vodacom na hadi sasa nina matawi 11 ila kwa sasa huo uwakala wa kujitegemea haupatikani tena labda ujiunge chini ya wakala mkuu ambae atakula 20% ya pato lako.

Kwa maelezo na ushauri zaidi ni pm.
 
Tahadhari lakini multiple deposit na direct deposit zitakunyima faida kubwa.

Kwa maelezo na ushauri zaidi ni pm.

...Nadhani utakuwa umefanya jambo jema zaidi kwa kuweka mambo hadharani ili wengi wafaidike bila kulazimika kuku-pm mkuu! Kwa mfano ukifafanu zaidi hapo kwenye red hata mimi nitafaidika...!
 
Mkuu ukitumia machine za selcom au maximalipo huesabiki kuwa moja ya wakala wa Tanesco. Hao jamaa (selcom na maximalipo) ndio wenye mkataba na Tanesco. walicho fanya ni subcontract kama mkataba wa Tanesco unavyo sema. Yaani Tanesco aliwakubalia selcom na maximalipo to subcontract under one condition. This condition is that lazima wateja wate watakao wa subcontract wauze Luku kwa bei ya Tanesco. Na mkataba unasema wasipo fanya hivyo then Tanesco kama mwajiri wa selcom na maximalipo will cancel their contract. Tanesco wanatoa commission ya 3% sasa selcom na maximalipo their decided to share this profit with their customers. Wale wote wenye machine za maximalipo na selcom wanapata 1.5% na wajiri wao wanabakiza 1.5%. There4 ukizingatia hayo utajikuta kwamba unawafanyia kazi selcom au maximalipo.
Nivyema kwenda Tanesco kwa marketing manager Mr Mzava (huyu jamaa nimzuri sana) atakupa maelezo. Na kwa vile uko Dar atakwambia maeneo gani ambayo wanaitaji mawakala. Ukisha pata huo uwakala pia unaweza kufanya kazi kama selcom or maximalipo. Kuna routers za 3G unaweza kutumia moja kwenye 50 POS kama za maximalipo. ila hii router bei yake iko juu sana lakini inafanya kazi nzuri sana. Hutotakiwa kuingia gharama kama za maximalipo au selcom.

Mkuu, naomba unijuze zaidi jinsi ya kupata hiyo 3G router
 
Kwa maana hiyo, mkulima ameajiriwa na mlaji, mwenye duka ameajiriwa na wenye bidhaa, seremala ameajiriwa na mteja wake nk. Hivyo msamiati wa kujiajiri hauna maana..

Yaani anakusudia kuwa siku wakala wa mpesa akiamua kutokwenda bandani kwake mpaka aombe ruksa vodacom vinginevyo atapoteza ajira yake.
 
umenifungua macho sana. je niandae kama shilingi ngap as start up? na naweza nkaweka bishara nyingine zipi ktk hilo banda la e-money?

Andaa 1 milion kwa mtaji wa MPesa na Tigo pesa 1 Milion, kisha tafuta Fridge la vinywaji na watu siku hizi wanapendelea yale mafrige ya kioo ambayo mteja anona drinks zikiwa ndani ya fridge kisha anachagua kinywaji atakacho
.
Nakushauri ukiisha pata hiyo mitaji na Fridge usisahau kununua TUBE LIGHT YA KUANGALIZIA KAMA NOTE NI HALALI AU FAKE -Ni muhimu sana mimi nimeuza line yangu ya Mpesa baada ya kijana wangu kumuwekea mtu hela LAKI 4 NA SITINI ELFU , kwenye simu yake zikiwa zangu ni halali na akanipa note za Elfu kumi laki nne na sitini elfu. NIKAACHA HIYO BIASHARA SO INABIDI UWEKE BUDGET YA HIYO TUBE LIGHT
 
Kwa mawakala wa M-pesa, Tigo pesa, Airtel money na Ezy pesa. Naombeni msaada jamani nataka nifungue ofc ya M-pesa lkn nimeambiwa kwa sasa vodacom hawatoi Till number mpya. Lkn kwa bahati kuna mtu kasema anaweza akanipa line yake nitumie, sasa naombeni kwa wataalamu mnielezee utalaamu wa hii kitu hasa faida na masharti mengine kwa faida yangu na ya wenzangu pia.
 
Back
Top Bottom