Kwanza
Mfanyakazi atakuoiga kama siyo wewe mwenyewe unayehamishia wateja pesa. Wafanyakazi wanasajili line wanakuwa wanatoa hudumu wewe line yako haifanyi kazi kabisa.
Pili,
Makapuni ya Simu wanakuibia ile Commission, hawakupi kama ukivyotakiwa kupewa.
Tatu,
Unakaribisha panya road na mbwa mwitu maana, wanasasambua sana humo kwenye vibanda hasa huku dar nasikia ni kawaida.
Nne,
Faida yake nasikia siyo kubwa kiviile, yaani usitarajie miujiza ya kipato kupitia hiyo biashara faida yake siyo kubwa na hasa ukirejea namba hizo juu zote zinasababisha faida kuwa ndogo.
Tano,
Kama una pesa ya mawazo na hesabu Kali. Usitarajie faida ndani ya siku au wiki ni uwekezaji unaohitaji mtu mvumilivu na aliye na vyanzo vinginevyo vya mapato.
Wengine watakuongezea mambo mengine maana, nami hayo yote nimeyasoma umu humu JF kuhusu uwekezaji.
Nikutakie uwekezaji mwema.