Fahamu Sifa kuu za Muislamu ni pamoja na kujizuia, uvumilivu, kusamehe, huruma na hawana woga wa kusema ukweli tuifate dini ya mwenyezi Mungu

Fahamu Sifa kuu za Muislamu ni pamoja na kujizuia, uvumilivu, kusamehe, huruma na hawana woga wa kusema ukweli tuifate dini ya mwenyezi Mungu

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Hizo ndizo sifa kuu za Muislamu
Uslamu ndiyo dini ya haki duniani kote


Ni wenye akili. Daima wapo makini, kwa sababu wana ufahamu wa ibada zao. Daima huwahudumia waumini na dini kwa kutumia akili. (al-Mumin, 40/54; az-Zumar, 39/18)

Ni wenye kupambana kiakili kwa nguvu dhidi ya wakanushaji kwa ajili ya Allah. Hususan wakanushaji wakubwa. Huendelea na mapambano yao bila ya hofu wala uvivu. (al-Anfal, 8/39; al-Hajj, 22/78; al-Hujurat, 49/15; at-Tawba, 9/12)

Hawana woga wa kusema ukweli. Hawana hofu ya kuuweka wazi ukweli kwa kuhofia watu. Hawaogopi wakisemacho wakanushaji dhidi yao; hawapuuzi mashambulizi na dhihaka zao; Hawaogopi kukosolewa na wale wenye kuwalaumu. (al-Maida, 5/54, 67; al-Araf, 7/2)

Kufikisha dini ya Allah kwa watu. Ni wenye kuwaita watu katika dini ya Allah kwa kutumia njia tofauti. (Nuh, 71/5-9)

Si madhalimu. Ni wenye huruma na huathirika na shida za wengine. (an-Nahl, 16/125; at-Tawba, 9/128; Hud, 11/75)

Ni wenye kujizuia na hasira; ni wenye uvumilivu na kusamehe. (Aal-i Imran, 3

waaminifu. Huonyesha utu wenye nguvu na husifika kwa kujiamini. (ad-Duhan, 44/17-18; at-Takwir, 81/19-21; al-Maida, 5/12; an-Nahl, 16/120)

Wanaumizwa na ukandamizaji na ukatili. (ash-Shuara, 26/49, 167; al-Ankabut, 29/24; Yasin, 36/18; Ibrahim, 14/6; an-Naml, 27/49, 56; Hud, 11/91)

Ni wenye kuvumilia shida. (al-Ankabut, 29/2-3; al-Baqara, 2/156, 214; Aal-i Imran, 3/142, 146, 195; al-Ahzab, 33/48; Muhammad, 47/31; al-Anam, 6/34)

Hawana hofu na dhulma pamoja na umauti. (at-Tawba, 9/111; Aal-i Imran, 3/156-158, 169-171, 173; ash-Shuara, 26/49-50; as-Saffat, 37/97-99; an-Nisa, 4/74)

Ni wenye kupambana na mashambulizi na vitimbi ya wakanushaji. (al-Baqara, 2/14, 212)

Wapo chini ya himaya ya Allah. Vitimbi vyote dhidi yao hushindwa. Allah huwafanya washindi kwa kuwahami dhidi ya uzushi wote na vitimbi. (Aal-i Imran, 3/110-111, 120; Ibrahim, 14/46; al-Anfal, 8/30; an-Nahl, 16/26; Yusuf, 12/34; al-Hajj, 22/38; al-Maida, 5/42, 105; an-Nisa, 4/141)

Ni wenye umakini mkubwa dhidi ya wakanushaji. (an-Nisa, 4/71, 102; Yusuf, 12/67)

Ni wenye kuwafanya maadui shetani na wafuasi wake. (Fatir, 35/6; az-Zukhruf, 43/62; al-Mumtahina, 60/1; an-Nisa, 4/101; al-Maida, 5/82)

Ni wenye kupambana na wanafiki; hawautumii muda wao pamaja nao. (at-Tawba, 9/83, 95, 123)

Ni wenye kujikinga na udhalimu wa wakanushaji. (al-Ahzab, 33/60-62; al-Hashr, 59/6; at-Tawba, 9/14-15, 52)

Ni wenye kufanya mambo yao kwa kushauriana. (ash-Shura, 42/38)

Hawana wivu au kuiga maisha ya kifahari ya makafiri. (al-Kahf, 18/28; at-Tawba, 9/55; Taha, 20/131)

Hawaathiriki na utajiri na cheo. (al-Hajj, 22/41; al-Qasas, 28/79-80; an-Nahl, 16/123)

Ni wenye uangalifu na umakini kuhusu ibada; wanatekeleza sala, funga na ibada kwa uangalifu. (al-Baqara, 2/238; al-Anfal, 8/3; al-Muminun, 23/1-2)

Hawafuati wingi bali vipimo vilivyowekwa na Allah. (al-Anam, 6/116)
 
Kupambana kwa ajili ya Allah?
kivipi yan?
Yaani Mnampigania Mungu wenu akiwa yeye yuko hoi hajiwezi?
 
Uislamu ungekua hivyo dunia ungekua sehemu salama Ila hapo Kuna mengi hujadadavua
 
Uislamu ungekua hivyo dunia ungekua sehemu salama Ila hapo Kuna mengi hujadadavua
Unahukumu uislamu kupitia wachache ambao wanajinasbisha na uislam lakin uislamu hauwatambui hebu ufuatilie uislamu wenywe kwanza utajua nani wa kweli na wakina nani wamejichomeka, salama ya maisha yako na dunia kwa ujumla ni kufuata dini ya haqq uislamu.
 
Muogope muumba wako na usisahau kuwa kwake utarejeshwa, mungu ni mwenye upendo na sio upendo
Allah akuongoze
Watakao nielewa ni wachache Tena wasio wadini kama wew mkuu, usicho kijua nikwamba dini ni njia ya kumjua Mwenyezi MUNGU, lakini MUNGU ameweka njia zake za kumtafuta.

Alafu kingine wew ndio umuogope MUNGU Kwa kuandika jina lake Kwa herufi ndogo.
 
Kupambana kwa ajili ya Allah?
kivipi yan?
Yaani Mnampigania Mungu wenu akiwa yeye yuko hoi hajiwezi?
Hicho ni kipimo chake allah
Kuwabainisha wakweli na waongo

أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ ﴿٢﴾

2. Je, wanadhani watu kwamba wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini, nao ndio wasijaribiwe?


وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ ﴿٣﴾

3. Kwa yakini Tuliwajaribu wale wa kabla yao. Na kwa yakini Allaah Atawatambulisha wale walio wakweli, na kwa hakika Atawatambulisha walio waongo.

سورة العكبوت
 
In Arabic , 'arab means " inhabitants of the desert". Waarabu walipangiwa na Mungu wakae jangwani ambapo hakuna chemchemi za maji .
 
Unahukumu uislamu kupitia wachache ambao wanajinasbisha na uislam lakin uislamu hauwatambui hebu ufuatilie uislamu wenywe kwanza utajua nani wa kweli na wakina nani wamejichomeka, salama ya maisha yako na dunia kwa ujumla ni kufuata dini ya haqq uislamu.
Wewe unafkiri Mimi n mwepesi katika elimu ya uislam la hasha unajidanganya nauelewa nzuri? Ila wewe umekuwa programmed tyr pambania tu uione pepo
 
Back
Top Bottom