Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Hii kitu naona mafundi wameshaachana nayo mda sana, niliona jamaa mmoja akifitisha geti ndio alikuwa anatumia sana kuweka level, na ni very precise!!!
kama huna dumpy level hiyo ni good option esp. kwa mafundi wetu wa uswazi
 
hawa wanaandaaga boq kiumtaani errors zinakuwa kubwa
Mkuu mm ni fundi nilioko field, nikiona mchoro na nikakiona kiwanja, hua najua mpaka idadi ya misumari itakayo tumika. Kama unavyojua lengo la BOQ nikumjulisha client idadi ya material .
 

Hongera kwa elimu uliyoitoa kuhusiana na baadhi ya mambo ya msingi kuhusu ujenzi.Asilimia kubwa ya watu wanaogopa kuanza ujenzi moja ya sababu ikiwa ni kukosa uelewa kuhusu mchakato mzima wa ujenzi.

Mbali ya elimu ya darasani,elimu itokanayo na uzoefu kazini ni muhimu sana jambo ninaloliona kwako. Japo baadhi wameonekana kukushambulia ila kwa mtazamo wangu uzoefu ulionao ni muhimu sana hasa hasa katika fani ya ujenzi.
Ushauri wangu kwako ni kuendelea kujielimisha kwani kutokana ukuaji wa teknolojia zipo mbinu mpya za ujenzi zenye kupunguza gharama za ujenzi.

Ushauri wangu kwa wanaotarajia kujenga na wataalam wa ujenzi, wasifanye mambo kwa mazoea kwani zipo style nyingi za ujenzi zenye kutumia gharama ndogo kwa mfano matumizi ya interlocking block,semi prefabricated slab(hii ni aina mpya ya ujenzi wa slab(jamvi) yenye kutumia nondo kidogo na zege kidogo bila kuathiri ubora).

Pia ningependa kushauri wengi wetu tujenge tabia ya kuwatumia watalaamu katika hatua za mwanzo kabla ya kuanza ujenzi. Tumia wataalam kupata ushauri na wakuandalie ramani kulingana na mahitaji yako kwani hii inaweza kukusaidia kupunguza gharama zinazoweza kujitokeza baadae.

Mwisho kabisa kwako fundi naomba unieleweshe tiles nzuri zenye ubora ni zipi? Bei yake ikoje? Na katika box moja zinakuwa tiles ngapi na size gani?

Ahsante.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Well explained, ila in some cases beams inawezekana kutumia nondo 3, mbili chini na moja juu zikizungushiwa stirups.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu ubora wa tiles inategemeana na toleo. Mfano kuna tiles za china ni imara na zimenyooka sana ,huwa hazipauki. Pia Kuna za kichina zinazopauka mapema. Tiles ambazo mara nyingi za uhakika ni za spain ambazo bei yake huanzia @45000 kwa box.
Kuhusu idadi ya tiles kwa box inategemeana na size (ukubwa) wa tiles . Cha Msingi angalia coverage area ya tiles kwa box. Mfano kunazinazo cover Sqm 0.6 - 1.5sqm
 

Ahsante mkuu, kwa hio bei ya 45,000/=@box inaweza kucover sqm ngapi? Iwapo size ya tile ni 60cmx60cm au size nyingine?




Sent using Jamii Forums mobile app
 
upana wa bati linalotoka nje ya ukutu,vipimo standard vya kwenye ramani ni fut 2 hadi cm 80 na kwenye gables isipungue futi moja na isizidi cm 50
 
Kweli japo Mimi siyo mtaalamu wa ujenzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna sababu kadhaa but ni ngumu kupata specific cause lakini kiujumla husababishwa na mchanganyo kua laini sana au kulikua na vumbi so wakati inakauka itakua na ile contraction and expansion kutokana na joto,pili maji machafu au ratio ya cement kuzidi au kupungua nk nk but kitu muhimu mchanga usiwe na vumbi na usiwe rojo sana pia plaster au zege lisimwagwe wakati wa jua kali na curing iwe mda wote
 
Na wanaotumia mkaa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gharama inategemeana na ukubwa wa Jengo, aina ya udongo unapojenga, Kuna slop au tambalale na mkoa unaojenga.
Je kwenye jengo la ukubwa huu gharama itakuwaje?
Vyumba vya kulala vitano.
Sebule mbili @ chini na juu
Location: village
Aina ya udongo mixed sand and clay

Landscape. Tambarare



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akijibu haya nami nitajifunza mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok. Shukrani kwa maelezo mazuri mkuu. Ukifanya skimming kama nyufa za aina tajwa hapo juu zilikuwepo kwenye plaster zitaendelea kutokea?. Kama curing process ilisha isha?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…