Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Beam ni Mkanda wa zege + nondo uliopo chini ya mlango na dirisha wakati lintel ni ni Mkanda wa zege + nondo Ambao Upo juu ya dirisha na mlango
Samahani mkuu naomba niingilie mada yako
Beam yapasa kutamkwa Ring beam
Hivyo tofauti ya linter ni zege lenye chuma ila linawekwa kwenye uwazi wa milango ,madirisha na n.k
Na ring beam ni zege lenye chuma ila linawekwa kwenye mzunguko wa jengo lote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona mmeanza kutuchanganya ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boss jaribu kufanya utafiti kidogo, hizo nyumba zenye chimney mara nyingi huwa wanatumia kuni as a source of energy, sasa kwa nyumba zetu hizi nani anatumia kuni ndani!?, nafikiri zile kitchen ventilation za umeme ndio zinatufaa zaidi ya traditional chimneys.
 
Vyovyote utakavyoiita kitchen ventilation au chimney kwanini wachoraji wa ramani hawaziweki? Structure engineer pia hawaweki nani aweke?!Unapika, ndani moshi
 
Vyovyote utakavyoiita kitchen ventilation au chimney kwanini wachoraji wa ramani hawaziweki? Structure engineer pia hawaweki nani aweke?!Unapika, ndani moshi
Boss shida yako ni nini, mtu ndani ana jiko la gas, je huo moshi utatokea wapi, ndio maana nakuambia kwa nyumba zetu hizi za kibongo, air vent ndio mzuri na kuhusu mchora ramani kuiweka kwenye plan sio kitu cha ulazima, mbona mfumo wa umeme hauwekwi pamoja na mchoro wa nyumba!?.
 
Uko sahihi sana nadhani ni kijana mwenye nia nzuri na anayependa na kujali kazi yake,
na mara nyingi hawa wenye uwelewa kiasi wana confidence kubwa sana kuliko wale wenye uwelewa wa juu hawa wa higher education, naomba tumtie moyo na naamini atafika mbali sn.

Itashangaza kwa kusema ukweli kwamba SIO RAHISI Qualified Engineer kujitokeza wazi kwenye public kama hivi na kuelezea taaluma yake kinagaubaga hivi,
kwanza anawaza risk involved pili kila point ina walakini na sababu kibao mwisho kukosa kabisa kujiamini aidha kuogopa kudharirika, hayo ndio moja ya madhara ya elimu yetu ya juu TZ theory nyingi sana mwisho uoga practical ZERO.
 
Vipi kuhusu kujenga ghorofa?
Nazungumzia kuhusu msingi za slab na nguzo. Gharama, utaalamu wa kuzingatia, faida?

Kifupi kabisa natamani kujua mambo muhimu ya kuzingatia katika kupunguza gharama, kuepuka makosa na mbinu nzuri za ujenzi wa nyumba ya kawaida ya makazi ya ghorofa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…