Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Gharama inategemeana na ukubwa wa Jengo, aina ya udongo unapojenga, Kuna slop au tambalale na mkoa unaojenga.
 
Gharama inategemeana na ukubwa wa Jengo, aina ya udongo unapojenga, Kuna slop au tambalale na mkoa unaojenga.
Kurahisisha maelezo ili kutoa mwangaza wa hili jambo, tuchukulie haya mambo.

-Mkoa Dar.

-Udongo ni kichanga.

-Eneo ni tambarare.

-Ukubwa wa jengo ni square meter225(15m×15m).

-Nyumba ni ghorofa moja.

-Paa litaezekwa kwa Slab.

-Mtindo wa nyumba ni vyumba viwili(kimoja master), sebule, Public toilet na Kitchen, vitu vyote vitakuwa kwenye kila floor, kama ujenzi wa apartment hivi. (Hivyo ground floor itakuwa hivyo, na 1st floor itakuwa nayo hivyo hivyo). Hakuna complication, muundo wa kawaida au kizamani!!

-Ngazi inategemea, ama ziwe ndani kuunganisha ground floor na 1st floor au ziwe nje kuondoa mwingiliano kati ya ground froor na 1st floor)


Nimekupa picha hapo.

Nadhani ufafanuzi wako utakuwa na manufaa kwa watu wengi ambao wana viwanja vidogo lakini maeneo mazuri au kutaka kubadilisha fashion za ujenzi. Na hilo ndio lengo langu na kwa kuwa nimeona picha hapo juu katika huu uzi ukisimamia kazi ya ujenzi wa ghorofa, nikavutiwa kuuluza hayo.
 
Ok sawa
 
Wakati naandaa mchanganuo wa items budget yako isipungue 260mil. Nitakuja na mchanganuo wake
 
sio hayo tu unakuta mafundi wamewashauri wateja wao wamejaza manguzo unnecessary kwenye nyumba wakat hakuna uzito wowote zinabeba,kupaua kwa kuinua mapaa mwisho wa siku gharama znakua juu sana yaan mafundi ni jipu
 
afu unakuta wanalaza nondo labda mbili ndo zege inafuata bila hata kuweka stirrups sasa unauliza ya kaz gan eti inazuia nyufa,buree kabisaa
 
sio hayo tu unakuta mafundi wamewashauri wateja wao wamejaza manguzo unnecessary kwenye nyumba wakat hakuna uzito wowote zinabeba,kupaua kwa kuinua mapaa mwisho wa siku gharama znakua juu sana yaan mafundi ni jipu
Wala hujakosea boss. Maisha yako hivi "mtoa huduma anakutana na changamoto nyingi wakati wa kutoa huduma wakati huohuo mpokea huduma naye anakutana na changamoto nyingi wakati wa kupokea huduma.
 
Wakati naandaa mchanganuo wa items budget yako isipungue 160mil. Nitakuja na mchanganuo wake
Pamoja na kutokuwa na ramani husika. 160 ni ndogo. Nina uzoefu wa kutosha na kazi hizi. Kazi hiyo inahitaji 400m +,

Lakini pia kwa mwenye kazi hiyo Bora awaone wataalamu kwa ushauri zaidi. Maana vipimo hivyo vya jengo la 15 x 15, ni kama jengo flani ambalo linaweza lisiwe na mvuto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wataalam, ukiona tu vipimo vya jengo, unaanza kupata picha ya namna ya mwanga utakavyoingia kwenye jengo, hewa( air circulation), na aunthetics/ mvuto wa jengo. Pamoja na hayo. Ukipauwa kwa kutumia zege, utambue kuna gharama kubwa ya waterproofing kwenye hiyo zege. Kwa mfano ukitumia kryton,krystol, MoyaShield au Organix Zina gharim si chini ya 50,000 kwa square meter moja ya mraba.

Kwa Hilo jengo itakuwa 225 x 50,000=11,250,000

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila zipo products nzuri na bora pia za w/proof za bei ya chini. Ulishawahi sikia neno SIKA?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…