Nimechanganyikiwa mana nimepasukiwa na condom wakati tukifanya mapenzi ikabidi tukapime nikakuta kumbe mwenzangu ana VVU wamenipa dawa PEP. Imetokea leo asubuhi hayajapita masaa 24 nimemeza PEP
Je kweli zitanikinga?
Update
======
Nimepima tarehe 6/10/2017 nipo HIV negative, nina furaha saana maana nilitembelea rim, nimejifunza jambo kubwa saana katika maisha yangu....
================================
Ilivyokuwa
====!!!!!=====
Alikuja kunitembelea toka mkoani tarehe 21 June 2017, tunagegedana kwa kinga, siku hiyo ya tarehe 21 mara mbili kisha tukalala, Asubuhi kabla sijatoka tunagegedana, nikiwa nakaribia kufika climax condom ikapasuka, nikamalizia, Nilipomaliza nikapata hofu maana sikuwa najua status yake.
Nikamwambia tukapime alikubali tukaenda hospital kupima. Nikaona ana hofu japo amekubali ikabidi nisisitize kwenda ,tukaenda dispensary kupima.
Tulipofika tukatoa damu tukaambiwa tusubiri, Baada ya dakika 10-15 akaitwa akatolewa damu tena. Nikaanza kupata hofu.
Muda wa majibu ulipofika tukaitwa, kufika ndani baada ya mazungumzo na yule mtoa Ushauri yaliyodumu kwa nusu saa akauliza mpo tayari kupokea majibu!? Tukasema ndio, akasema "kaka hongera sana majibu yako ni mazuri hauna maambukizi, Dada unaishi na maambukizi ya virus vya UKIMWI".
Nikajieleza juu ya mkasa wa kupasukiwa na condom, wakanipa dose ya pep for 28 days.
Hizo dawa ni kali vibaya mno, zinalevya hatari yaani Unachoka unajihisi kuumwa, mawenge na ndoto za ajabu ajabu kila siku. Asee asikuambie mtu ni dawa strong sana.
Yule binti alikataa kuanza clinic, akadai yeye Si Mgonjwa hana maambukizi