Faida 04 za kijana kuoa ukiwa na miaka 20

Faida 04 za kijana kuoa ukiwa na miaka 20

Mkuu, miaka 20 utaoa utamlisha nn mtoto wa watu? At least miaka 28 hiv hapo utakuta mtu anaweza kuingiza hata 800k na kuendelea,
Unaoa hata geto huna microwave 😂😂😂
 
Mkuu, miaka 20 utaoa utamlisha nn mtoto wa watu? At least miaka 28 hiv hapo utakuta mtu anaweza kuingiza hata 800k na kuendelea,
Unaoa hata geto huna microwave 😂😂😂
😁😁 acha uoga. Umri hauna uhusiano na kupata kipato. Kama sio brainwashing za shuleni na media. Miaka 20 anaweza kuwa na biashara kubwa tu za kuuza hizo microwave sio tu kumiliki.
 
Nilipata mtoto wa kwanza nikiwa na miaka 23 nikiwa chuo, nilipata changamoto kipato😂

Ila now naangalia dume zangu mbili daaah nafarijika sana🙏🙏

Natumaini nikifikisha miaka 45 nitakuwa na vijana waliomaliza vyuo vikuu ikiwa watapita salama
 
Ukio na umri kuanzia 20-25 hiyo ndoa Ina asilimia 70 za kuvunjika na ukioa ova 35 hiyo ndoa Ina asilimia 50 za kuvunjika
Babu yangu alioa akiwa na miaka 22, akiwa ni meneja na anashindia suti.
Hadi leo wako na mke wake japo alipitia misukosuko yq mahusiano. Hiyo ilikiwa miaka ya 1940s.

Awazavyo mtu moyoni mwake ndivyo alivyo. Ukiwaza kuachika utaachika, akili inakaa standby kwa devorce ukiwa na mentality za kusherekea mapenzi ya ndoa utaishi miaka mingi tu bila hizo kero.

Hapo ni uchaguzi wa waoanaji
 
Wahenga wa jamii yangu wana msemo unasema " Kuoa na kuolewa ni ujanani na mali unaipata ukiwa na nywele nyeupe kichwani". Kwa tafsiri ya haraka ni kwamba unatakiwa kuona na kuolewa mapema bado ukiwa kijana mwenye nguvu ili uweze kusukuma majukumu ya malezi mapema then katika umri wa makamo unatafuta maliza za ziada huku ukiwa umemaliza majukumu ya malezi. sasa kama utachelewa kuoa hutaweza kuwa na nguvu za kutafuta mali baada ya kumaliza majukumu ya malezi maana utakuwa umezeeka.

Namuunga mkono mleta hoja.
 
Nilipata mtoto wa kwanza nikiwa na miaka 23 nikiwa chuo, nilipata changamoto kipato😂

Ila now naangalia dume zangu mbili daaah nafarijika sana🙏🙏

Natumaini nikifikisha miaka 45 nitakuwa na vijana waliomaliza vyuo vikuu ikiwa watapita salama
Ni hofu tu, ungeoa kabisa. Mimi nilipanga kuoa 22 muolewaji ndio alikuwa na wenge akapoteza hiyo fursa ikaangukia kwa mwanamke mwingine miaka michache baadae. Ila hiyo ni moja ya majuto yangu katika documentary ya maisha yangu. Kuchelewa kuoa nikiwa na miaka 22.
 
Kijana wa miaka 20 anaoa binti wa miaka mingapi? Lets assume 18. Huyu binti hapa anaolewa akiwa hajui anataka nini sasa
Kwa dunia ya leo ya uhuru wa mtoto wa kike binti akifika miaka 23 amenawiri yupo na minyama nyama na kijana atakuwa na 25 itokee ana kipato cha kawaida Kuilinda hii ndoa isivunjike kunahitaji miujiza ya hali ya juu sana.
 
Kwa familia makini. Mzazi hatafuti mali kwa ajili yake tu. Anatakiwa kutafuta hadi kwa wana wa wana wake (wajukuu) ili kuwaboost kuwapa kianzio cha maisha ili wao wasonge mbele.

Kwa umri huo pia anatakiwa kuwa ameivishwa na kuwa na uwezo wa kuingiza kipato. Haihitaji degree ndio upate hela za kulisha mke. China kuna mabilionea wengi sana under 22.

Ni mindest za umasikini tu ndio zinatupa hii hofu dhaania.
Mazingira ya Bongo unalinganishaje na China Wewe ?
Huu umasikini humu Bongo na mifumo mibovu ndio unafikiri mtu anaweza kuwa bilionea kwa umri huo ?
 
kwa kusoma kama ulivoandika look so simple but in reality tunadanganyana why?

1. MATURITY
Umri wa miaka 20 kwa mtoto wa kiume anakua maturity "physical" but not ""Mentaly so hawezi kuhimili mikiki ya ndoa.
Umri wa Miiaka 20 tunategemea aoe kijana wa kike wa miaka 20 au chini ya hapo ambao kimtazamo akili zao wote hawa ni za kitoto bado hawawezi kupambanua mambo katika upana wa kufanya ndoa iwe "STABLE" matokeo ni kesi za kupigana, kuchitiana na utoto toto mwingi mwisho wa siku kuwapa mzigo wazazi hata kuachana.

2. ECONOMIC STABILITY
Kwa asilimia kubwa kwa vijana wengi wa kiume umri wa miaka 20 ndo kwaanza wapo chuo au wanajitafuta ukiachiliana mbali kupima uwezo wao wa kufua nazi kupimia nyenzo tofauti tofauti i mean wako PEAK in sexual drive...So my point is ni ngumu kukuta yupo kiuwezo kifedha wa kumtunza MKE na watoto kwa jamii yetu kama hii ya KITANZANIA.

3. LIFE EXPERIENCE and EXPOSURE
hahaha nimecheka kwa kuwa najua kuna watu wanaweza kuona kama sio point ya msingi lakini ina umuhimu wake..Taasisi ya ndoa kwa kijana wa kiume wa kitanzania ili uindeshe vizuri basi lazima uwe umepitia changamoto mbalimbali za kimaisha na kuweza kuzibakabili kimwili,kiakili na hata kiroho kuna kauzoefu flani lazima upate utaopima ujasiri na uwezo wa kutatua mambo kwenye maisha, sasa kwa kijana wa miaka 20 HAHAHAHA Ndo kwaaanza wengi akili zao zinakua zipo stage1 of maturity ni shida tupu alafu uje umpe ndoa asee ni vichekesho.

CONCLUSION
Kwangu mimi BIG NO kwa misingi na mifumo ya jamii zetu za kiafrika miaka 20 kwa kijana wa kiume kuingia kwenye NDOA.
 
Inatafuta hela kwa ajili ya legacy yake na aombe kupata watoto wakuiendeleza
 
Mazingira ya Bongo unalinganishaje na China Wewe ?
Huu umasikini humu Bongo na mifumo mibovu ndio unafikiri mtu anaweza kuwa bilionea kwa umri huo ?
Nimeenda usukumani watu wanaoa hadi na miaka 18, chini ya uangalizi wa jamii bado watoboa hadi uzeeni.

Ishu ni mindest na hofu tu.
 
kwa kusoma kama ulivoandika look so simple but in reality tunadanganyana why?

1. MATURITY
Umri wa miaka 20 kwa mtoto wa kiume anakua maturity "physical" but not ""Mentaly so hawezi kuhimili mikiki ya ndoa.
Umri wa Miiaka 20 tunategemea aoe kijana wa kike wa miaka 20 au chini ya hapo ambao kimtazamo akili zao wote hawa ni za kitoto bado hawawezi kupambanua mambo katika upana wa kufanya ndoa iwe "STABLE" matokeo ni kesi za kupigana, kuchitiana na utoto toto mwingi mwisho wa siku kuwapa mzigo wazazi hata kuachana.

2. ECONOMIC STABILITY
Kwa asilimia kubwa kwa vijana wengi wa kiume umri wa miaka 20 ndo kwaanza wapo chuo au wanajitafuta ukiachiliana mbali kupima uwezo wao wa kufua nazi kupimia nyenzo tofauti tofauti i mean wako PEAK in sexual drive...So my point is ni ngumu kukuta yupo kiuwezo kifedha wa kumtunza MKE na watoto kwa jamii yetu kama hii ya KITANZANIA.

3. LIFE EXPERIENCE and EXPOSURE
hahaha nimecheka kwa kuwa najua kuna watu wanaweza kuona kama sio point ya msingi lakini ina umuhimu wake..Taasisi ya ndoa kwa kijana wa kiume wa kitanzania ili uindeshe vizuri basi lazima uwe umepitia changamoto mbalimbali za kimaisha na kuweza kuzibakabili kimwili,kiakili na hata kiroho kuna kauzoefu flani lazima upate utaopima ujasiri na uwezo wa kutatua mambo kwenye maisha, sasa kwa kijana wa miaka 20 HAHAHAHA Ndo kwaaanza wengi akili zao zinakua zipo stage1 of maturity ni shida tupu alafu uje umpe ndoa asee ni vichekesho.

CONCLUSION
Kwangu mimi BIG NO kwa misingi na mifumo ya jamii zetu za kiafrika miaka 20 kwa kijana wa kiume kuingia kwenye NDOA.
Anaweza maisha nikufanya na sio kujaribu . Rafiki yangu wa sasa kakijana tu kanaitwa dogo ameoa 18 mke ana 17 wote walianza maisha hayo hapa mjini na wote waliajiriwa kama wafanya usafi wa kaanz akodogo kidogo wakasave sasa hivi wana kimgahawa chao kinaingiza ml 3 kwa siku kama hutaki acha wanapika chipsi kuanzia saa sita mpaka sanane usiku na amewaakiri wafanyakazi wakumsaidia kupeleka chipsi kutengeneza kachumbari hadi now mwenzako sio yeye . Maisha sio yakuogopa na uchaguzi
 
Watu wapo class

Na wengi tegemeo ni heslb
Wala hakuna tatizo, kwani wataishi maisha hayo hayo.

Tatizo ni mafunzo mabaya tunayowapa watoto pengine toka kwa wazazi au kwenye mitandao juu ya ueleo wa maisha. Kijana hataki kuoa mpaka ajiandae. Na kujiandaa kwa tafsiri ya mitandao inamaanisha awe na mjengo pengine na gari na kazi ya maana ya kuajiriwa. Wengine hutamka kabisa kuwa siolewi na mwanaume aliyeajiriwa serikalini katika kazi "A" au "B". Hizi ni fikra mbovu!

Anzeni maisha pamoja, mkiwa na kitanda kimoja, sufuria 4 na n.k mkajua kuna siku mnaweza lala njaa na siku za mafanikio. Yote mnayabeba pamoja.

Wengi nawafahamu wameoa mwaka wa kwanza chuo kikuu na mpaka leo maisha yanakwenda. Maisha ni wewe tu.
 
Back
Top Bottom