kwa kusoma kama ulivoandika look so simple but in reality tunadanganyana why?
1. MATURITY
Umri wa miaka 20 kwa mtoto wa kiume anakua maturity "physical" but not ""Mentaly so hawezi kuhimili mikiki ya ndoa.
Umri wa Miiaka 20 tunategemea aoe kijana wa kike wa miaka 20 au chini ya hapo ambao kimtazamo akili zao wote hawa ni za kitoto bado hawawezi kupambanua mambo katika upana wa kufanya ndoa iwe "STABLE" matokeo ni kesi za kupigana, kuchitiana na utoto toto mwingi mwisho wa siku kuwapa mzigo wazazi hata kuachana.
2. ECONOMIC STABILITY
Kwa asilimia kubwa kwa vijana wengi wa kiume umri wa miaka 20 ndo kwaanza wapo chuo au wanajitafuta ukiachiliana mbali kupima uwezo wao wa kufua nazi kupimia nyenzo tofauti tofauti i mean wako PEAK in sexual drive...So my point is ni ngumu kukuta yupo kiuwezo kifedha wa kumtunza MKE na watoto kwa jamii yetu kama hii ya KITANZANIA.
3. LIFE EXPERIENCE and EXPOSURE
hahaha nimecheka kwa kuwa najua kuna watu wanaweza kuona kama sio point ya msingi lakini ina umuhimu wake..Taasisi ya ndoa kwa kijana wa kiume wa kitanzania ili uindeshe vizuri basi lazima uwe umepitia changamoto mbalimbali za kimaisha na kuweza kuzibakabili kimwili,kiakili na hata kiroho kuna kauzoefu flani lazima upate utaopima ujasiri na uwezo wa kutatua mambo kwenye maisha, sasa kwa kijana wa miaka 20 HAHAHAHA Ndo kwaaanza wengi akili zao zinakua zipo stage1 of maturity ni shida tupu alafu uje umpe ndoa asee ni vichekesho.
CONCLUSION
Kwangu mimi BIG NO kwa misingi na mifumo ya jamii zetu za kiafrika miaka 20 kwa kijana wa kiume kuingia kwenye NDOA.