Faida na hasara za kujenga nyumba yenye flat roof

Faida na hasara za kujenga nyumba yenye flat roof

Cost. According to Improve Net's online roofing calculator, a flat roof is significantlycheaper than a pitched roof. ... Flat roofs' repair costs are more expensive than pitched roofs' are, and because they are less prone to moisture damage, a pitched roof may be more affordable in the long-term.
 
Design ya namna hii ni nzuri.
A. Faida :-
bati na mbao ni chache.
Nzuri kimazingira.
Ni vigumu kuezuliwa na Upepo.
Kwa kiasi inaongeza ukubwa wa nyumba.
Unasaidia katika uvunaji wa maji ya mvua.
B. Hasara:-
Isijengwe palipo na miti mirefu.
Huitaji uangalizi hasa katika usafi juu ya papa.
Huitaji mfumo imara wa kupitisha maji ya mvua.
Ni rafiki kwa wanyama na ndege.
Ni lazima uwe na ngazi ya kufikia paa (usafi /ukarabati).
Huitaji umaliziaji mzuri kwa nje.
Huitaji headroom kubwa ili kupunguza Jotoridi ndani ya nyumba.

Kujenga nyumba ya namna hakupunguzi gharama za Ujenzi kwani nafuu ya kitu fulani huongeza gharama ya kitu kingine.

Hata hivyo Flat roof (0-10 degree slopes) kama ikijengwa kwa zege manufaa yake ni mengi zaidi kuliko kupaua kwa bati.
Hii ya ZegeUnaweza save asilimia ngapi roughly, kulinganisha na upauaji wa kawaida?! Just estimations tu
 
Wakuu naombeni turudi kwenye huu uzi

Poor design mzee flat inakua imefunguka Kwa nyuma hapo au uweke sehem ya kutolea maji tofaut Na hapo hyo roof itageuka kua swimming pool
Hii kwako haipendezei? Ama kweli uzuri upo machoni kwa mtu!
img-20180628-wa0056-jpg.807274

Mi naomba kujulishwa material ya huku kwenye kuta za nje nitumie rangi au nini ambayo haitabanduka kirahisi?

Pia naomba kujua niweke kozi ngapi za tofali toka kwenye lenta mpaka juu ili kuleta muonekano mzuri?

Ntashukuru kwa msaada wenu.
 
Wakuu naombeni turudi kwenye huu uzi




Mi naomba kujulishwa material ya huku kwenye kuta za nje nitumie rangi au nini ambayo haitabanduka kirahisi?

Pia naomba kujua niweke kozi ngapi za tofali toka kwenye lenta mpaka juu ili kuleta muonekano mzuri?

Ntashukuru kwa msaada wenu.

Ntashukuru sana nikipta majibu ya haya maswali wakuu
 
Poor design mzee flat inakua imefunguka Kwa nyuma hapo au uweke sehem ya kutolea maji tofaut Na hapo hyo roof itageuka kua swimming pool
Hivi mnatumiaga nini kuelewa vitu!!?? Umeshaambiwa roof inakuwa na slope sasa hiyo swimming pool inatokea wapi.!!!??? Au hujui maana ya slope!!!

Watu kama nyie mnatakiwa mpelekwe site kabisa uone ndio utaelewa hivi hivi utatuchosha sana tunaozielewa.

Mtu unaambiwa kuna gutter za kupitisha maji, but anauliza maji yatapita wapi!!!! Serious!!! Ifike mahali tuwe tunaelewa vitu haraka na kama neno lililotumika hulielewi ni bora kuuliza ueleweshwe.
 
Kwa vile umeomba ushauri basi wacha tushauri....
Flat roof ni cheaper sana kuliko pitched roof, lakini kama kutakua na leakage ili ufanye maintenance basi pitched roof ni cheaper kuliko flat roof,
Pia kwa life span , flat roof ni kuanzia 10 -15 years, ukipita huo mda basi inaanza kusumbua,
Kama nipo kwenye nafasi yako ningechagua pitched roof
Kuna nyumba zina flat roof zina miaka zaidi ua sitini
 
Design hizi ni nzuri lakini naomba nieleweshwe je distance kati ya ceiling board na bati kwa ndani ikoje? Je inaweza kuwa na nafasi kiasi cha mtu/fundi kuingia pale ukarabati unapohitajika? mathalan fundi wa umeme au kufanya usafi au kuua wadudu kama panya wanaotanbaa juu ya dari? Au hapo fundi itambidi àcrow ili kuweza kuingia ndani ya ceiling?
 
Wanajamvi nahitaji ushauri,

Nimedunduliza nakaribia kuvunja kibubu cha ujenzi wa nyumba. nimeshachorewa ramani na makadirio ya gharama. leo kwa shauku kubwa nimemuonyesha ramani boss wangu akanishangaa kwanini nimechora ramani yenye paa la gharama kubwa namna hiyo😵 akaniambia flat roo ingegharimu robo tu ya gharama zote za paa hili (ramani yangu ina paa la kawaida tu).

Amenistua kwasababu mchora ramani alinihakikishia hii ramani ni ya nyumba nafuu kabisa.

Sasa wadau nisaidieni mawazo kw ayeyote anaejuaa faida na hasara za kujenga nyumba yenye flatroof kabla sijabadilisha mawazo nikaingia mkenge.

Natanguliza shukrani za dhati


Picha tafadhali
 
My dream roof
 

Attachments

  • 182D4FC4-2945-437F-B001-F6443FE116CF.jpeg
    182D4FC4-2945-437F-B001-F6443FE116CF.jpeg
    42.2 KB · Views: 88
Back
Top Bottom