Faida na hasara za kujenga nyumba yenye flat roof

Faida na hasara za kujenga nyumba yenye flat roof

Huwa hakuna kuingia kwenye dari. Hakikisha umeziba vizuri wadudu kama panya wasiingie.
Wiring inafanywa kwenye ukuta chini sio darini. Yaani connection za waya ni kwenye switch/socket chini. Juu zinapita waya nzima nzima so ukiweka gypsum hupandi tena shoti ya umeme unarekebisha chini.
Asante mkuu hapo nimepata shule ya uhakika
 
Nyumba ya KAWAIDA baada ya ring beam unazungusha kozi tatu,hii ni kozi tano mpaka sita. So kuna ongezeko la kozi 2-3. Nafikiri unajua bei ya mbao na mabati.
Ya kwangu roof ya KAWAIDA ningetumia mabati at least 100, hii nimetumia mabati 40+. Mbao ndio wala sisemi.

Ni kweli mkuu. Pia uzuri ni kuwa hizo kozi 2-3 zinazoongezeka ni kwa kuta zinazozunguka nyumba tu sio pamoja na kuta za ndani. Tena wengine anazungusha ukuta mbele, kushoto na kulia nyuma inabaki wazi kwahiyo bati zinamwaga maji kwa nyuma ya nyumba
 
Kwa juu Nina nyumba nyingine sasa hapo reservoir ya Maji almost Lita 40,000 ambazo navuna Maji ya mvua. Hope nitajenga kibanda cha kupumzika juu Yake.
hii kitu ukiimaliza itakuwa matata sana...
 
Ni kweli kabisa haya yamenikuta juzi nilimwonesha bosi wangu nyumba ninayojenga yaani kabadilika kawa adui naona hata salamu zimekwisha na ili aingie ofisini kwake lazima apite kwangu. Yaani tulikuwa friend sana ila kwa sasa nafikiri anatamani hata niondoke kazini. Kila saa anajifanya nimekosea katika maagizo yaani imekuwa tabu sana
Huyo boss wako itakuwa kaona weevu! 🙄🙄🙄 Na siku za hivi karibuni jiandae kisaikolojia kupokea warning letter zinazofululiza bila sababu maalum!
Mambo ya maendeleo sio ishu za ku expose sana ofisini.
Kuna jamaa yangu alikuwa procurement kwenye kampuni yetu. Akanunua gari kali sana ila ya bei nafuu.
Nilimkataza sana asije nayo ofisini yeye hukunisikia. Alipoanza kuja nayo kazini, hakumaliza mwezi wakamuundia zengwe wakamfukuza kazi.
 
Wanajamvi nahitaji ushauri,
Nimedunduliza nakaribia kuvunja kibubu cha ujenzi wa nyumba. nimeshachorewa ramani na makadirio ya gharama. leo kwa shauku kubwa nimemuonyesha ramani boss wangu akanishangaa kwanini nimechora ramani yenye paa la gharama kubwa namna hiyo😵 akaniambia flat roo ingegharimu robo tu ya gharama zote za paa hili (ramani yangu ina paa la kawaida tu).
Amenistua kwasababu mchora ramani alinihakikishia hii ramani ni ya nyumba nafuu kabisa.
Sasa wadau nisaidieni mawazo kw ayeyote anaejuaa faida na hasara za kujenga nyumba yenye flatroof kabla sijabadilisha mawazo nikaingia mkenge.
Natanguliza shukrani za dhati
nani Kakuambia umuoneshe bosi wako?
 
Nadhani zile hasara za design ya Maputo ndiyo hizo hizo za flat desing ya paa.
 
Hizo nyumba ni nzuri ila zinahitaji utaalamu Mkubwa sana
 
Hivi flat roof ya bati na zege gharama zake zinatofatiana sana? Tofauti zipo kwenye nini hasa?
 
Back
Top Bottom