Faida ya kuishi duniani ni ipi kama tulizaliwa ili tufe?

Life is a cycle, kufa sio mwisho wa kuishi...

Hivyo unakufa ili uhamie maisha ya upande mwingine, kifo ni kama tiketi tu...
 
Mungu alifanya kila kitu kwa sababu zake.Yeye ndiye anayejua kwanini aliamua iwe hivyo.Binadamu sisi tunabashiri tu ila sababu anazo Mungu mwenyewe.Tukionana naye tutamuuliza.
 
Kila kitu ukionacho kitakufa tofauti tu mda .mfano jua ili litakufa baada ya miaka bilioni 5
 
Kwa story yako is it fair wewe uteswe kisa Babu yako alikula chapati bila ruhusa? Huyo Mungu yupo fair?
 
Life is a cycle, kufa sio mwisho wa kuishi...

Hivyo unakufa ili uhamie maisha ya upande mwingine, kifo ni kama tiketi tu...
Ndo maana waafrika mnaishi maisha maskini na duni yasiyo na maendeleo alafu wazungu wanaishi maisha ya kitajiri yenye ujuzi na technology. Wameachana na dhana potofu Kama hizi..hizi dhana ndo walizitumia katika utumwa katika ukoloni...eti tunateseka Ila baada ya kifo Kuna uzima..nani ameenda amerudi..Kuna dini kibao ndo mchezo huu huu ili kuchukua sadaka za watu na kucontrol maisha yao. Ukiwa umekufa this is your life.
 

Mleta mada kauliza swali hili...

Faida ya kuishi duniani ni ipi kama tulizaliwa ili tufe?

Je, ulichoandika wewe kinajibu hilo swali?
 
BIBLE its a Coded book tulia hivyo hivyo ufe na ujinga wako
 
Kwa story yako is it fair wewe uteswe kisa Babu yako alikula chapati bila ruhusa? Huyo Mungu yupo fair?
Ni fair kwa sababu ama ni hasi au chanya na hakuna hasichanya or any other way around it

Kwani Babu zetu wanapoacha legacy ama urithi je hatufurahii yale waliyoacha hata kama hatukuyavujia jasho hata tone??

Vipi yasiyo mema? yes, tutake au tusitake, thats it ishatokea
 
Unaweza fananisha urithi na uzao wote kuumia katika magonjwa njaa shida vita utumwa etc kisa Babu alikula chapati ambayo amewekewa kwenye sahani asile?
 
Ebwanaee, kuna utata sana apo kuhusu suala la kufa ndo maana wanasemaga usijudge sana kuhusu mungu unaweza ukakufuru ikala kwako....ila kwamfano maandiko yamesema mshahara wa dhambi ni mauti, jee kwann watenda mema nao wanakufa? na kama wakifa hao watenda dhambi kwanini wafufuliwe afu wauwawe tena au kuteswa kwenye jehanum
 
Kunakitu ulitaka kukiandika ILa hujakiandika.
 
Ukiwa utelezini huwa mawazo haya yanakujia au pale ni mapambio na kusifu.muwe mnashukrani sometime😂joke
 
Sasa hilo tunda lilikuwa bustani la kazingani??
Bwana wee hamna cha tunda wala nini wanaweka mafumbo tu au majazi yan inshot adam alimbandua hawa kwa hawa kufumbuliw macho na shetan kua akamtege tege adam akaw avai vijan akajfunika maungo yake anajiachia achia ovyo mzee baba akashndwa kushkilia bomba ndio mungu akawatmua ila adam alitubia ila afta dat ndio wakashushwa hku dunian lakn amna ushahid km bnadam alikua afi ad alipokula tunda na km alikua afi mbona alipulziw roh it mean alkua mfu hana uhai kbla ajapulziw roh
 
1. Kila mtu anakufa acha uwongo
2. Wages of sin is death maana yake kipindi hicho kulikuwa na option mbili uzima wa milele au kufa tu...wakaona haitoshi wakaamua kutengeneza story za Motoni ili kutishia watu zaidi wawe wakristo, old testament haina hell as fire Ina Sheol ambayo ni sehemu tu Jerusalem hawakuipenda
3. Waliokutishia wanataka sadaka zako na kucontrol maisha yako. Kwanini usijudge, kwa Nini story za Mungu ziwe na utata kuliko story zote duniani. Hizi ni story za mababu wasio na ujuzi wa maarifa na mazingira wakajiita mitume so acha uwoga wenzetu washatoka huku
 
Hatukuzaliwa ili tufe, kufa ni matokeo ya uchaguzi usio sahihi wa Adam. Sio kwamba alikula tunda fulani ndio akafa, hapana hiyo haitakuwa sahihi. Kwa nini Mungu aumbe matunda ambayo yatawaua watoto wake?

Ukweli ni kwamba suala la kula matunda ni lugha iliyotumiwa na Musa kufundisha kuhusu kuamini kile Mungu alisema nao kuhusu hatma yao.

Adam na Hawa kuishi milele pasipo kufa ilikuwa chini yao mwenyewe. Mungu aliwaumba wakawa hai, kisha suala la kuishi milele Mungu aliacha juu yao kama matokea ya choice yao. Ndio maana ya ubinadamu, Mungu hakutaka kucontrol maamuzi ya mtu, alimpa uhuru huo wa kuchagua lakini Adam hakuamini katika maneno Mungu alimwambia.

Kufa kwa Adam sio kwamba Mungu ndo alimuua, bali ni matokeo ya uchaguzi wake. Yaani, kuchagua tofauti na Mungu alivopendekeza ndio mauti yenyewe.
Mfano. Baba anaweza mshauri mwanawe kwamba ukigusa moto hakika utaungua; mtoto akikaidi na kugusa moto ule ataungua kweli, na hatuwezi kusema Baba kamuunguza, hapana. Kadhali Mungu hakumuua Adam bali hiyo ilikuwa ni matokea ya kutokutii maelekezo.

Kwa hiyo ni wazi kabisa kwamba Adam alipewa maelekezo ambayo kama angeamini katika hayo basi angeishi milele (Immortality) na pia angezaa watoto kwa namna yake ambao nao wangeishi milele.

Its not over yet. Bado plan ya Mungu ya kumfanya mtu aishi milele iko pale pale. Mtu anapoamini katika injili ya Kristo anapokea uwezo huo wa kuja kuishi milele baadae katika mwili mpya. Bado mwanadamu anao uchaguzi, achague uzima au mauti. Hilo Mungu hawezi kumlazimisha mtu, mtu mwenyewe anachagua.

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe wa pekee ili kila mtu AMWAMINIYE ASIPOTEE BALI AWE NA UZIMA WA MILELE
 
1. Mbona unaamini ukristo Kati ya dini 10k na miungu 3000 iliyokuwepo? Wat if dini zingine ndo za ukweli yako ya uwongo? Ukitoa ukoloni na familia una sababu gani ya kuamini dini yako?
2. We ukijua mtoto wako atakufa na unaweza ukamuokoa na unampenda si utafanya asife? Na hamna sehemu kwenye Biblia wamesema kwamba kabla ya kula tunda kulikuwa hamna kifo. Kama kifo hakikuwepo mti wa uzima wa milele ulikuwa una maana gani au Mungu alitegemea wale tunda ili waweze kufa au awanyime na tunda la uzima? 😅🤣Hii story ni ya kijinga na ya uwongo ndo maana hata kufikiria unaogopa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…