kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Siku hizi ni rahisi kuona timu ngeni zikija na mapipa yake kwaajili ya kuweka maji yenye barafu (maji baridi sana) kwaajili ya wachezaji. Faida hizi ya maji baridi sana sio TU kwa wwchezaji lakini ni kwa watu wote wanaooga maji baridi sana.
Ili mwili ufanyekazi zake vizuri unahitaji nguvu (ATPs), nguvu hizi ndizo anazozihitaji mchezaji ili kumudu kukimbia uwanjani kwa mafanikio makubwa.
Nguvu inazalishwa wapi na nini? Kuna vyanzo viwili vya kupata nguvu mwili, glucose (wanga) kutoka kwenye nafaka na mafuta kutoka kwenye nyama na mimea.
Kivipi? Ili mwili kutoa nguvu lazima chakula ulichokula kisangwe tumboni na kifyonzwe kwenye damu (glucose/fat acid), kisha chakula hiki kisafirishwe kutoka kwenye damu kuingia ndani ya seli za misuli ya mwili yaliko matanuli (mitochondria) ya kuunguzia chakula (Krebs Cycle) na kuzalisha nishati (ATPs) pamoja na joto, carbon dioxide, na maji. Hivyo, ili mwili uzalishe nguvu unahitaji chakula kingi, mitochondria nyingi, oxygen nyingi na Insulin nyingi. Ingawa wakati wa mazoezi hata bila insulin chakula kitaunguzwa TU.
Mabarafu yanafanya nini? Ukizamishwa kwenye maji baridi sana joto la mwili litashuka ghafla sana, Hali hii itasababisha mwili kuwasha mitambo yote ya kuongeza joto haraka kujiokoa na baridi (hypothermia), hivyo kuongeza kiwango cha kuchakata chakula (metabolism) ili kupata joto jingi haraka sana. Kitendo hiki kitazalisha glucose nyingi, mitochondria (matanuli) nyingi, oxygen nyingi kutoka mapafuni (hyperventilation) ili kuzalisha nishati kubwa sana mwilini, hatimaye nguvu nyingi kwa mchezaji ambazo zilipotea kwenye mechi iliyopita.
Kifupi kabisa mabarafu yanasaidia kuongeza na kurudisha matanuli (mitochondria) ya kuchomea na kuzalisha nguvu kwenye seli za misuli hivyo kumrejeshea nguvu zake mchezaji kwa kipindi kifupi sana kuliko kama angezirudisha kwa kupewa siku nyingi za kupunzika, chakula na mazoezi tu.
Nimejaribu kufupisha hii sayansi lakini nadhani umenipata.