Faida za mkopo wa muda mrefu na mfupi

Faida za mkopo wa muda mrefu na mfupi

Wewe mshahara wako ni Tsh ngapi?
Mbona 8mil ni pesa ndogo sana.
Kwa mtumishi wa umma, hakuna kitu chochote unachoweza kufanya bila kukopa. Hata gari tu ya milioni 8 huwezi kusema ukusanye mishahara mpaka itimie hiyo hela. Cha maana ni kuwa na malengo na kuhakikisha unapokopa pesa hiyo unaipeleka kwenye lengo husika.
 
Hiyo asilimia 5 ni kwa mwezi au kwa mwaka?
Riba ya mkopo full

Hiyo 5% ni riba ya mkopo utakaochukua kwa muda wote wa marejesho yako..

Ni saccoss ya ofisi hiyo ndo tunakopeshwa kwa riba ya 5%
Mf. Nakopa 10M
10,000,000 riba ya 5% ni 500,000.. so nitakuwa nina jumla ya deni la 10,500,000/= machaguzi ya kukatwa kwa muda wa miezi 12/18/24 ni yako.

Cc Financial Freedom
 
Watu wengi wa kawaida hawana financial literacy na maarifa sahihi ya namna ya kutumia Leverage eg loans for their favor. Wengi wa matajiri hutumia kanuni hizi mbili kuendelea kuwa matajiri. (1) OPM(Other people's money eg. Loans)
(2) OPM (Other people's time).
Loans sio mbaya, tatizo ni kutumia hiyo loans kuwekeza kwenye liabilities ambazo haziwezi rejesha hiyo hela wala faida yake.
Kuna utofauti kati ya mkopo mbaya na mkopo mzuri. Mkopo mbaya ni ule unaolazimika kuulipa kwa jasho na damu kutoka kwenye paycheck. Mkopo mzuri ni ule ambao, uwekezaji wako (Mahali utakapo kwenda kuwekeza) kuwe kunaweza kurejesha huo mkopo.
 
Wewe mshahara wako ni Tsh ngapi?
Mbona 8mil ni pesa ndogo sana.

Mil 8 ni pesa ndogo kwa nani? Mkuu, hebu panua mawazo kidogo acha kujifungia kwenye box. Usidhani kwamba kwa vile wewe umebahatika kuwa na vijihela basi watu wote ni kama wewe. Kwa taarifa yako mil 8 ni hela nyingi sana kwa majority ya watanzania..!
 
Riba ya mkopo full

Hiyo 5% ni riba ya mkopo utakaochukua kwa muda wote wa marejesho yako..

Ni saccoss ya ofisi hiyo ndo tunakopeshwa kwa riba ya 5%
Mf. Nakopa 10M
10,000,000 riba ya 5% ni 500,000.. so nitakuwa nina jumla ya deni la 10,500,000/= machaguzi ya kukatwa kwa muda wa miezi 12/18/24 ni yako.

Cc Financial Freedom

Aisee..🙄
 
Kuna utofauti kati ya mkopo mbaya na mkopo mzuri. Mkopo mbaya ni ule unaolazimika kuulipa kwa jasho na damu kutoka kwenye paycheck. Mkopo mzuri ni ule ambao, uwekezaji wako (Mahali utakapo kwenda kuwekeza) kuwe kunaweza kurejesha huo mkopo.

Mkuu hapa naomba nitofautiane kidogo na wewe. Kwangu mimi, mkopo mzuri ni ule ambao nimeufanyia kitu cha maana HATA KAMA ntalazimika kuulipa kwa jasho na damu! Hii ni kwasababu, bila ya mkopo huo basi hicho kitu cha maana kisingefanyika.

Mfano; Kama nina lengo la kununua gari ya kutembelea, nikakopa hela na kununua gari niipendayo, kwangu mimi huo ni mkopo mzuri maana sasa nna gari ya kutembelea. Yes, ntaumia for sometime kulipa huo mkopo lakini baadae ntaendelea ku enjoy benefits za kuwa na gari yangu, ambazo ni kubwa kuliko kuning'inia kwenye daladala.
 
Wataalam wa mikopo wanakwambia usikope kununua gari ya kutembelea maana gari liability haliingizi chochote Bali litakufanya pia utoe hela mfukoni ili kulihudumia kwa hiyo litakunyonya zaidi, kama unataka kununua gari basi nunua ya biashara eg hiace, coaster, kirikuu, tipper etc ili ilete hesabu pia hata kujenga nyumba ya kuishi kwa mkopo hawashauri pia labda ujenge ya biashara let say guest house, vyumba vya biashara n.k. Jana niliiona video moja ya MO anasema watu wanakosea kwa kukopa hela then wanajenga nyumba ya kuishi kwa nin hiyo hela usiifanyie biashara na wewe ukaendelea kupanga nyumba yenye gharama ndogo then biashara ikikua na kuanza kuingiza faida ya kutosha ndio unajenga nyumba kwa kutumia faida unayoipata
 
kwa nin hiyo hela usiifanyie biashara na wewe ukaendelea kupanga nyumba yenye gharama ndogo then biashara ikikua na kuanza kuingiza faida ya kutosha ndio unajenga nyumba kwa kutumia faida unayoipata

Na hili ndio kosa kubwa ambalo hao wanaojiita "wataalamu" hua wanafanya. Ku assume kwamba, kila mtu anaweza kufanya biashara na ikakua na kuleta faida! Biashara ingekua rahisi kiasi hicho kila mtu angekua milionea.

Ifike mahali tuelewe jamani, biashara ni kipaji kama vipaji vingine na sio kila mtu anacho hicho kipaji. Hao hao wataalamu wanatuambia kwamba katika kila biashara 10 zinazoanzishwa, 7 hua zinakufa kabla ya miezi 6! Kama huna kipaji cha biashara, kuliko ukatumbukize hela ya mkopo kwenye biashara ya majaribio ni heri mara 100 ujenge nyumba ya kuishi, au ununue gari ya kutembelea angalau utakua unaiona...!

Aftaroo kwa nchi zetu hizi, wengi wetu lengo sio kua matajiri kama Mo, lengo ni kuishi maisha decent - nyumba nzuri, gari nzuri, watoto wale, wasome shule nzuri na nikiugua nisikose tiba, thats all.
 
Riba ya mkopo full

Hiyo 5% ni riba ya mkopo utakaochukua kwa muda wote wa marejesho yako..

Ni saccoss ya ofisi hiyo ndo tunakopeshwa kwa riba ya 5%
Mf. Nakopa 10M
10,000,000 riba ya 5% ni 500,000.. so nitakuwa nina jumla ya deni la 10,500,000/= machaguzi ya kukatwa kwa muda wa miezi 12/18/24 ni yako.

Cc Financial Freedom

Nje ya mada mkuu naomba nikuulize..

Hiyo SACCOS yenu ina wafanyakazi iliowaajiri mnaowalipa mshahara? Je, mna ofisi ambayo mnalipa kodi, umeme, maji, ulinzi nk? Mna bodi ambayo inalipwa allowances? Mnafanya mafunzo? Mwisho wa mwaka mnapata gawio?

Nauliza kwasababu kwa mchanganuo huo ulioutoa hapo juu, ina maana mtu akichukua mkopo wa 10m kwa miezi 24, analipa riba ya shilingi 20,800 kwa mwezi. Ili muweze kumlipa mfanyakazi mmoja mshahara wa tsh 500,000 tu kwa mwezi, itabidi mtoe mikopo ya 250m. Hapo tuna assume mna mfanyakazi mmoja tu na hakuna gharama nyingine zozote za uendeshaji.

Au nyie wenzetu mnafanyaje..?
 
Watu wengi wanaumia kwa kutaka iga wengine

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Wanatumia vibaya akili zao hao wapeleke watoto shule nzuri kwasababu unao uwezo huo sio kwa kukopa pesa ambazo zitakuumiza mwisho wa siku watoto wanahitimu chuo halafu ajira hakuna wanabaki kukutegemea tena Kama wewe ni muajiriwa ustaafu uwapatie pension yako wakafungue biashara wakati walisoma sociology mwisho wanashindwa kusimamia biashara wanafilisika unapata presha unakufaaaa.
 
Mkuu hapa naomba nitofautiane kidogo na wewe. Kwangu mimi, mkopo mzuri ni ule ambao nimeufanyia kitu cha maana HATA KAMA ntalazimika kuulipa kwa jasho na damu! Hii ni kwasababu, bila ya mkopo huo basi hicho kitu cha maana kisingefanyika.

Mfano; Kama nina lengo la kununua gari ya kutembelea, nikakopa hela na kununua gari niipendayo, kwangu mimi huo ni mkopo mzuri maana sasa nna gari ya kutembelea. Yes, ntaumia for sometime kulipa huo mkopo lakini baadae ntaendelea ku enjoy benefits za kuwa na gari yangu, ambazo ni kubwa kuliko kuning'inia kwenye daladala.
Duuh noma sana.
 
Kiukweli faida za kila mkopo uwe wa muda mrefu au mfupi utazipata kulingana na jinsi ulivoutumia mkopo kwa malengo.
Mikopo ya muda mfupi faida zake ni kwamba deni litawahi kumalizika mapema hivyo hivyo hata kama uliwekeza kwa hasara athari zake zitakutesa kwa muda mfupi then you get recovery.
Mikopo ya namna hiyo ni mizuri kutumia kwa kwa miradi ya maendeleo isiyo ya kibiashara mfano kununulia gari, kulipa ada ya mtoto au kujengea nyumba ya kuishi.
Kwa upande mwingine mkopo wa muda mrefu faida zake ni pamoja kulipa mkopo kidogokidogo lakini pia tambua kuwa marejesho yake pia ni ya muda mrefu hivyo unapokopa hakikisha sehemu ya mkopo unaipandikiza kwenye mradi wa biashara, vinginevyo ukiuwekeza kwenye anasa au kwa hasara maumivu yake huwa ni makali sana, maana utateseka muda mrefu hadi kumaliza mkopo, hapa walio wengi hushindwa kuvumilia na kuba unfanya top up, matokeo yake unnazeeka a mkopo! Unaweza kuwa mwanzo wa kupata magonjwa kama kisuksri, BP na mengine!
 
Nje ya mada mkuu naomba nikuulize..

Hiyo SACCOS yenu ina wafanyakazi iliowaajiri mnaowalipa mshahara? Je, mna ofisi ambayo mnalipa kodi, umeme, maji, ulinzi nk? Mna bodi ambayo inalipwa allowances? Mnafanya mafunzo? Mwisho wa mwaka mnapata gawio?

Nauliza kwasababu kwa mchanganuo huo ulioutoa hapo juu, ina maana mtu akichukua mkopo wa 10m kwa miezi 24, analipa riba ya shilingi 20,800 kwa mwezi. Ili muweze kumlipa mfanyakazi mmoja mshahara wa tsh 500,000 tu kwa mwezi, itabidi mtoe mikopo ya 250m. Hapo tuna assume mna mfanyakazi mmoja tu na hakuna gharama nyingine zozote za uendeshaji.

Au nyie wenzetu mnafanyaje..?
Hiyo saccoss iko ndani ya ofisi..

let say ofisi ni udsm, na saccoss iko ndani ya udsm ‘special kwa staff wake

Saccoss haihusiki na expenses zozote za ofisi.

Ni kama tunanunua hisa, unachagua kukatwa kwa mwezi 50/100K/200k na zaidi depends na kipato chako.
Mwishoee ukitaka kukopa inajumlishwa michango yako yote times 3..
Let say nilichanga M3.. basi itakuwa M3 times 3= M9 ‘hisa zitaniruhusu kukopa mpaka M9.

Na makato ni kama kawaida, kabla mshahara hujakufikia.
 
Habari wakuu, mimi ni mtumishi wa Umma ambapo nina fursa za kukopa benki mkopo wa muda mrefu na mfupi na siku hizi benki nyingi zimeongeza muda wa mkopo hadi miaka 8.
Nilikuwa naomba mawazo yenu kuhusu faida za mkopo wa muda mrefu na muda mfupi ingawa nafahamu kuwa changamoto kubwa ya mkopo wa muda mrefu ni riba kuwa kubwa, Je zipi faida nyingine?
muda mrefu unapata hela nyingi na rejesho linakuwa dogo ila riba inakuwa .
kumbuka riba ni kwa mwaka, sasa miaka ikiwa mingi , riba nayo inadaradadi
 
Back
Top Bottom