Kwanini ume-quote kwa kingereza na sio kiarabu wala kiswahili?
Sijakupa masharti bali nimekupa darasa.Muislam husamehe bila masharti, na kuhusu huo ujuzi unaosema hakuna mjuzi Dunian ila Allah pekee wengine sisi wote twafwata mafundisho yake
Damas na Titusnataka kujua majina ya wale wanyang'anyi wawi
li waliosulubiwa na Yesu.. mmoja alikuwa kushoto na mwingine kulia ...majina yao tafadhali
ujajibu swali#300General Knowledge.
Naam, kama kichwa cha habari kinavyojieleza.
Natumia fursa hii ya mtandao adhyim wa JF kuwapa fursa wanamtandao wote wapate fursa ya kuuliza kuhusu mada au jambo lolote ambalo unataka upatiwe majibu.
Si majibu yote yatatoka kwangu binafsi, bali nitajitahidi iwezekenavyo kukupatia majibu murwa na yanayolingana na swali lako na ambapo sina jibu itakuwa fursa kwa wengine kutoa majibu.
Hapa ni kwa ajili ya kuelimishana na kujuzana bila kikomo, iwe swali lolote liwalo.
Yesu wa kwenye Biblia.
Na Isa wa kwenye Qurani.
Hivi wewe uliwahi kuolewa hapo zamani je wewe ni mke ya mtu?je katika imani yako unafungamana na kundi gani la kigaidi?
Dini hii inafundisha chuki...chuki.. machafuko.. upanga kisasi na vita ndio maana upanga na kumwaga damu hakuishi kwa nchi zao!!Si kweli.
Uislam haufundishi ugaidi wala haufungamani na kundi lolote la kigaidi.
Uislam unafundisha:
Qur'an 5:
32. Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.
33.Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa.
Maashaallah!AlhamduliLlah, mimi sijawahi kuolewa.
Mimi nimeoana na mume wangu zamani na mpaka sasa mume wangu ni huyohuyo mmoja.
Sifungamani na kundi lolote la ugaidi na dini yangu hairuhusu ugaidi.
Majibu mujarabu, sasa, hawa wanaochinja watu na kuvamia wengine kwenye Biashara za m-pesa na kuwapora na kuwaua huku wakidai ni ibada wanatumia kitabu gani na aya zipi?
weka jina lako halisi, ili tuweze kuhakikisha hiyo elimu yako. otherwise tutakuwa tunamuuliza maswali magumu ****** mmoja asiyejua chochote.
Sina chuki na Joyce Ndalichako bali nnauhakika si kiongozi mzuri, alivurunda kama mkuu wa NECTA mpaka baadhi ya Waislam wa Tanzania wakaandamana kumkataa. Jikumbushe:
Hivi dada nyumbani kwako unaweza kumkaribisha mkiristu aliyefunga kipindi cha kwaresma na muda wa kufuturu ukifika unamuandalia chakula kama mama yangu mzazi alivyokuwa anawaandalia futari na daku marafiki zangu niliosoma nao wajapo kunitembelea na hautaweka sumu?
kwahyo umefanya nini hapa nchini maana naona u mwanamama mwenye elimu toka miaka hyo ambayo ni nadra kumpata mwanamke aliesoma elimu ya degree!Sijaishi Tanzania katika umri wangu wa kuwa "productive".