Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Muislam husamehe bila masharti, na kuhusu huo ujuzi unaosema hakuna mjuzi Dunian ila Allah pekee wengine sisi wote twafwata mafundisho yake
Sijakupa masharti bali nimekupa darasa.
Hii haina tofauti na kusengenya.
Na hayo mafundisho ndio ujuzi wenyewe.
Kama huna ujuzi au elimu ya kuchangia hoja ni bora kukaa kimya!!!
 
General Knowledge.

Naam, kama kichwa cha habari kinavyojieleza.

Natumia fursa hii ya mtandao adhyim wa JF kuwapa fursa wanamtandao wote wapate fursa ya kuuliza kuhusu mada au jambo lolote ambalo unataka upatiwe majibu.

Si majibu yote yatatoka kwangu binafsi, bali nitajitahidi iwezekenavyo kukupatia majibu murwa na yanayolingana na swali lako na ambapo sina jibu itakuwa fursa kwa wengine kutoa majibu.

Hapa ni kwa ajili ya kuelimishana na kujuzana bila kikomo, iwe swali lolote liwalo.
ujajibu swali#300
 
Hivi wewe uliwahi kuolewa hapo zamani je wewe ni mke ya mtu?je katika imani yako unafungamana na kundi gani la kigaidi?

AlhamduliLlah, mimi sijawahi kuolewa.

Mimi nimeoana na mume wangu zamani na mpaka sasa mume wangu ni huyohuyo mmoja.

Sifungamani na kundi lolote la ugaidi na dini yangu hairuhusu ugaidi.
 
Si kweli.

Uislam haufundishi ugaidi wala haufungamani na kundi lolote la kigaidi.

Uislam unafundisha:


Qur'an 5:
32. Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.

33.Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa.
Dini hii inafundisha chuki...chuki.. machafuko.. upanga kisasi na vita ndio maana upanga na kumwaga damu hakuishi kwa nchi zao!!
Basi ebu tukwambie Mwenyezi Mungu asema!!
" Msilipize kisasi cha aina yeyote Ila maana kisasi n juu yake""
Wanafunzi wa Yesu wakamuuliza juu ya kumpiga mwanamke aliyekamatwa anazini kama ilivyo sheria ya Musa
"Nae akawambia anaejiona mkamilifu, yeye asie na dhambi na awe wa kwanza kupiga mawe"
Ukiwambia watakwambia Marekani ,ni ajabu sana wakati marekani!! Sasa najiulza je marekan ndio kaja hata huku mavyuoni kwenye ubaguz au mitaan au kaenda galisa,Nigeria Sudan somalia !! Hata wenyewe kwa wenyewe wanauana " Yemen Vs Saudi Arabia...bado watasema marekani!!
........,..........."yeyote atakae UA kwa upanga nae atakufa kwa upanga".........
 
Majibu mujarabu, sasa, hawa wanaochinja watu na kuvamia wengine kwenye Biashara za m-pesa na kuwapora na kuwaua huku wakidai ni ibada wanatumia kitabu gani na aya zipi?


Watu wengi hutumia "dini" kama joho la kuficha au kuhalalisha madhambi yao lakini nnauhakika dini njema hazifundishi maovu.
 
Sina chuki na Joyce Ndalichako bali nnauhakika si kiongozi mzuri, alivurunda kama mkuu wa NECTA mpaka baadhi ya Waislam wa Tanzania wakaandamana kumkataa. Jikumbushe:

DSC08684.jpg

Hoja dhaifu eti alivurunda kama mkuu wa NECTA,Ndalichako hamfanyii mwanafunzi mitihani.
 
Hivi dada nyumbani kwako unaweza kumkaribisha mkiristu aliyefunga kipindi cha kwaresma na muda wa kufuturu ukifika unamuandalia chakula kama mama yangu mzazi alivyokuwa anawaandalia futari na daku marafiki zangu niliosoma nao wajapo kunitembelea na hautaweka sumu?


Mimi nnawaalika sana Wakristo nyumbani kwangu na nna marafiki wengi sana Wakristo kuliko unavyofikiria na wengi wengineo wanakuja kwangu bila mualiko, ni kama kwao tu.

Nnawaandalia vyakula si tu wakati wa "kwaresma" bali siku yoyote ile.

Kwanini nikuwekee sumu, umeshasikia wangapi wamekufa kwa sumu kwa ajili wameenda kula kwa Muislam?

Futa hayo mawazo ya kijinga.

Napenda uelewe kuwa wakati wa Mtume Muhammad Salla Allahu Alayhi Wasalaam, Waislam waliamrishwa na mtume wa "immigrate" kwenda Habashi na huko ilikuwa ni nchi Kikristo na Mfalme Mkristo aliwapokea na walipomueleza walipotoka akawauliza maswali walivyomjibu, akawaambia, naam, huyo kweli ni Mtume wa Mwenyeezi Mungu na akawakaribisha vizuri sana.

Ukipenda kisome kisa hicho hapa: Migration to Abyssinia - Wikipedia
 
Waislam wanaposema Quran imeshushwa maana yake nn? Kilishuka kitabu (aya) ama ni vipi?
 
Back
Top Bottom