FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
- Thread starter
- #1,461
1. Kukusikia na kukuona
2. Kutaka kujua siri ya wewe kujua mambo na uwezo wako wa kujibu maswali bila kuhamaki na ku-panic
3. Kuna tetesi wewe ni MTU mkubwa Sana hapa TZ kwa maana ya wadhifa kitaifa ( sina ushahidi)
4. Kukuskia kwa maskio yangu ukiongelea juu ya serikali ya JPM. Juu ya uchumi wake baada ya miaka minne iliyobaki.
5. Ushauri wako juu ya maswala la kitechnolojia, kwann swala la internet likua ishu TZ wakati ilipaswa kuwa compulsory ili kusaidia ujuzi wa ziada katika kazi na Elimu. Nini kifanyike?
1) Si muhimu sana.
2) Soma.
3) Si kweli.
4) Nisome tu humu JF.
5) Technolojia inaweza kuifanya nchi ipige hatua ndefu kwa haraka kuleta maendeleo kama itatumika vyema na inaweza ikaifanyia nchi ipige hatua kumi nyuma na kuwa ni janga badala ya neema kama haitowekewa mikakati ya matumizi sahihi.
Miundo mbinu ya kusambaza teknolijia tuliyonayo Tanzania ni bora kuliko nchi nyingi sana duniani. Tumpongeze sana Jakaya Kikwete kwa kufanya jitihada hizo hadi kufikia kusambaza "mkonga" wa taifa wa "fiber optics" Tanzania nzima. Ni hatua kubwa sana kwa nchi inayoendelea.
Watanzania bado hatutumii hata asilimia 5 ya uwezo wa huo mkonga.
Kulikuwa na mikakati mizuri sana iliyoanzia wakati wa Kikwete kuhusu teknolijia ya "internet":
1) Mitandao ya mawasiliano imesambazwa Tanzania nzima
2) Kikwete aliamuru shule zote ziwekewe umeme kama si wa gridi basi japo wa solar au njia nyingine, moja ya mafanikio yake ni REA., ili kila shule iweze kufundishika kwa mbali kupitia "internet".
3) Mkonga wa Taifa.
4) Super Computer (zipo)
Utaona kuwa miundo mbinu tayari kwa kiasi kikubwa kuhusu hilo la kuifanya "internet kuwa "compulsory".
Ni matumaini yetu kuwa awamu hii italitimiza lengo hilo kwani kwa kiasi kikubwa miundo mbinu yake ipo.