Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Jibu lani hili la miaka zaidi ya 1400 iliyopita:

Qur'an 28:
55. Na wanapo sikia upuuzi hujitenga nao na husema: Sisi tuna vitendo vyetu, na nyinyi mna vitendo vyenu. Salamun Alaikum, Amani juu yenu! Sisi hatutaki kujibizana na wajinga.

ni kweli tunapo sikia upuuzi wa qaraa tunaachana nao na kushahadia!; HAKIKA HAKUNA MUNGU APASWAYE KUABUDIWA ILAHA YESU NA PAULO MTUME WAKE!
 


Naam, nimerudi kama nilivyokuahidi, nnaona hujazileta hizo aya kama nilivyokutaka lakini si kitu.

Aya ya za 2:191-193 ukitaka uzipate kwa "context" yake anzia aya ya 2:190 - 195, soma:

190. Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui. Maelezo

Na maelezo yake ni haya:

190. Na katika kumcha Mwenyezi Mungu ni kustahamili mashaka katika kumt'ii Yeye, na mashaka makubwa kabisa juu ya nafsi ni kuwapiga vita maadui wa Mwenyezi Mungu. Lakini wakikuvamieni, basi piganeni na hao wavamizi. Na mmepewa ruhusa kuurudi uvamizi wao, lakini nyinyi msivamie kwa kuanza nyinyi, au kwa kumuuwa asiye kupigeni vita wala hana mahusiano na vita; kwani Mwenyezi Mungu hawapendi wavamizi.

191. Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wakupigeni huko. Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri.Maelezo

Maelezo yake:

191. Wauweni walio kuanzeni vita popote mnapowakuta, na watoeni Makka, wat'ani wenu ambao wamekulazimisheni kuutoka. Wala msione vibaya, kwani walio kufanyieni nyinyi ni maovu zaidi kuliko kuuwa msikitini, nako ni kuwafitini Waumini katika Dini yao kwa kuwaadhibu huko Makka mpaka wakauacha mji wao kuhifadhi Dini yao. Na huu Msikiti Mtakatifu una utakatifu wake, basi msiuvunje kwa kupigana ndani yake. Lakini wakikupigeni vita ndani yake basi nanyi pia wauweni, na nyinyi kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, mtashinda. Na malipo ya makafiri ni kufanyiwa wanayo wafanyia watu.

192. Lakini wakiacha basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. Maelezo

Maelezo yake:

192. Wakirejea wakaacha ukafiri, wakafuata Uislamu basi Uislamu humuitikia anaye uelekea. Na Mwenyezi Mungu atawasamehe ule ukafiri wao wa zamani kwa fadhila yake na rehema yake.

193. Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu. Maelezo

193. Wapigeni vita walio taka kukuuweni na kukugeuzeni muache Dini yenu kwa maudhi na mateso mpaka ing'oke mizizi ya fitina na isafike Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Wakiuacha ukafiri wao basi wamejiokoa nafsi zao na wataepukana na adhabu. Hapo basi haifai kuwafanyia uadui. Uadui hufanyiwa mwenye kuidhulumu nafsi yake akaiteketeza kwa maasi na akaacha uadilifu kwa maneno na vitendo.

194. Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu. Maelezo

194. Na pindi wakikushambulieni katika mwezi mtukufu msiache kupigana nao, kwani huo ni mtukufu kwao kama ulivyo kuwa mtukufu kwenu. Ikiwa wao watauvunja utukufu wake basi nanyi wakabilini kwa kuzilinda nafsi zenu katika huo mwezi. Na katika mambo matukufu na matakatifu pana sharia ya kisasi na kutendeana mfano kwa mfano. Anaye kushambulieni katika matakatifu yenu nanyi jilindeni na uadui huo kwa mfano wake. Na mcheni Mwenyezi Mungu, msikiuke mipaka katika kulipiza kisasi. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwanusuru wachamngu.

195. Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema. Maelezo

195. Kupambana na makafiri kunahitaji kutoa roho kama ilivyo kutoa mali. Basi toeni kwa kuandaa vita, na jueni kuwa kupigana na hawa ni kupigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi msikae tu. Toeni mali kwa ajili yake, kwani mkitofanya na mkafanya ubakhili adui atakupandeni na atakudhilini. Hapo itakuwa kama mlio jitokomeza wenyewe kwenye maangamio. Tendeni lilio kuwajibikieni kwa uzuri na vilivyo, kwani Mwenyezi Mungu hupenda anapo fanya jambo mtu alifanye vizuri.

Aya 190 mpaka 195 zinaeleza sharia ya vita katika Uislamu. Nazo zinaeleza kwa matamshi yalio wazi haya yafuatayo:
*1. Ruhusa ya kupigana imetolewa kwa ajili ya kujilinda na uvamizi wa vita wa vitendo khasa, au zikidhihiri dalili kuwa maadui wanataka vita. Vita havikulazimishwa kwa ajili ya vita wala kwa sababu ya kutaka kuwasilimisha watu kwa kuwauwa na kuwapiga vita.
*2. Kunakatazwa kuvamia au kuanza uadui kwa njia yoyote ile. Basi hapana ruhusa kufanyiwa uadui asiye pigana, wala hapana ruhusa kuvuka mipaka ya uadui wakati wa vita: basi hauliwi asiye chukua silaha, wala hakhusiani na vita bali ni mwenye kukumbwa tu na vita. Wala hauliwi mwenye kusalimu amri na akatupa silaha. Wala hapana ruhusa kuwavunjia watu nyumba zao, huko ni kupita mpaka.
*3. Mzingatie fadhila iliyo onyeshwa kwa kuamrishwa kuchamngu. Basi msivunje heshima ya wanawake kuwanajisi, hata washirikina wakifanya hayo. Wala msiwakatekate walio uwawa hata ikiwa makafiri wakiwafanyia hayo Waumini. Washirikina walimfanyia hayo Bwana wa Mashahidi, Hamza, wala Mtume s.a.w. hakutoa ruhusa kumfanyia hayo maiti yeyote, bali alikataza akasema:"Tahadharini msiwakatekate maiti".
*4. Vita vinakwisha wakiacha washirikina kuwafitini Waumini katika Dini yao, na Dini inakuwa inataka akili na nyoyo zimwelekee Mwenyezi Mungu kwa uhuru.
*5. Hapana vita katika mwezi mtukufu, nayo ni miezi ya Hija na Umra. Ikiwa washirikina watapigana katika miezi hiyo, basi Waumini nao yawapasa wapigane.
*6. Kuacha kutoka kwenda pigana na maadui wanauwa pasina nasi kupigana nao ni kuipoteza kheri na wema. Kwa haya inadhihiri kuwa vita vya Islamu vina fadhila katika sababu zinazo pelekea kuanza kwake, na vina uadilifu katika kuviendesha. Viwapi hivi na vita vya mataifa mengine ya zamani na ya sasa! Vita vyao hao ni vya uchafu, na vita vya Islamu ni vya Haki na vyenye fadhila.

semper saratoga

Nnaona mpaka hapo utagunduwa kuwa ulipozitowa hizo aya zilikuwa si kwa "context" yake.

Jee, kuna tatizo katika hayo mafundisho mema kabisa?
 
ni kweli tunapo sikia upuuzi wa qaraa tunaachana nao na kushahadia!; HAKIKA HAKUNA MUNGU APASWAYE KUABUDIWA ILAHA YESU NA PAULO MTUME WAKE!

Qur'an 28:
10. Na moyo wa mama yake Musa ukawa mtupu. Alikuwa karibu kumdhihirisha, ingeli kuwa hatukumtia nguvu moyo wake ili awe miongoni mwa Waumini.
Maelezo
 
Kuna ujumbe nlikisudia ukufikie ili niondoshe dhimma mbele ya muumba. Kuusoma ni khiyari yako


Unaweza kuuweka hapa kama kweli una nia safi na itakuwa ni darsa kwe wengine pia.

Kuna nini cha kuficha hadi kuutuma PM? Hapa tunaelimishana wote kwa faida ya wote.
 
Asante kwa ufafanuzi nilikuwa off line kidogo. Ngoja nirudie tena taratibu nielewe zaidi.
 
FaizaFoxy : wakati naendelea soma na kuchambua majibu yako nilikuwa na swali la nyongeza. Je kabla ya kuja kwa uislam wale ambao waliishi enzi hizo (waarabu na wasio waarabu mathalani wakina mzee mangungo wa msowero) watahukumiwa kwa sheria gani?Quaran itatatumika kuwahukumu retrospectively? (i mean kwa iman ya dini yako)
 
Unaweza kuuweka hapa kama kweli una nia safi na itakuwa ni darsa kwe wengine pia.

Kuna nini cha kuficha hadi kuutuma PM? Hapa tunaelimishana wote kwa faida ya wote.
Dini inaenda ka utaratibu ulowekwa. Nafikiri yatosha kiasi hichi na samahani kw usumbufu
 
Hili ndilo swali ambalo nimemuuliza dada yangu, hajatoa jibu mpaka sasa...ukitoa maelezo marefu anajibu pale ambako haujauliza swali. Hili swali ni gumu sana jibu ambalo ni common ni kwamba kwakua hawakufikiwa na meseji ya Allah ... hukumu yao itakuwa determine siku ya kufufuliwa.... very simple answer kwa swali gumu. Sometimes ni bora useme haujui... how kila swali una uwezo wa kujibu....
 
Labda bado anafukua nondo mkuu ngoja tusubirie tupate ilim kidogo
 
Faiza ama mwingine yeyote mwenye ufahamu humu jukwaani. Nataka agiza simu ya HTC 10 toka marekani (moja kwa moja toka website ya htc hii hapa: One Size Fits All. $200 Off HTC 10 | 2016 Best Smartphone | HTC United States) shida ni kwamba hawafanyi shipping kutoka nje ya marekani (as far as i know). Kwasasa imeshuka toka dola 699 mpaka dol 499. Je kuna njia rahisi ya kuzisafirisha kuja huku ama kuna watu wanafanya hizo makitu kwa uhakika hapa dsm? (Yes i know zipo kwenye maduka hapa Dar ila mimi siziamini kwa kuwa taya nimenunua simu mbili hapa HTC ONE M7; HTC ONE E8 wakanipa warranty ya miezi sita lakin zikakorofisha baada ya mda mfupi tukaanza kusumbuana sana sana kurekebisha ). wajuzi wa mambo tafadhali...
 
Habari yako faiza...., Nilitaka kujua Nini maana ya Mfumo Kristo.
1/ Je huu mfumo hapa kwetu Upo?
2/ Kama upo.....
....Nini madhara yake?.
3/ Mfumo hu una mahusiano na Serikali ama chama chochote cha Siasa?.
4/ Nini mahusiano yako Wewe na huo mfumo ama chama chenye Fungamano na huo mfumo?.
5/ Kwa namna gani Waweza kuushinda mfumo huo kwa kupamba na waziri,Katibu... ama mkurugenzi?.
6/ Nini maoni yako kws wanasadiki kuwepo kwa Mfumonhuo na hatua wanazopaswa kichukua.
 
Dini inaenda ka utaratibu ulowekwa. Nafikiri yatosha kiasi hichi na samahani kw usumbufu

Hivi utaratibu wa Dini "ulowekwa" ni "inaenda" kwa PM?

Makubwa haya, madogo yana mambo.

Dini ni njia na ikiwa tutazificha njia kwenye PM ni nani wa kufaidika? Kuna siri ipi kwenye mambo ya dini hata iwe PM?

Tafadhali sana tusitake kutishana kwenye njia ya haki. Na kama upo kwenye haki basi usiogope kuwa muwazi. Unakificha nini?
 


Kuna paper iliwekwa na Mohamed Said humuhumu JF ikafutwa harakaharaka kuhusu hayo, nnakusihi pitia post hii:

https://www.jamiiforums.com/threads...-rise-of-muslim-militancy-in-tanzania.171128/

Hapo utapata majibu ya maswali yako na jaribu unachokiona humo google.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…