Naam, nimerudi kama nilivyokuahidi, nnaona hujazileta hizo aya kama nilivyokutaka lakini si kitu.
Aya ya za 2:191-193 ukitaka uzipate kwa "context" yake anzia aya ya 2:190, soma:
190. Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui. Maelezo
Na maelezo yake ni haya:
190. Na katika kumcha Mwenyezi Mungu ni kustahamili mashaka katika kumt'ii Yeye, na mashaka makubwa kabisa juu ya nafsi ni kuwapiga vita maadui wa Mwenyezi Mungu. Lakini wakikuvamieni, basi piganeni na hao wavamizi. Na mmepewa ruhusa kuurudi uvamizi wao, lakini nyinyi msivamie kwa kuanza nyinyi, au kwa kumuuwa asiye kupigeni vita wala hana mahusiano na vita; kwani Mwenyezi Mungu hawapendi wavamizi.
191. Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wakupigeni huko. Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri.Maelezo
Maelezo yake:
191. Wauweni walio kuanzeni vita popote mnapowakuta, na watoeni Makka, wat'ani wenu ambao wamekulazimisheni kuutoka. Wala msione vibaya, kwani walio kufanyieni nyinyi ni maovu zaidi kuliko kuuwa msikitini, nako ni kuwafitini Waumini katika Dini yao kwa kuwaadhibu huko Makka mpaka wakauacha mji wao kuhifadhi Dini yao. Na huu Msikiti Mtakatifu una utakatifu wake, basi msiuvunje kwa kupigana ndani yake. Lakini wakikupigeni vita ndani yake basi nanyi pia wauweni, na nyinyi kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, mtashinda. Na malipo ya makafiri ni kufanyiwa wanayo wafanyia watu.
192. Lakini wakiacha basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. Maelezo
Maelezo yake:
192. Wakirejea wakaacha ukafiri, wakafuata Uislamu basi Uislamu humuitikia anaye uelekea. Na Mwenyezi Mungu atawasamehe ule ukafiri wao wa zamani kwa fadhila yake na rehema yake.
193. Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu. Maelezo
193. Wapigeni vita walio taka kukuuweni na kukugeuzeni muache Dini yenu kwa maudhi na mateso mpaka ing'oke mizizi ya fitina na isafike Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Wakiuacha ukafiri wao basi wamejiokoa nafsi zao na wataepukana na adhabu. Hapo basi haifai kuwafanyia uadui. Uadui hufanyiwa mwenye kuidhulumu nafsi yake akaiteketeza kwa maasi na akaacha uadilifu kwa maneno na vitendo.
194. Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu. Maelezo
194. Na pindi wakikushambulieni katika mwezi mtukufu msiache kupigana nao, kwani huo ni mtukufu kwao kama ulivyo kuwa mtukufu kwenu. Ikiwa wao watauvunja utukufu wake basi nanyi wakabilini kwa kuzilinda nafsi zenu katika huo mwezi. Na katika mambo matukufu na matakatifu pana sharia ya kisasi na kutendeana mfano kwa mfano. Anaye kushambulieni katika matakatifu yenu nanyi jilindeni na uadui huo kwa mfano wake. Na mcheni Mwenyezi Mungu, msikiuke mipaka katika kulipiza kisasi. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwanusuru wachamngu.
195. Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema. Maelezo
195. Kupambana na makafiri kunahitaji kutoa roho kama ilivyo kutoa mali. Basi toeni kwa kuandaa vita, na jueni kuwa kupigana na hawa ni kupigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi msikae tu. Toeni mali kwa ajili yake, kwani mkitofanya na mkafanya ubakhili adui atakupandeni na atakudhilini. Hapo itakuwa kama mlio jitokomeza wenyewe kwenye maangamio. Tendeni lilio kuwajibikieni kwa uzuri na vilivyo, kwani Mwenyezi Mungu hupenda anapo fanya jambo mtu alifanye vizuri.
Aya 190 mpaka 195 zinaeleza sharia ya vita katika Uislamu. Nazo zinaeleza kwa matamshi yalio wazi haya yafuatayo:
*1. Ruhusa ya kupigana imetolewa kwa ajili ya kujilinda na uvamizi wa vita wa vitendo khasa, au zikidhihiri dalili kuwa maadui wanataka vita. Vita havikulazimishwa kwa ajili ya vita wala kwa sababu ya kutaka kuwasilimisha watu kwa kuwauwa na kuwapiga vita.
*2. Kunakatazwa kuvamia au kuanza uadui kwa njia yoyote ile. Basi hapana ruhusa kufanyiwa uadui asiye pigana, wala hapana ruhusa kuvuka mipaka ya uadui wakati wa vita: basi hauliwi asiye chukua silaha, wala hakhusiani na vita bali ni mwenye kukumbwa tu na vita. Wala hauliwi mwenye kusalimu amri na akatupa silaha. Wala hapana ruhusa kuwavunjia watu nyumba zao, huko ni kupita mpaka.
*3. Mzingatie fadhila iliyo onyeshwa kwa kuamrishwa kuchamngu. Basi msivunje heshima ya wanawake kuwanajisi, hata washirikina wakifanya hayo. Wala msiwakatekate walio uwawa hata ikiwa makafiri wakiwafanyia hayo Waumini. Washirikina walimfanyia hayo Bwana wa Mashahidi, Hamza, wala Mtume s.a.w. hakutoa ruhusa kumfanyia hayo maiti yeyote, bali alikataza akasema:"Tahadharini msiwakatekate maiti".
*4. Vita vinakwisha wakiacha washirikina kuwafitini Waumini katika Dini yao, na Dini inakuwa inataka akili na nyoyo zimwelekee Mwenyezi Mungu kwa uhuru.
*5. Hapana vita katika mwezi mtukufu, nayo ni miezi ya Hija na Umra. Ikiwa washirikina watapigana katika miezi hiyo, basi Waumini nao yawapasa wapigane.
*6. Kuacha kutoka kwenda pigana na maadui wanauwa pasina nasi kupigana nao ni kuipoteza kheri na wema. Kwa haya inadhihiri kuwa vita vya Islamu vina fadhila katika sababu zinazo pelekea kuanza kwake, na vina uadilifu katika kuviendesha. Viwapi hivi na vita vya mataifa mengine ya zamani na ya sasa! Vita vyao hao ni vya uchafu, na vita vya Islamu ni vya Haki na vyenye fadhila.
semper saratoga
Nnaona mpaka hapo utagunduwa kuwa ulipozitowa hizo aya zilikuwa si kwa |context" yake.
Jee, kuna tatizo katika hayo mafundisho mema kabisa?