Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

BI.FOXY,NIMERUDI TENA "MZEE WA KUANDIKA KWA HERUFI KUBWA" KESHO NITATOA DARASA KWA WANAOTAKA KUTAJIRIKA KWENYE MCHEZO WA KAMARI AINA YA "KENO" KWANI KAMARI INA IDADI KUBWA SANA YA WAFUASI THIS TIME....NAKUSHAURI TUJUMUIKE KWA PAMOJA KATIKA DARASA LANGU NA NITARUHUSU MASWALI MBALIMBALI ....karibu bi.foxy
Salaam.
 
what do you think of scientific atrocities going on around the globe?
I can only point race of arms in describing "atrocities" in science.

The reasons are obvious, we are not in peace with our inner selves how can we be in peace with our fellow creatures?

It's simply because politicians are decision makers in the world and not realists.

Imagine the scientists are being funded to research on what will kill most and quicker! Who can fund such researches other than a demonic politician?

We have to go back and start choosing our leaders in an Islamic described manner, we won't go wrong.

Indeed its pathetic.
 
I salute you. Wherever you are take a drink i will pay.
 
As-salamu alaykum FaizaFoxy

1. Je unapenda kusoma vitabu kwa muda wako wa ziada?

2. Iwapo jibu ni ndio; Je ni vitabu gani japo vitatu vilivyobora na ungependa na wengine wavisome? - ukiacha vitabu vya dini

3. Je una lipi la kuwaambia vijana wa sasa wasio na tabia yakujisomea vitabu.

1. Naam, nnasoma sana tena sana, mpaka imekuwa tabia kuwa sipati usingizi mpaka nijisomee, na ni hivyo kwa miaka mingi sana sasa.

2. Kusema kweli katika vitabu vyote nilivyosoma hakuna kinachonishangaza na kushindwa kuchoka kukisoma kama Qur'an. Ni kitabu cha ajabu sana ambacho sijawahi kuchoka kukisoma na kila nikisoma nnakutana na ufumbuzi mpya.

Besides Qur'an. nnasoma kila aina ya vitabu, hususan vya "non fiction", kimoja ambacho nnaweza ku ki recommend ni cha "how to", kinaitwa How to win friends and influential people cha Dale Carnegie. Kingine ni cha history kinachoitwa Empires of The Monsoon cha Richard Seymour Hall, vitabu vingine nilivyotokea kuvipenda na ningependa vijana wavisome ni The Perfumed Garden cha Sheikh Nefzawi kilichotafsiriwa na Sir Richard Burton , bila kusahau Alf Lela u Lela au Arabian Nights: One Thousand and One Nights kilichotafsiriwa pia na Sir Richard Burton.

3. Vijana nnawaasa wajiwekee hata saa moja kwa siku ya kujisomea, besides, kusoma kutawapa uelewa mpana sana tena sana. Wawachane na kusoma udaku, unawaharibia mawazo mapana.
 
Faiza nilikua nina swali linanitatiza sana,
UTANI WA MAKABILA,
Utakuta kabila flani na kabila flan ni watani,
Mfano:Wahaya na Wajaluo,
Wazaramo na Wasukuma,
Nakadhalika,

Je nini ilisababisha wawe watani?

Kuna manufaa ya kabila na kabila kutaniana?

Natanguliza Shukrani.
 
Ahsante kwa swali zuri sana la "mila" hususan za kwetu Tanzania.

Nijuavyo, utani wa kimila ni pale makabila yalipopigana huko nyuma na kupatana na mwishowe wanakuwa watani.

Pia ushindani wa "nani zaidi" hupelekea watu kuwa watani, mfano "Simba na Yanga" ingawa huu hauhusiani na makabila lakini nimeutolea mfano kwa kuwa makabila mengi yalikuwa na ushindani hususan katika kucheza ngoma za asili, mashindano ya michezo ya asili. Yote yalipelekea mwishowe kuwa watani.

Napenda kuongezea kuwa, hii mila ya utani, niionavyo ni njema sana na imepelekea hapa kwetu pakawa na amani ya kuanzia zamani sana, enzi na enzi. Ukitazama nchi zingine zisizokuwa na huu utani, uhasama wa makabila hauishi.

Ningependa hili na wachangiaji wengine waliongezee kwa wajuavyo na mtazamo wao, hili ni somo kamili la "anthropology".
 
Ahsante kwa swali zuri sana la "mila" hususan za kwetu Tanzania.

Nijuavyo, utani wa kimila ni pale makabila yalipopigana huko nyuma na kupatana na mwishowe wanakuwa watani.

Pia ushindani wa "nani zaidi" hupelekea watu kuwa watani, mfano "Simba na Yanga" ingawa huu hauhusiani na makabila lakini nimeutolea mfano kwa kuwa makabila mengi yalikuwa na ushindani hususan katika kucheza ngoma za asili, mashindano ya michezo ya asili. Yote yalipelekea mwishowe kuwa watani.

Napenda kuongezea kuwa, hii mila ya utani, niionavyo ni njema sana na imepelekea hapa kwetu pakawa na amani ya kuanzia zamani sana, enzi na enzi. Ukitazama nchi zingine zisizokuwa na huu utani, uhasama wa makabila hauishi.

Ninegependa hili na wachangiaji wengine waliongezee kwa wajuavyo na mtazamo wao, hili ni somo kamili la "anthropology".
Shukrani sana, nimepata Elimu kubwa, sikua nafahamu kabla.

Wengine wanaweza kuongezea kwa mifano kama Wachaga na Wapare ilikuaje wakawa watani, nakadhalika.
 
Hivi wewe uliwahi kuolewa hapo zamani je wewe ni mke ya mtu?je katika imani yako unafungamana na kundi gani la kigaidi?
Ukisema LA kigaidi nahis umekosea swal na mantik ya swal Lako lishapotea, mana alishatoa maelezo kwa chart diagram kukanusha mahusian ya ugaid na uislamu, kidooog umuulize anafungamana na kundi gan LA mujaahedeen
 
"Qur'an 49:13.
Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu niMwenye kujua, Mwenye khabari"

Kwakuwa wewe umekuwa mwenye kurekebisha makosa yote yafanywayo na watu hapa JF kwenye lugha ya kiswahili kimaandishi, naamini una uelewa mpana wa lugha ya kiswahili, swali langu ni;

- Maandishi yenye rangi nyekundu hapo juu yana maana gani?
- Uumbaji ulifanywa na wangapi?

Natanguliza shukrani za dhati.
Mungu anapongea hutumia nafsi ya kwanza uwingi(sisi) , wala hajinati kwa nafs ya kwanza umoja (mimi). Pia refer suratul kauthar
"Hakika tumekupa kheri nyingi sana ewe Muhammad (s. a. w) "
 
Kwanini? Watu wana uliza maswali ya kejili kwako

Kwa sababu hawana "exposure". Na utakuta hiyo si kwangu tu, ukipitia nyuzi za humu JF utakuta watoa kejeli ni hao hao kwa wengi tu.

Walienda shule kusomea ujinga.
 
Habari yako Dada FAIZA FOXY...?! Hivi nini maana ya neno HASANTE (thanks) maana napata tabu.....Ukipewa, anaweza sema HASANTE.....Ukitukanwa......Ukikaribishwa......Ukipewa POLE......Ukiushinda mtihani...Hongera..HASANTE.

Naomba kufahamu maana HALISI, naona ni NENO limekaa KINAFIKI....
 
Hilo neno uliloandika "HASANTE", mimi silijuwi mimi nnajuwa Ahsante.

Ahsante ni kuonesha kuwa uliyempa ahsante kakufurahisha na kuonesha kuwa umeridhika na alichokwambia au alicho kifanya au kukufanyia.

Kama unalitumia tu kwa "kumpaka mtu mafuta kwa mgongo wa chupa" basi utakuwa ni unafik.

Mara nyingine neno hilo hilo moja huweza kuleta maana nyingine kutokana na sentensi utakavyoliongelea. Neno ahsante mara nyingine hutumika kuonesha kutokuridhika, kama vile mtu anapokukosea ukamwabia "ahsante sana kwa uliyonitendea".

Nnatumai nimeeleweka.

Ahsante.
 
Mimi nlikuwa na swali moja, kama sjakosea naona una misimamo fulani juu ya Chama, na Chama ni mfumo WA democracy, katika Soma Soma zangu vitabu na kupitia video nlizopata kusiliza za shekhe fulan ughaibun, alikuwa anaongea kuhus ubaya na uharam WA democracy.
SWALI: katika kusoma kwako vitabu, hukuwah kukutana na hii elimu ya democracy na uharam wake??? Kama ndio naomba unipe Elim mana bado naendelea kutafta
 
samahani FaizaFoxy kama nitakalouliza limeshawahi kuulizwa:
1. Jini au Majini ni nini?
2. Je, kuna aina ngapi za Majini?
3. Je, kuna uhusiano gani wa Jini au Majini na dini ya Uislamu?
 
Mimi nlikuwa na swali moja, kama sjakosea naona una misimamo fulani juu ya Chama, na Chama ni mfumo WA democracy, katika Soma Soma zangu vitabu na kupitia video nlizopata kusiliza za shekhe fulan ughaibun, alikuwa anaongea kuhus ubaya na uharam WA democracy.
SWALI: katika kusoma kwako vitabu, hukuwah kukutana na hii elimu ya democracy na uharam wake??? Kama ndio naomba unipe Elim mana bado naendelea kutafta

Asili ya neno "democracy" ni Kiyunani. "Demos" = The People, "Kratia" power, rule.

Sijasoma na kumsikia huyo Sheikh kwa hiyo siwezi comment kuhusu huyo Sheikh, kwa mtazamo wangu sioni ubaya wowote wa democracy kama haikuzuwii kuabudu kwa imani yako.
 
Back
Top Bottom