Ahsante kwa swali zuri sana la "mila" hususan za kwetu Tanzania.
Nijuavyo, utani wa kimila ni pale makabila yalipopigana huko nyuma na kupatana na mwishowe wanakuwa watani.
Pia ushindani wa "nani zaidi" hupelekea watu kuwa watani, mfano "Simba na Yanga" ingawa huu hauhusiani na makabila lakini nimeutolea mfano kwa kuwa makabila mengi yalikuwa na ushindani hususan katika kucheza ngoma za asili, mashindano ya michezo ya asili. Yote yalipelekea mwishowe kuwa watani.
Napenda kuongezea kuwa, hii mila ya utani, niionavyo ni njema sana na imepelekea hapa kwetu pakawa na amani ya kuanzia zamani sana, enzi na enzi. Ukitazama nchi zingine zisizokuwa na huu utani, uhasama wa makabila hauishi.
Ninegependa hili na wachangiaji wengine waliongezee kwa wajuavyo na mtazamo wao, hili ni somo kamili la "anthropology".