Mimi nnawaalika sana Wakristo nyumbani kwangu na nna marafiki wengi sana Wakristo kuliko unavyofikiria na wengi wengineo wanakuja kwangu bila mualiko, ni kama kwao tu.
Nnawaandalia vyakula si tu wakati wa "kwaresma" bali siku yoyote ile.
Kwanini nikuwekee sumu, umeshasikia wangapi wamekufa kwa sumu kwa ajili wameenda kula kwa Muislam?
Futa hayo mawazo ya kijinga.
Napenda uelewe kuwa wakati wa Mtume Muhammad Salla Allahu Alayhi Wasalaam, Waislam waliamrishwa na mtume wa "immigrate" kwenda Habashi na huko ilikuwa ni nchi Kikristo na Mfalme Mkristo aliwapokea na walipomueleza walipotoka akawauliza maswali walivyomjibu, akawaambia, naam, huyo kweli ni Mtume wa Mwenyeezi Mungu na akawakaribisha vizuri sana.
Ukipenda kisome kisa hicho hapa:
Migration to Abyssinia - Wikipedia