safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Yani kupelekwa kwenye swarfu kidogo unaanza kusema tunajua kiarabu mama yangu? Sasa tusiende kwa nini.lengo sio kubishana kiarabu.Tena huko usiende kabisa kwa kuwa wewe kule tulipoanzia na hapa napo unajaribu kulitafsiri neno "Nikah" Kwa Kiswahili na kulifanya ni 'kuoa". Wakati aya haijaandika Kiswahili.
Tafsiri ya Kiswahili ni kusaidia tu wasiofahamu Kiarabu na si lugha ya Qur'an. Kumbuka hilo.
Kwa kukujuza tu hata Kwa Kiswahili, neno "kuoa" haliwezakani kuwa na maana mpaka kiwepo hicho cha kuoana nacho.
Huwezi kuvaa kamdambili na makubadhi ukasema vimeoana.
Kwa Kiarabu ndio kabisa ﺗُﻨْﻜَﺢُ. "tunkahu" haliendi peke yake ni uwingi. Tena Kwa kukujuza tu, neno hilo kwa Kiarabu nje ya Qur'an hutumika kama tafsida ya kujamiiana.
Huwezi kupata "aqd" (mkataba) wa "Nikah" kama hakuna mwenza wa kisheria.
Hiyo "nikah" utaifanyaje peke yako?
Neno kuoana ndiyo sahihi Kiswahili.
Mimi sijaolewa, nimeoana na mume wangu. "Zawaj".
Na Kwa kuwa wewe na mwwenzako anaejiita Zurri mnajidai mnakijuwa Kiarabu Kwa kupachika pachika vineno vya Kiarabu kutaka kunijaribu, sasa nawaambia hivi, tuuendeshe huu mjadala Kiarabu. Ya nini tuandikie mate na wino upo?
Naanza...
منذ الموضوع هو في القرآن الكريم، ونحن جميعا نعرف اللغة العربية دعونا نواصل هذه المناقشة باللغة العربية مع جميع الاحترام الواجب
Unaweza kuwa mzuri wa kuongea kiarabu ila kamanswarfu na nahwu huwezi basi huwezi kutafsiri maandiko kwa sababu yana tekniki nyingi hasa.
Hujajibu hoja yangu ya swarfu hapo unasema tuu ooh kiswahili na hivi na vilee.
Nimekuambia hivi katika fani ya swarfu maneno huoimwa kwa mizani tofauti toffauti.
Mfano neno tunkahu limepimwa kwa mizani ya tuf'alu.
Na wazni wa tuf'alu hujulikana ni kwa mtendwa wa jambo ndiyo anayefanyiwa.
Sasa wewe kanusha hapo na ulete mizani zako kinahwu tuone huko kufanyana (kuowana) kunapimwa kwa wazni gani ?
Kwa hyo hapo tunkanu manake huolewa na sio huowana.
Ukisema kuowana tuambie umetumia wazni gani wa kiswarfu...?
الشرعة مقدم من اللغة
Sheria inatangulizwa zaidi kuliko lugha mama.
Sent using Jamii Forums mobile app