Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Bi Faiza kuna sehemu nilikusoma hapa jamii forum kwamba wewe umeshuhudia karibu awamu zote za uongozi wa nchi yetu hii .
Kwa mantiki hio wewe ni mtu mwenye upeo mkubwa kwenye mambo ya siasa na maendeleo yatokanayo na siasa kwa ujumla wake .
Kwa kuwa dhamana ya maendeleo yetu kama taifa yameshikwa na wana siasa, mimi ningependa kujua kwako mambo kadhaa kulingana na ufahamu na upeo wako kwenye nyanja hio.

(1) kuna dalili zozote tukapata maendeleo ya jumla na kutoka kwenye umaskini kama taifa chini ya uongozi utakao katika chama cha Mapinduzi ccm?

(2) kuna wakati utafika ccm wakubali kuachia madaraka kwa chama kingine?

(3) kwa idadi ya rasilimali zilizopo katika taifa hili, haiwezekani kwa kiongozi yoyote kuzitumia ili kuleta maendeleo ya moja kwa moja kama taifa bila ya kutegemea wenzetu ambao wao wametumia rasilimali zao kupiga hatua na kufikia daraja la juu la maendeleo?

(4) kuna uhakika wowote wa kupata maendeleo kama taifa kupitia uwekezaji kutoka mataifa mengine ambao wao nao wanatafuta fursa ?

(5) vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na ujasusi wanauelewa na teknologia inayotumiwa na dunia kwa sasa , kwamba ni nadra sana kuwa na vita vya msituni kama zamani zile, kwamba sasa mapambano yapo kwenye teknologia na ujasusi wa kiuchumi?

Natanguliza shukurani.
 
Bi Faiza kuna sehemu nilikusoma hapa jamii forum kwamba wewe umeshuhudia karibu awamu zote za uongozi wa nchi yetu hii .
Kwa mantiki hio wewe ni mtu mwenye upeo mkubwa kwenye mambo ya siasa na maendeleo yatokanayo na siasa kwa ujumla wake .
Kwa kuwa dhamana ya maendeleo yetu kama taifa yameshikwa na wana siasa, mimi ningependa kujua kwako mambo kadhaa kulingana na ufahamu na upeo wako kwenye nyanja hio.

(1) kuna dalili zozote tukapata maendeleo ya jumla na kutoka kwenye umaskini kama taifa chini ya uongozi utakao katika chama cha Mapinduzi ccm?
Maendeleo yapo aina mbili, tulipopata uhuru Nyerere alituaminisha tuna maadui watatu, ujinga, umasikini na maradhi. Tumeendelea kuaminishwa hivyo mpaka awamu iliyopita.

Binafsi sikubaliani na maadui hao, nnaamini kabisa adui yetu ni mmoja tu, ujinga, baada ya kupata uhuru na mpaka leo tunae.

Ujinga wa wengi wetu wa kwanza kabisa ni kuamini kuwa serikali inaweza kubadili maisha yetu kutuletea maendeleo. Binafsi naamini serikali ya mama Samia imeliona hilo na ipo mbioni kwa sera za mabadiliko. Mbadiliko ayayoyaangolea mama Samia kwa mtazamo wangu, ya kwanza kabisa ni "mindset" zetu.

Tubadilike na tuamini kuwa maendeleo yetu inabidi tujiletee wenyewe na tusingoje serikali. Hakuna cha kutuzuwia kuwa na maendeleo, serikali yetu ya sasa siyo tuliyoanza nayo tulipopata Uhuru.

Maendeleo ya pili ni ya serikali kuwa na sera nzuri na kutimiza ahadi zake za miundo mbinu inayochochea maendeleo yetu binafsi, na inafanya hivyo kwa kasi sana.

Fanya bidii binafsi, maendeleo yapo tena makubwa sana.
 
(2) kuna wakati utafika ccm wakubali kuachia madaraka kwa chama kingine?

CCM ni chama cha siasa, siamni kama itafika wakati watakubali kuwachia madaraka, isipokuwa itafika wakati watakosa madaraka, kama kitatokea chama chenye sera nzuri na kitachotimiza ahadi zaidi yake.

Tazama mifano ya nchi nyingi zenye vyama vingi, wanaachiana madaraka kwa sanduku la kura lakini malalamiko hayaishi, malalamiko yakizidi vyama pinzani wanaunda sera na kushindana kwenye boksi la kura.

Mimi ni CCM na CCM ni kama vyama vingine vyote hakikosi mapungufu yake kwa kuwa kinaendeshwa na watu na siyo malaika. Lakini uzuri wa CCM kimepata uzoefu wa kustahamiliana na kuwa na demokrasia ndani ya chama, wanajifanyia marekebishpo mengi ya ndani ambayo ukiwa siyo mmwana CCM huwezi kuyaelewa.

Uzuri wa CCM ya sasa hivi ni wasikivu na wana juhusi sana ya kutimiza yote waliyoyaahidi ili wapewe kura. Tena naona mama Samia anakwenda mbalizaidi ya kutimiza ahadi. Ni mbunifu sana na anafanya vizuri sana.

CCM inazidi kukomaa na kuwa nzuri zaidi.
 
(3) kwa idadi ya rasilimali zilizopo katika taifa hili, haiwezekani kwa kiongozi yoyote kuzitumia ili kuleta maendeleo ya moja kwa moja kama taifa bila ya kutegemea wenzetu ambao wao wametumia rasilimali zao kupiga hatua na kufikia daraja la juu la maendeleo?
Unaweza kuwa na rasilimali nyingi sana lakini huna teknolojia au soko la kutosha kuzitumia hizo rasilmali zako.

Unajuwa mataifa yaliyoendelea, hususan ya Kimagharibi, wanailinda teknolojia yao na hawakupi bila wao kufaidika, kinachotakiwa ni kuwa na sera na mikataba mizuri ya kuendeleza watu wetu kiteknolojia, lakini siyo kitu cha kufumba na kufumbuwa.

Lakini tunaelekea huko. Tunaanza kuona kidogo kidogo rasilmali zetu zikianza kutuletea mafanikio. Inachotakiwa tuongeze juhudi.
 
CCM ni chama cha siasa, siamni kama itafika wakati watakubali kuwachia madaraka, isipokuwa itafika wakati watakosa madaraka, kama kitatokea chama chenye sera nzuri na kitachotimiza ahadi zaidi yake.

Tazama mifano ya nchi nyingi zenye vyama vingi, wanaachiana madaraka kwa sanduku la kura lakini malalamiko hayaishi, malalamiko yakizidi vyama pinzani wanaunda sera na kushindana kwenye boksi la kura.

Mimi ni CCM na CCM ni kama vyama vingine vyote hakikosi mapungufu yake kwa kuwa kinaendeshwa na watu na siyo malaika. Lakini uzuri wa CCM kimepata uzoefu wa kustahamiliana na kuwa na demokrasia ndani ya chama, wanajifanyia marekebishpo mengi ya ndani ambayo ukiwa siyo mmwana CCM huwezi kuyaelewa.

Uzuri wa CCM ya sasa hivi ni wasikivu na wana juhusi sana ya kutimiza yote waliyoyaahidi ili wapewe kura. Tena naona mama Samia anakwenda mbalizaidi ya kutimiza ahadi. Ni mbunifu sana na anafanya vizuri sana.

CCM inazidi kukomaa na kuwa nzuri zaidi.
Bibi fox.
Maswali yangu kwako.

1. Ni upi mtazamo wako kuhusu katiba tulionayo sasa inafaa au haifai na kama inafaa nieleweshe ni kivipi mwananchi ananufaika nayo akiitumia kukomesha viongozi wanaoende kinyume na maadili ya uongozi.

2.ni upi mtazamo wako kuhusu tume ya uchaguzi tulionayo sasa je ni tume huru au si tume huru.
Na je tuendelee kuitumia katika chaguzi zetu za viongozi.

3.ni upi mtazamo wako kwa Rais wa nchi kupewa mamlaka ya kuteuwa na kutengua viongozi wote wa taasisi kubwa kubwa za serikali.

4.unaamini kama taifa wanataifa tutapunguza umasikini kwa njia ipi?
 
Bibi fox.
Maswali yangu kwako.

1. Ni upi mtazamo wako kuhusu katiba tulionayo sasa inafaa au haifai na kama inafaa nieleweshe ni kivipi mwananchi ananufaika nayo akiitumia kukomesha viongozi wanaoende kinyume na maadili ya uongozi.
Katiba hizi ni maandiko ya binadam kwa wakati na uelewa na matamanio ya wakati ule wanapoziaandika, hazitakaa zifae miaka yote. Ni lazima zitakuwa na mabadiliko ya mara kwa mara.

Wanasiasa wanaitumia katiba ili wakidhi matakwa yao ya kisiasa, siwashangai, wa pande zote, wanaitumia fursa.

Kuna nchi duniani zimeona mbali na hazina katiba. Kazi yao ni kutunga sheria au kuiondoa, kuirekebisha inapohitajika. Wanaenda kisheria tu, hawana katiba rasmi. Na zinaenda vizuri tu.
 
Ni wakati gani wa kutumia
"Waleiykum salaam"

Na ni upi wa kutumia
"Waleiykum salaam Warahmatullah Wakarakat "!?
Na yana maana gani?

Maana ya waalaikumsalam ni "Na kwenu amani".
Wa alaykumus salam wa rahmatullah linaweza kutafsiriwa kama "Amani na rehema za Allah ziwe pamoja nanyi pia". Mwisho, Wa alaykumu s-salam wa rahmatullahi wa barakatuh itakuwa "Amani, rehema na baraka za Allah ziwe pamoja nanyi pia".

Kwa uelewa wangu yote hayana wakati maalum, ni bashasha na shauku.
 
Oh kumbe!
Akhsante

Na hii Juma Mubarak
Na Juma Kareem
Tofauti yake ni Nini?
 
Oh kumbe!
Akhsante

Na hii Juma Mubarak
Na Juma Kareem
Tofauti yake ni Nini?
Ijumaa ya baraka (heri).

Jumma inamaanisha "Ijumaa" na Mubārak anatafsiri kama baraka au "heri".

Kareem: ni ukarim (generous.

Kwa ufupi hizo ni dua za kuombeana heri.
 
Back
Top Bottom