Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Si kweli.

Uislam haufundishi ugaidi wala haufungamani na kundi lolote la kigaidi.

Uislam unafundisha:


Qur'an 5:
32. Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.

33.Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa.
Kwa hiyo hizi aya zina maana gani?
Q9:5 Q47:4
 
Kwa hiyo hizi aya zina maana gani?
Q9:5 Q47:4
Hizo aya au namba tu?

Hiyo 9.5 anza kuisoma kuanzia 9.1 mpaka 9.15 na kuendelea utaielewa tu. Haihitaji ufafanuzi, ipo wazi. Labda kushereheshwa tu.

Hiyo ipo kwenye sura Tawba (toba).

Hata hiyo 47.4 ukianzia 47.1 ipo wazi kabisa.

Ukiisoma Qur'an bila kuikata kata inakujibu yenyewe, haina shaka.
 
Vipi msimamo wako kuhusu maulid? Maana kuna watu wanatoka povu hadi kuandaa munaqasha. Mimi sio muisilamu ila huko mitandaoni huwa nashuhudia malumbano si ya kitoto kuhusu maulidi, wengine wakisema ni ushirikina
Wanaofanya wafanye wasiofanya wasifanye. Sioni sababu kwanini wanabishana.

Mie nikikuta pilau naipiga tu, siasa zao watajuwana wenyewe.
 
Jinsi hii Mungu aliupenda Ulimwengu,Hata akamtuma Mwanae wa pekee,ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele(Yohane 3:16-18)
Safi sana, hapo ume hakikisha imani ya Kiislam kutokea ndani ya Biblia, kuwa Yesu alitumwa. Siyo Mungu mwingine aliyetumwa bali ni mtoto wa Mungu.

Wana na watoto wa Mungu kwenye biblia wako wengi sana. Haimaanishi kuwa kazaliwa na Mungu, ni kama wewe na mimi, sote ni watoto wa Mungu. Tumeumbwa nae.

Akitaka kitu husesema "kuwa" kinakuwa.

Ahsante sana.

Hata sisi Waislam tunaamini Yesu alitumwa.
 
Wewe mwanamke, dini ya Kiislamu haikutambui, soma Tirmid juzuu 1 Hadith 338 inasema Kuna vitu 3 vikipita mbele ya Muislamu anaposwaki vinaweza kukata hiyo sala navyo ni: 1. Punda, 2. Mbwa mweusi, 3. Mwanamke. Hivyo wewe ni nuksi kwa dini ya Kiislamu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Punguza hasira, jisome tena halafu ulipokosea jirekebishe.

Wakati unajirekebisha soma hii:

wataingia Peponi ikiwa watafanya wema.

Ingieni Peponi nyinyi na wake zenu kwa furaha. (43:70)
Na anaye fanya mema, na akaamini, akiwa mwanamume au mwanamke, tutamhuisha maisha ya furaha. (16:97)
Qur'an inawausia wale wanaume wanaowadhulumu au kuwadhulumu wanawake:

Enyi mlio amini! Umekatazwa
kuwarithisha wanawake kinyume na matakwa yao.
Wala usiwatendee kwa ukali.
ili mchukue sehemu ya mahari
umewapa - isipokuwa wakati
wamekuwa na hatia ya uasherati wa wazi.
Kinyume chake ishi nao
kwa msingi wa wema na usawa.
Ikiwa unachukia kwao,
inaweza kuwa hupendi kitu
na Mwenyezi Mungu ataleta kupitia humo
mengi mazuri. (4:19)

Soma zaidi Chanzo: Women in the Quran and the Sunnah
 
Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh Da Faiza.
Swali langu nilisikia kuwa kuna dua ukiomba wakati unachimba kisima basi maji hutoka ya baridi yasiyo na chumvi je unaifahamu dua hiyo?
Naomba kuifahamu pia. Natanguliza shukran
 
Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh Da Faiza.
Swali langu nilisikia kuwa kuna dua ukiomba wakati unachimba kisima basi maji hutoka ya baridi yasiyo na chumvi je unaifahamu dua hiyo?
Naomba kuifahamu pia. Natanguliza shukran
Wa Alaikum salaam. sijawahi kusikia hilo, sina ujuzi huo. Nami ntaendelea kuulizia, In shaa Allah nikipata jibu ntarudi kukufahamisha.
 
Kuna binti hapa ananiambia eti amekua kwenye mahusiano kwa mwaka mzima ila kwa kipindi.chote hicho jamaa hajawahi kumkojoza hata mara moja.

Anadai genye za muda mrefu zimesababisha awe frustrated ila anaogopa kwa vile anampenda mtu wake anaogopa akimwambia atajisikia vibaya hasa ukizingatia jamaa anadai ex galfriend wake alikua akimtangaza kuwa ni mwanaume suruali.

Binti anadai hataki kumuumiza jamaa kama alivyoumizwa na ex galfriend ila anatamani jamaa ajue ila hajui amjuze vipi bila kuumiza hisia za kipenzi chake.

Wakuu mie nimeshindwa cha kushauri naomba mnisaidie

Nimeambiwa nikujibu swali hilo, nimekuleta huku kwenye uzi wangu.


Ningefurahi sana kulijibu hili swali ingekuwa huyo binti yupo kwenye ndoa na mumewe.

Ni mambo madogo sana hayo lakini yanaweza kuwa chachu ya ndoa.

Nawashauri waache uasherati, waowane kwanza, halafu kama bado tatizo linaendelea tutajitahidi liwaondokee. Wanasema "it takes two to tango".
 
Nimeambiwa nikujibu swali hilo, nimekuleta huku kwenye uzi wangu.


Ningefurahi sana kulijibu hili swali ingekuwa huyo binti yupo kwenye ndoa na mumewe.

Ni mambo madogo sana hayo lakini yanaweza kuwa chachu ya ndoa.

Nawashauri waache uasherati, waowane kwanza, halafu kama bado tatizo linaendelea tutajitahidi liwaondokee. Wanasema "it takes two to tango".
Asante sana kwa kujali Faiza.

Ushauri wako nitampatia ausome mwenyewe ili nisiongeze wala kupunguza neno.
 
Back
Top Bottom