Wapi aliposhindwa kusimama? Nyie mnataka Sugu amuangalie tu Faiza akifanya ujinga wake kisa anampenda bintiye? Na Sugu kipindi kile si alifight sana apewe custody ya mtoto, ila watu wakaingilia kati mtoto akabaki na mama yake? As much as Sasha is important to him; his wife and his boys are very important to him too. Kushindikana kwa mahusiano yao; isiwe sababu ya mke na watoto wake kuumia. Happy na watoto wake hawana hatia, kama ambavyo Sasha hana hatia. Na hata Sugu anaelewa kuwa mkewe ana moyo wa nyama; kashatukanwa tu; wacha na yeye atoe nyongo kidogo. Amevumilia mengi sana tu, kwa sababu ya upendo na heshima kwa mumewe
Happy amekula matusi ya kila aina na anakaa kimya; yaani unataka Sugu aangalie mkewe akilia ndani na watoto wake kutukanwa kisa tu Sasha ajisikie vizuri: hell no. Kuna siku Faiza aliandikaga eti anatamani asikie mama ake Sugu amefariki au hotel yake imeungua. Haya na mama yake na hotel yake walimfanyia kitu gani? Yaani Sugu avumilie yote hayo eti kisa Sasha? Upumbavu wa Faiza, ataulipia yule mtoto wake; unless abadilike though tayari kuna damage imeshatokea. Hata hizo child support anazolalamikia, wakati mwingine ni mdomo wake mchafu ndiyo maana Sugu anakaa tu kimya. Yeye sio wa kwanza kuzaa na huyo mtoto wake ni mtoto tu kama walivyo watoto wengine wa Sugu. Atavuna jeuri yake