Hapo nyuma kidogo kuna bandiko unadai kuwa ulikatishwa ndoto yako ya kusoma ili uolewe ,sasa je ni kitu gani hasa kilichochagiza suala hilo?
1)Je familia yako ilikuwa haijiwezi kiuchumi mpaka wakaamua kukuoza ili wapoze machungu ya ugumu wa maisha?
2)Je ulikuwa machepele sana kiasi kwamba wazazi wako wakahofia unaweza kuwaletea mimba isiyo na baba nyumbani mwisho wa siku ukawatia aibu?
3)Je kulikuwa na ulazima wowote wa ziada uliopelekea wewe kuolewa angali mdogo kiumri?
Na je kama uliolewa hali ya kuwa bado hujamaliza masomo yako sasa je;
1) Huyo mume wako ndiye aliyekulipia karo ya shule na vyuo mpaka unahitimu au ni wazazi wako ndiyo waliosimamia suala hilo?
2)Ni changamoto zipi ulizokumbana nazo wakati unasoma na pia ni mke wa mtu?
3)Je ulijiunga na shule kabla hujamzalia mume wako au ulimzalia baada ya kuhitimu?
4)Kitu gani kilichopelekea urudishwe tena shule wakati hapo awali ulikatishwa masomo yako?