Familia: Hayati Magufuli aliongoza sala na nyimbo kabla ya kifo chake, alipakwa mafuta matakatifu. Pia aliombewa na Mufti

Acheni kupotosha,huyo mwanafamilia na yeye kama kasema hivyo tuna mashaka nae,kifo cha JPM kina utata kwa sababu ya kazi kubwa aliyokua anafanya ya kuwakomesha washenzi
 
Ujinga unatuumiza sana.
Ukweli ni kwamba, ukibahatika kuomba msamaha muda mfupi kabla ya kifo chako, 100% unakuwa umepokelewa na Mungu.
Lakini pia ikumbukwe kuwa, hukumu ya Mungu si kama ya mwanadamu. Mungu haangalii kosa ulilofanya bali anaangalia sababu/dhamira iliyopelekea wewe kufanya kosa hilo.
Kwa mfano, unakutana na mtu amechukua sumu, na anasema kabisa kwamba anakwenda kutia sumu maji ya mto unaotumiwa na maelfu ya watu na wanyama wengine. Bila kuchelewa unamnyonga papo kwa papo.
Katika kesi hii, Mungu hataangalia kosa ulilofanya bali ataangalia zaidi dhamira yako kufanya hivyo, ambayo ni kuokoa maelfu ya watu ambao wangekufa kutokana na sumu ambayo ingetiwa mtoni.

Lakini, wengi wanapiga kelele eti ooh, aliua watu ingawa hawaleti hoja za msingi.
Tanzania ina watu takribani milioni 60. Kama ni kweli, tujiulize, kwa nini katika watu milioni 60 wachache tu kati yao ndo wauawe? Wamefanya au walidhamiria kuleta majanga gani katika Nchi?
Kwenye hili, tuache ujinga, tusihukumu kitu tusichokijua.
 
Bonge la point[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Ni kulilia nafsi zetu tu kwani hatujui mwisho utakuwaje
Wametuacha wazuri na wabaya lakini sisi sio wa kuhukumu

Naililia nafsi yangu
 
Ungeyajua maandiko usingeandika upuuzi huu

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Mimi binafsi, bila chembe hata moja ya unafiki, naamini kwa 98% JPM yupo Mbinguni pamoja na Malaika wa Mungu.

Watanzania, tutaacha lini kufikiri kipurure namna hiyo?
Ukweli ni kwamba, Rais legelege/ mtepetevu huua watu wengi mara mia zaidi ya Rais mwajibikaji kama alivyokuwa JPM.
Kwa maana hiyo, JPM katika uongozi wake ameokoa maisha ya watanzania wengi zaidi kuliko Rais yeyote yule ukiachana na Nyerere.
Maeneo ambayo JPM ameokoa maisha ya watanzania wengi ni kama vile:-
1. AJALI ZA BARABARANI.
Ajali za barabarani ambazo zilikuwa zikigharimu maisha ya watanzania wengi zilikwisha kutokana na uongozi shupavu wa JPM.
2.VIBAKA MITAANI.
Vibaka mitaani walikwisha kutokana na Askari kufanya kazi kwa bidii wakiogopa kukutana na mkono wa JPM.
3.WAGONJWA MAHOSPITALINI.
Wagonjwa wengi mahospitalini wameokoa maisha yao kutokana na Madaktari kuacha uzembe kazini kwa kuogopa kukutana na mkono wa JPM.
Hayo ni maeneo machache tu niliyoyataja.
Kwa hiyo, Rais legelege/ mtepetevu hawezi kusimamia mambo hayo kwa nguvu zote na kusababisha kuzaliwa kwa majanga ya kila aina katika Nchi.
Majanga hayo ni pamoja na uzembe makazini, Rushwa, uonevu, wizi wa mali za umma, unyang'anyi, vibaka kutapakaa mitaani, utapeli, uhujumu wa mali za umma nk.
Hayo yote huleta madhara makubwa sana kwa Wananchi.
JPM alijitahidi sana kupigania hayo, hivyo, anakosaje kuingia Mbinguni?
Rais legelege anaweza asifike Mbinguni kutokana na kutoweza kuyasimamia hayo na hatimaye kusababisha madhara makubwa kabisa kwa Wananchi.
 
Mkuu usimpake mafuta asiyostahili mareheme.
Magufuli alijua hatma yake na malipo ya dhambi za kukusudia na kupangwa ni hapahapa duniani.
Karma is real, you reap what you sow.
 
Mkuu usimpake mafuta asiyostahili mareheme.
Magufuli alijua hatma yake na malipo ya dhambi za kukusudia na kupangwa ni hapahapa duniani.
Karma is real, you reap what you sow.
Mkuu Magufuli alikuwa anamwamini Mungu Yehova kupitia Yesu Kirsto! Elewa imani hiyo nitofauti nayakwako! Endelea kuabudu majini! Mungu wetu anaupendo ukimuomba msamaha anasamehe!
 
Mkuu Magufuli alikuwa anamwamini Mungu Yehova kupitia Yesu Kirsto! Elewa imani hiyo nitofauti nayakwako! Endelea kuabudu majini! Mungu wetu anaupendo ukimuomba msamaha anasamehe!
Mtu anaye mwamini Mungu wa kweli haui mtu kwa roho ya kisasi, haibii kondoo wake, hatukani ovyo wananchi wake,kama ulivyo ambiwa kaa kwako na mavi yako!!!

Wala hafungi watu magerezani kwa hila, kuna mzee anaitwa Shamte, kafia gerezani kwa kubambikwa uhujumu!

Ukimpenda mtu wa namna hiyo hata Mungu hayupo moyoni mwako.
 
Kuna ukweli hapa
 
Tatizo watu hawajaamini kuwa yule mwovu alishakufa zamani na sasa mwili wake unaliwa na funza!
 
Hakuna mtawala yeyeto duniani amewahi kupambana na watu na akawashinda si farao, nebukadineza, hitter,nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…