Familia: Hayati Magufuli aliongoza sala na nyimbo kabla ya kifo chake, alipakwa mafuta matakatifu. Pia aliombewa na Mufti

Kama alipata neema hio ya kitubio Mungu you mwema.Nami kwa niaba ya wote namuombea msamaha Mola amuepushe na adhabu zote.
Yaliyopita yashapita
 
Mimi mwenyewe ni Padre.

Uhalisia ndio huo jombaa.
Nje ya mada Padre kwanini kwenye ibada ya leo pale uwanjani askofu na mapadre walivaa majoho meupe badala ya zambarau kama tunavyowaonaga kwenye ibada za mazishi
 
Poleni sana ndugu wafiwa Mungu awape nguvu ktk kipindi hiki kigumu
 
Lakini Mungu naye angejiongeza tu akamsamehe huyu mzee wetu mpendwa,maana kumuweka moto mmoja pamoja na akina Osama bin Laden haitaleta picha nzuri kwa watakaokuwa peponi na inaweza kuzua taharuki huko peponi
 
Ndio maana ya toba, imetajwa hapo
Kumbe unaweza ukafanya ubaya wa kila aina alafu ukiumwa ukahisi kamba inaenda katika unatubu na kuingia mbinguni..

Kama ndio hivyo huyu Mungu atakuwa wa upendeleo sana..
 
Angeanza kabisa kiomba msamaha kwa wanafunzi wa special diploma ya ualimu UDOM aliowafukuza kama mbwa japo walikua na haki zote. Maana wale watoto wengi walikia under 18 na wanatoka mikoa mbalimbali ikabidi walale stand iliumiza sana
 
R.I.P

Ben Saanane
Azory Gwanda
Lwajabe
Aqwelina

Na wengineo.
Pole kwa wanafunz wa specila diploma ya ualimu Udom waliofukuzwa kama mbwa na kulala standa kisa hawana nauli wengi wao wakiwa under 18
 
Magufuli yupo siti ya mbele mahali pema peponi!
 
Kwa hiyo baada ya hapo ndo akafa? Uongo mwingine bana chee
 
Acha uongo
 
Ni Mungu pekee ndiye anayejua hatma ya marehemu.

Huku duniani ni kubahatisha tu na kuweka Kampeni zisizokuwa na ushawishi wowote kwa maamuzi yake juu ya marehemu.
 
Hao watu Mashekhe na Maaskofu walikwenda mzee alikuwa keshazimika. Sasa hiyo sala ya toba aliongozwa akiwa Marehemu?
Mkuu msemaji wa familia amesema alikuwa anaimba means alikuwa bado hajafariki,sijapenda pm alivyotuongopea kuwa ni mzima anatusalimia!!
 
Umedadavua vema kama hakufanya hayo ni ngumu kupata msamaha maana Mungu keshasema wazi wazi hivi
[emoji116]
14 Tena, nimwambiapo mtu mwovu, Hakika utakufa; kama akighairi, na kuiacha dhambi yake, na kutenda yaliyo halali na haki;
Ezekieli 33:14

15 kama mtu mwovu akirudisha rehani, na kumrudishia mtu mali yake aliyomnyang'anya, akizifuata sheria za uzima, asitende uovu wo wote; hakika ataishi, hatakufa.
Ezekieli 33:15

16 Katika dhambi zake zote alizozitenda, hata mojawapo haitakumbukwa juu yake; ametenda yaliyo halali na haki; hakika ataishi.
Ezekieli 33:16

Kama hakufanya haya wala hakutoa maagizo hayo basi hana asubuhi
 
Akimuomba mola wake inatosha na ndio maana ya mpako wa mafuta matakatifu kwetu sisi wakatoliki ni maana kubwa sana.
Mpako wa mafuta sio kanuni ya Mungu kumsamehe mtu makosa yake

Anatakiwa kufanya haya

14 Tena, nimwambiapo mtu mwovu, Hakika utakufa; kama akighairi, na kuiacha dhambi yake, na kutenda yaliyo halali na haki;
Ezekieli 33:14

15 kama mtu mwovu akirudisha rehani, na kumrudishia mtu mali yake aliyomnyang'anya, akizifuata sheria za uzima, asitende uovu wo wote; hakika ataishi, hatakufa.
Ezekieli 33:15

16 Katika dhambi zake zote alizozitenda, hata mojawapo haitakumbukwa juu yake; ametenda yaliyo halali na haki; hakika ataishi.
Ezekieli 33:16
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…