Familia: Hayati Magufuli aliongoza sala na nyimbo kabla ya kifo chake, alipakwa mafuta matakatifu. Pia aliombewa na Mufti

Kwahiyo wamasai kwa mila zao hawataingia mbinguni
 
Kumbe unaweza ukafanya ubaya wa kila aina alafu ukiumwa ukahisi kamba inaenda katika unatubu na kuingia mbinguni..
Kama ndio hivyo huyu Mungu atakuwa wa upendeleo sana..

28 Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu.
29 Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende.
30 Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda.
31 Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.

Mathayo 21:28-31
 
Hao watu Mashekhe na Maaskofu walikwenda mzee alikuwa keshazimika. Sasa hiyo sala ya toba aliongozwa akiwa Marehemu?
Kigogo hii aliisema kuwa viongozi hao wa dini walitoka ndani wakiwa wanalia
 
Ilikuwaje Mufti tu ndiyo alikuwepo Kumuombea lakini Roman Catholic Cardinal Ruwa'ichi Thadeo hakuwepo au hata tu wa Madhehebu mengine? Nayasubiri Majibu ya Wanafamilia Ndugu au kama unaweza Kuwajibia pia itapendeza. Why Mufti was the Special One to him especially on his last Prayers before he died?
 
Hii sasa ni blah blah! Huyo mtu, siku zote alizokuwa anaumwa, alifichwa! Hizo SAKRAMENTI alipewa na wauguzi wake?
Waendelee kutuongopea hapa hapa Duniani tu. Huko alikoenda hakuna KUONGOPEANA!


Kazi ipo!​
 
Kumbeeeee.. basi Biblia inatufundisha tusiwe wema mpaka tukikaribia kufa ndio tutubu
 
Alikuwepo Pengo na Padri Makubi.
 
Nje ya mada Padre kwanini kwenye ibada ya leo pale uwanjani askofu na mapadre walivaa majoho meupe badala ya zambarau kama tunavyowaonaga kwenye ibada za mazishi
Zambarau ni rangi ya maombolezo. Leo ilikuwa sikukuu ya kumwaga rais wetu alietutoka.

Tunachukulia kifo kwa mtazamo tofauti, ni Safari kutoka hatua moja kwenda nyingine nzuri zaidi. Hivyo badala ya kuhuzunika tunasherekea mwenzetu kutoka katika hatua moja ya chini kwenda hatua ya juu zaidi.
 
CCM ni waongo sana.
Wanataka kutuaminisha kuwa mwenyekiti wao ni mtu Safi,tusikumbushie makosa yake.
Angesema neno kuhusu uchaguzi mkuu wa 2020 na wasiojulikana tungeelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…