Familia: Hayati Magufuli aliongoza sala na nyimbo kabla ya kifo chake, alipakwa mafuta matakatifu. Pia aliombewa na Mufti

Familia: Hayati Magufuli aliongoza sala na nyimbo kabla ya kifo chake, alipakwa mafuta matakatifu. Pia aliombewa na Mufti

Huyo Sauli unamjua? Unauhakika gani kama no kweli au ni hadithi za kusadikika?
Am dealing with a typical homo sapiens ambaye Hana imani na maandiko matakatifu yakiyoandikwa baada ya mafunuo,

Nimefunga huu mjadala Mimi na wewe hatushahabiani kwenye mlengo wa imani.
 
Tunaingilia majukumu ya Mungu kujadili kama wa mbinguni au laa...tuendelee kumuombea dua njema tuu na tuishi kwa kusamehe ndio dawa kubwa...
 
Kuna makosa aina mbili katika imani;

1) Kumkosea Mungu.

2) Kumkosea Mwanaadamu.

Kuna baadhi ya makosa mungu hasamehi mpaka ukamuombe msamaha uliemkosea kwanza, mfano Kulala na Mke/Mume Wa Mtu. Hapa kwa mungu kosa ni kuzini, kwa mwanaadamu umemchafulia haki yake inayotambulika mpaka mbinguni.

Msamaha kwa mungu unakubalika kwa kuapa kutokurudia tena kosa, sambamba na kurekebisha ulipo kosea (Mfano umefunga mtu gerezani kwa chuki, unapaswa kumwachia huru kwanza na kumpa fidia stahiki kwa kifungo ulichompa, halafu ndio unaomba msamaha kwa mungu na kuapa kutokurudia tena kufunga mtu asie na hatia - Ukiua mtu asie na hatia, unapaswa kukiri kosa na kuwaomba msamaha wana familia kwanza then unarudi kwa mungu kutubia na kuapa kutokurudia tena kuua).

Then walio dhulumiwa na kufungwa magerezani kwa chuki basi aliwaachia kabla ya kutubia dhambi zake?

Alikwenda kuwaomba msamaha familia za waliopoteza maisha yao kwa kivuli cha watu wasiojulikana?

Alirudisha haki za watu waliopewa kesi za uhujumu uchumi ili walipishwe fidia?

Alirudisha haki za watu waliobambikozwa KODI na MAKOSA iwe ya trafik barabarani n.k?

Ni rahisi sana kumnyoshea kidole mtu mwingine hata kwa dhambi unazozitenda kila siku.

Halafu kuna fikra potofu kwamba kuna dhambi ndogo na kubwa. Kwa Mungu, dhambi ya kuua, ya kuzini, ya kuiba, etc. ziko sawa na zote zinasameheka kwa degree ile ile. Dhambi pekee isiyosameheka ni ya kutomuamini Mungu. Usipomuamini Mungu imekula kwako!
 
Am dealing with a typical homo sapiens ambaye Hana imani na maandiko matakatifu yakiyoandikwa baada ya mafunuo,

Nimefunga huu mjadala Mimi na wewe hatushahabiani kwenye mlengo wa imani.
Umesahau kuwa wewe pia ni Homo Sapiens?

Au wewe ni Zinjanthropus?
 
Lakini jana wakati anahojiwa na UTV Shekh Mkuu Zuberi alipoulizwa kwamba alipomtembelea wàkati anaumwa Mh. Hayati Rais Magufuli, Shekh alijibu kwamba kwa siku za karibuni toka kuugua kwake sijawahi kumtembelea..."

Hili la wanafamilia kwamba aliombewa na Shekh Zuberi wamelitoa wapi?
Kwani mtu hawezi ombea mtu mwingine kwa simu?
 
Hiyo Sakramenti ya mwisho ya Mpako Mtakatifu hufanywa kwa mgonjwa ambaye tu karibu na kufa , sasa mpaka hayo yote yanafanyika lakini bado wananchi walikuwa wanaambiwa jamaa anafanyakazi na kwamba tu mzima kabisa.?!
 
Back
Top Bottom