Familia: Hayati Magufuli aliongoza sala na nyimbo kabla ya kifo chake, alipakwa mafuta matakatifu. Pia aliombewa na Mufti

Familia: Hayati Magufuli aliongoza sala na nyimbo kabla ya kifo chake, alipakwa mafuta matakatifu. Pia aliombewa na Mufti

Amefanya toba lakini bado kama kuna wanaoendelea kulia kwasababu yake toba haitakuwa na maana. Ndugu za akina Ben Saanane, waliofungwa bila hatia n.k

Hawezi kuwa redeemed unless wote walioteseka kwa mkono wake wamepata haki.
Ben saa nane atarudi sasa!! walio potezwa watajulikana tunachotaka sisi kujua tu hata km alikufa tuomboleze kuwa ndugu yetu katutoka.kwa style hii tuweke kumbukumbu km shujaa!!

ila Damu ya tundu lisu italia na wengi... duuu... kalienda kuroga kajamaa haka
 
Hii sasa ni blah blah! Huyo mtu, siku zote alizokuwa anaumwa, alifichwa! Hizo SAKRAMENTI alipewa na wauguzi wake?
Waendelee kutuongopea hapa hapa Duniani tu. Huko alikoenda hakuna KUONGOPEANA!
Lies! Lies! Lies by liars!!!
 
Marehemu (Tingatinga) nitamkumbuka kwa UHODARI wa kupiga NGOMA.....
Tuache hili mkuu. Familia imesema aliongoza sala na nyimbo kabla ya kufariki. Tuachie hapo hapo.
 
Basi sawa.
Maza tukishamaliza kuzika kimbiza wote na tuanze alifu kwa ujiti.
Nani anachangisha pesa za mchango ili nimchangie maza aweze kulifanikisha hili?
Nalog off
 
Basi mtangazeni kuwa ni Mtakatifu kama Nyerere. Maana huwa mnasema ni Nyerere wa pili
Ilikua inadhaniwa hivyo na kanisa katoliki uganda. ila katika mchakato wake kulionekana na dosari hivyo mpango ulifeli hivyo kanisa la roma halikuendelea na huo mchakato sababu ya dosari katika maisha ya Nyerere alietarajiwa kutangazwa mtakatifu na kanisa, dosari zenyewe zipo nyingi
 
Inashangaza sana. Bora hata mngalitujuza hali ya mzee watu wange muomba Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi kwa magumu alokua anapitia kama alivyo kuwa anatuomba tumwombee kila siku
Sasa tunaona mnaleta mapichapicha hapa.
Vile mlitujuza kuwa alikuwa okay anapiga kazi home kupitia wale wajumbe wa uongo tena wakiwa wamesimama kwenye mimbari ya nyumba za ibada
Leo mtuache kwanza tuzike then tutawahoji hayo yote
 
Kuna makosa aina mbili katika imani;

1) Kumkosea Mungu.

2) Kumkosea Mwanaadamu.

Kuna baadhi ya makosa mungu hasamehi mpaka ukamuombe msamaha uliemkosea kwanza, mfano Kulala na Mke/Mume Wa Mtu. Hapa kwa mungu kosa ni kuzini, kwa mwanaadamu umemchafulia haki yake inayotambulika mpaka mbinguni.

Msamaha kwa mungu unakubalika kwa kuapa kutokurudia tena kosa, sambamba na kurekebisha ulipo kosea (Mfano umefunga mtu gerezani kwa chuki, unapaswa kumwachia huru kwanza na kumpa fidia stahiki kwa kifungo ulichompa, halafu ndio unaomba msamaha kwa mungu na kuapa kutokurudia tena kufunga mtu asie na hatia - Ukiua mtu asie na hatia, unapaswa kukiri kosa na kuwaomba msamaha wana familia kwanza then unarudi kwa mungu kutubia na kuapa kutokurudia tena kuua).

Then walio dhulumiwa na kufungwa magerezani kwa chuki basi aliwaachia kabla ya kutubia dhambi zake?

Alikwenda kuwaomba msamaha familia za waliopoteza maisha yako kwa kivuli cha watu wasiojulikana?

Alirudisha haki za watu waliopewa kesi za uhujumu uchumi ili walipishwe fidia?

Alirudisha haki za watu waliobambikozwa KODI na MAKOSA iwe ya trafik barabarani n.k?
Kumkosea Mungu yupi?
kuna Kumkosea Mungu anayeabudiwa kupitia Ushoga,Ugaidi,Ufisadi, Ubeberu nk.Huyu ukigusa wahumini wake kelele nyingi sana na Miruzi
Lakini kuna Kumkosea Mwenyezi Mungu aliye hai ,huyu hategemei uwakosee wanadamu ndipo akushukie,huyu mipango yake haipimiki na njia zake ni ngumu sana kuzijua.Alimwacha Mfalme wa Misiri Farao awatumikishe na kuwatesa wana wa israel miaka mingi wakanungunika na kulalamika lakini muda wa ukombozi ulikuwa bado.
Kwa hiyo tambua kwamba ukiongoza wananchi takribani millioni 50 Usisahau kwamba kila mwananchi ana Mungu wake na Ikiwa aliyekupa Nguvu ya Utawala si Mungu wao lazima Upinzani utokee na kelele nyingi haswa za wenye Mungu asiye na Nguvu.
 
35 Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu; 36 Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 40 Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.

Mathayo 22:35-40
Ndugu yangu usipotoshe watu. Hakuna kifungu chochote kwenye Injili kinachosema au kusisitiza kuwa ili mtu asamehewe dhambi zake basi ni lazima kwanza akawaombe msamaha wale aliowakosea.
Ingekuwa hivyo basi hata Mfalme Daudi asingesamehewa dhambi yake ya kulala na Mke wa askari wake kisha kuamuru askari yule atangulizwe mbele vitani na kuachwa afe.
Mfalme Daudi alipotubu hiyo dhambi mbele ya MUNGU, alisamehewa na wala hakuambiwa akawaombe kwanza msamaha ndugu za yule askari aliyeuwawa.
YESU KRISTO alishakufa na kufufuka kwa niaba ya "dhambi" zetu, hivyo msamaha wa dhambi hauna "masharti" yoyote yale zaidi ya kutubu na kubatizwa basi.
 
Ndugu yangu usipotoshe watu. Hakuna kifungu chochote kwenye Injili kinachosema au kusisitiza kuwa ili mtu asamehewe dhambi zake basi ni lazima kwanza akawaombe msamaha wale aliowakosea.
Ingekuwa hivyo basi hata Mfalme Daudi asingesamehewa dhambi yake ya kulala na Mke wa askari wake kisha kuamuru askari yule atangulizwe mbele vitani na kuachwa afe.
Mfalme Daudi alipotubu hiyo dhambi mbele ya MUNGU, alisamehewa na wala hakuambiwa akawaombe kwanza msamaha ndugu za yule askari aliyeuwawa.
YESU KRISTO alishakufa na kufufuka kwa niaba ya "dhambi" zetu, hivyo msamaha wa dhambi hauna "masharti" yoyote yale zaidi ya kutubu na kubatizwa basi.
Hebu angalia vizuri. Umeni-quote lakini sijazungumza chochote kati ya hayo unayoyasema nimepotosha. Mimi nimeweka kifungu cha biblia Mathayo 22:35-40, cha ajabu naona umequote post yangu halafu unazungumza mambo tofauti kabisa. Kwa ufupi sijakusoma kabisa
 
Hebu angalia vizuri. Umeni-quote lakini sijazungumza chochote kati ya hayo unayoyasema nimepotosha. Mimi nimeweka kifungu cha biblia Mathayo 22:35-40, cha ajabu naona umequote post yangu halafu unazungumza mambo tofauti kabisa. Kwa ufupi sijakusoma kabisa
Wewe uliponi quote mara ya kwanza na kuniwekea hiyo Mathayo 22:35-40, kifungu hicho kilikuwa kinaenndana na hoja yangu?
 
Msemaji wa familia ya hayati Magufuli amesema mpendwa wao kabla ya kufa alibahatika kuongoza sala ya maombi ya kumuombea pamoja na nyimbo.

Pia alipata sakramenti ya toba na mafuta matakatifu.

Kadhalika Mufti wa Tanzania sheikh Zubeir alimuombea.

Katika maisha ya binadamu hii ni neema kubwa ambayo watu wengi huikosa wawapo kufani.

Binafsi sitaomboleza kwa kuvaa nguo nyeusi bali nitavaa nguo nyeupe kwa ajili ya shukrani kwa Mungu kwa maisha ya John hapa duniani.

Maendeleo hayana vyama!
Vipi kuhusu msafara wa "wataalam" kutoka Chato?
 
Back
Top Bottom