Familia: Hayati Magufuli aliongoza sala na nyimbo kabla ya kifo chake, alipakwa mafuta matakatifu. Pia aliombewa na Mufti

Familia: Hayati Magufuli aliongoza sala na nyimbo kabla ya kifo chake, alipakwa mafuta matakatifu. Pia aliombewa na Mufti

Kiimani, Marehemu Magufuli, kama alipata nafasi ya kuomba masamaha kwa dhati ya dhamira ya moyo wake, wakati wa mwisho wa safari yake hapa Duniani, atakuwa alipata msamaha kamili wa dhambi zake. Ndivyo maandiko yanavyotuambia.

Neno la Mungu linasema,

Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo ya dhambi, nami nitawapumzisha.

Andiko jingine lasema, Ijapokuwa dhambi zako ni nyekundu, zitakuwa nyeupe kama theluji.

Kama tu wana wa Mungu, tunayetaka atusamehe dhambi zetu, nasi tunastahili kusamehe. Hivyo, yatupasa kumsamehe marehemu tunapoona alitukosea.

"Utusamehe makosa yetu kama nasi tunavyowasamehe wale waliotukosea"
 
Msemaji wa familia ya hayati Magufuli amesema mpendwa wao kabla ya kufa alibahatika kuongoza sala ya maombi ya kumuombea pamoja na nyimbo.

Pia alipata sakramenti ya toba na mafuta matakatifu.

Kadhalika Mufti wa Tanzania sheikh Zubeir alimuombea.

Katika maisha ya binadamu hii ni neema kubwa ambayo watu wengi huikosa wawapo kufani.

Binafsi sitaomboleza kwa kuvaa nguo nyeusi bali nitavaa nguo nyeupe kwa ajili ya shukrani kwa Mungu kwa maisha ya John hapa duniani.

Maendeleo hayana vyama!
===

Msemaji wa familia ya Hayati Magufuli Ngusa Samike amesema "kabla ya kifo chake Rais Magufuli aliongoza sala na nyimbo akiwa na Madaktari na Wauguzi wake."

Alisema kabla ya kifo pia, "Mwadhama Polycap Kardinali Pengo na Paroko wa Parokia ya St. Peter Padre Alister Makubi walimpatia Rais Magufuli huduma ya kiroho ya mpako mtakatifu,"

"Pia Shekhe Mkuu wa Tanzania Mufti Aboubakar Zubeir naye alimfanyia maombi kabla ya kifo chake."
Hiyo sala aliongoza akiwa kwenye ventilator? 🙄
 
Inaonekana kukosekana kwa msimamo yaan mkristo ambaye anamwamwini KRISTO hawezi kuombewa na sheik ( akifanya ivo atakuwa haamin anachokiamin a.k.a imani kachumbari
 
Amefanya toba lakini bado kama kuna wanaoendelea kulia kwasababu yake toba haitakuwa na maana. Ndugu za akina Ben Saanane, waliofungwa bila hatia n.k

Hawezi kuwa redeemed unless wote walioteseka kwa mkono wake wamepata haki.
AMEN
 
Kiimani, Marehemu Magufuli, kama alipata nafasi ya kuomba masamaha kwa dhati ya dhamira ya moyo wake, wakati wa mwisho wa safari yake hapa Duniani, atakuwa alipata msamaha kamili wa dhambi zake. Ndivyo maandiko yanavyotuambia.

Neno la Mungu linasema,

Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo ya dhambi, nami nitawapumzisha.

Andiko jingine lasema, Ijapokuwa dhambi zako ni nyekundu, zitakuwa nyeupe kama theluji.

Kama tu wana wa Mungu, tunayetaka atusamehe dhambi zetu, nasi tunastahili kusamehe. Hivyo, yatupasa kumsamehe marehemu tunapoona alitukosea.

"Utusamehe makosa yetu kama nasi tunavyowasamehe wale waliotukosea"
Kuna dhambi za aina mbili kwa mujibu wa amri kumi za Mungu,kumkosea Mwenyezi Mungu na kumkosea mwanadamu.Aliomba toba ipi hapo.
Kwa wanadamu aliowaumiza je aliomba msamaha?
 
Kuna dhambi za aina mbili kwa mujibu wa amri kumi za Mungu,kumkosea Mwenyezi Mungu na kumkosea mwanadamu.Aliomba toba ipi hapo.
Kwa wanadamu aliowaumiza je aliomba msamaha?
Hakuna ajuaye. Itabakia kuwa ni siri kati yake na Muumba
 
Nimesoma comments zote. Jamaa alikuwa mbaya na kadri ubaya na dhulma alizofanya zinazidi kudhihirika ndiyo Moto unazidi kuchochewa. Na aungue maana katesa wengi.

Juzi jumanne tarehe 23 November 2021 nilimsikia mtangazaji Sudi Mnete wa DW mchana kwenye kipindi cha kinagaubaga, akimuhoji mke wa Azory Gwanda. Aisee inatia huruma sana. Yule mtu alikuwa mwovu sana
 
Ndio maana ya toba, imetajwa hapo
Utaratibu wa toba kanisa katoliki:
  • Tafakari dhambi zako.
  • Omba msamaha uliowakosea.
  • Ungama dhambi zako mbele ya Padre.
  • Timiza kitubio utakachopewa na Padre, na azimia kutotenda dhambi tena.

Mh. Magufuli alitenda dhambi nyingi hadharani dhidi ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa jumla, kwa mawazo, maneno na matendo yake. Hakuwahi kuomba msamaha, hasa zile dhambi alizotenda hadharani. Kama aliwaomba msamaha kina Tundu Lissu, familia ya Ben Saanane etc sijui. Ingawa hakuwatenda yeye moja kwa moja, lakini ndiye alikuwa kiongozi mkuu aliyepaswa kuhakikisha haki inatendwa na ionekane wazi imetendwa.
 
Inaonekana kukosekana kwa msimamo yaan mkristo ambaye anamwamwini KRISTO hawezi kuombewa na sheik ( akifanya ivo atakuwa haamin anachokiamin a.k.a imani kachumbari
Mtu yeyote anaruhusiwa kumwombea binadamu mwenzake jema lolote. Wengine sio waumini wa MUNGU ila ile roho ya ubinadamu inajikuta kufanya hivyo. Saa ingine hata wanyama ikitokea shida wanataka wawe salama wote.
 
Ukiwa muumini wa vyama vya giza siku yako ikifika unajua, taarifa unakuwa nazo tayari hofu,mashaka na mahangaiko uanza thus wapo wanamuziki walianza kuimba nyimbo za vifo tupac, michael jackson,kanumba,nk hizi zote huwa wanaiambia Jamii kuhusu kile kinachokwenda wakuta wanakua washaona umauti mbele,so mtu akikuambia mniombee usipuuze mtafutie toba Ili umnasue,wengi uingia vyama vya Siri kwa upumbavu wanapopata kweli ujutia Sana wakililia toba but shetani hawezi kukuruhusu uogelee ufike nchi Kavu ni lzm akunyweshe maji, huwezi mshinda shetani kama huna Mungu.
 
Mtu yeyote anaruhusiwa kumwombea binadamu mwenzake jema lolote. Wengine sio waumini wa MUNGU ila ile roho ya ubinadamu inajikuta kufanya hivyo. Saa ingine hata wanyama ikitokea shida wanataka wawe salama wote.
Sio kweli, toba ni majuto dhidi ya dhambi ulizomkosea Mungu au watu.
Je kama ajutii dhambi zake, kumuombea msamaha ni kumpigia Mungu kelele.
 
Inaonekana kukosekana kwa msimamo yaan mkristo ambaye anamwamwini KRISTO hawezi kuombewa na sheik ( akifanya ivo atakuwa haamin anachokiamin a.k.a imani kachumbari
Kwa nini asiombewe? hata Osama bin Ladin alishindwa kutoombewa na Wakristo. Unamzuiaje mtu anayekuombea? Akikuombea, unaombewa. Sivyo?
 
Wakati hayo yote yanafanyika, Waziri Mkuu anatudanganya tu! na kutushangaa tunao muulizia Marehemu!

Tena akaenda mbali zaidi kwa kutuuliza tulitaka tumuone wapi eti! Magomeni!! Kariakoo sokoni! 🤔
Halafu akaja kuwa Mwenyekiti wa mazishi.
Sheria ipi inasema kiongozi wa nchi ugonjwa wake ni siri.
 
Nimesoma comments zote. Jamaa alikuwa mbaya na kadri ubaya na dhulma alizofanya zinazidi kudhihirika ndiyo Moto unazidi kuchochewa. Na aungue maana katesa wengi.

Juzi jumanne tarehe 23 November 2021 nilimsikia mtangazaji Sudi Mnete wa DW mchana kwenye kipindi cha kinagaubaga, akimuhoji mke wa Azory Gwanda. Aisee inatia huruma sana. Yule mtu alikuwa mwovu sana
Mzee Mungu hawazi na hafanyi kama ww bnadamu unvyofkiri na kuwaza,Maguful unasema alkuw mbaya,sawa,je aliupita ubaya wa paulo alyewaua na kuwatesa vibaya wakrsto kila alpokutana nao?na leo haitwi paulo tu anaitwa Mtakatifu Paulo,Mungu ana huruma sku zote,Mtakatfu Paulo sasa hv kaketi kuume kw Mungu baba though aliumiza watu wa Mungu na kuwaua!chamsingi ww unayejiona malaika jiombee uweze kuwa na mwsho mwema na sio kuzungumzia watu ambao hujui wapo wapi sasa hivi!SHAME ON YOU!!!!!MUNGU HAWAZI NA HAFANYI NA HATAKUJA KUFANYA NA KUWAZA KAMA MWANADAMU ANAVYOWAZA ABADANI NA KIKUBWA MUNGU HAPANGIWI.
 
Mke wa Azory alihojiwa BBC aisee hadi huruma anasema kinachomtesa zaidi ni mtoto wake Mdogo amsumbuae KILA siku "mama baba yupo wapi ulisema atarudi mbona arudi" kumbuka wakati Azory anatekwa shambani mkewe wake alikuwa ni mjamzito ndo hicho kitoto kishakuwa kikubwa.
So laana hii itawafikia wote walioshiriki kwenye mchakato mzima wa utekaji akiwemo dereva na watu wale wanne waliokuwa kwenye gari siku ya mateko,Mungu ameona na alishaanza na boss wao so nao wajiandae,wote walioshiriki kufanikisha mpango wa shetani kuwatoa kafara Lwajaba, Azory,ben,Elisha Eliya,Dilunga,na wengi tu wameuliwa kwa kuhisiwa ni kigogo,pia laana hii isiwaache hata wale askari waliokuwa zamu kulinda Area D na kuruhusu magaidi wakamshambulia Lisu Dodoma na wote waliotolewa kafara na shetani.Shetani hana huruma akamtoa kafara mjumbe wake baada ya kukiuka mashariti.
 
Mzee Mungu hawazi na hafanyi kama ww bnadamu unvyofkiri na kuwaza,Maguful unasema alkuw mbaya,sawa,je aliupita ubaya wa paulo alyewaua na kuwatesa vibaya wakrsto kila alpokutana nao?na leo haitwi paulo tu anaitwa Mtakatifu Paulo,Mungu ana huruma sku zote,Mtakatfu Paulo sasa hv kaketi kuume kw Mungu baba though aliumiza watu wa Mungu na kuwaua!chamsingi ww unayejiona malaika jiombee uweze kuwa na mwsho mwema na sio kuzungumzia watu ambao hujui wapo wapi sasa hivi!SHAME ON YOU!!!!!MUNGU HAWAZI NA HAFANYI NA HATAKUJA KUFANYA NA KUWAZA KAMA MWANADAMU ANAVYOWAZA ABADANI NA KIKUBWA MUNGU HAPANGIWI.
Paulo alitubu kwa Mola wake na akamwahidi Mungu atamtumikia kwa kupambana na shetani kama njia ya malipizi jinsi alivyomtenda Mungu na Mtume Paulo ndie aliyeusambaza Ukristo ulimwengu na kuwafanya watu wengi wawe wafuasi wa Kristo na kumjua Mungu hata sasa.
Thus tunaona na tukishuhudia waliokuwa waganga, wachawi,majambazi wakubwa wameuwa watu wengi sana kwa uchawi, risasi,nk wakatubu wanalia Sana na kujutia upumbavu waliotenda wameamua kutoa Siri zote za giza kwa kupambana na shetani kwa kuhubiri habari za Mungu wakijitoa kwa bidii.Wapo leo watumishi wa Mungu wakubwa kabisa ambao kabla walikuwa wachawi, majambazi, waganga wameua watu wengi sana.
Huwezi ombewa toba ukiwa coma,bali unajiombea mwenyewe,
 
Back
Top Bottom