Familia inayomuweka Marehemu kwenye Sanduku/Jeneza la kuanzia laki 3 kwenda Juu,hiyo Familia itakuwa na matatizo ya kiakili

Familia inayomuweka Marehemu kwenye Sanduku/Jeneza la kuanzia laki 3 kwenda Juu,hiyo Familia itakuwa na matatizo ya kiakili

hii imetokea hv karibuni kwenye familia yangu...mungu ampe kauli thabiti marhem anko,yaani hali inasikitisha...
kipindi anaumwa kula ilikua ya shida kwenye msiba watu wanagombania daftari kuandika majina ya mchango daaah

Jamii zetu zina shida ya kiakili sana mkuu!
 
Ukihitaji salamu kutoka kwangu nenda kwanza kwa CAG ukasome ripoti ya Mwaka uliyopita,Tofauti na hapo utaambulia chuya!

Huwa nashangazwa sana na namna ambavyo Familia nyingi zimekuwa zikihaha,kukabana na kushikana mashati wakati wa Msiba eti kisa tu ipatikane pesa ambayo inatakiwa iende kwenye ununuzi wa Jeneza,na majeneza ambayo unakuta wananunua ni yenye pesa ndefu!

Hivi inawezekanaje maiti ikawekwa kwenye jeneza la milioni 5,Hivi kweli mnakuwa mko Serious?

Hii tabia ipo kwa Wakristo sana sana,nashukuru Waislam wao huwa hawanaga huu ujinga!

Yawezekanaje mtu alikuwa anaumwa na pengine hata pesa tu ya matibabu mlishindwa kumchangia,lakini akifa tu ndo unaona sasa wanafamilia "Viherehere" wanaopendaga show off misibani wakijitolea kununua jeneza la bei chafu,kwanini huyo mtu asizikwe kwenye jeneza tu la kawaida la mbao zisizozidi elfu 50?,Kwanini mnaharibu pesa kwenye Maiti?,Hizo pesa si bora zingefanya shughuli nyingine?

Any way nisiwapangie lakini mimi binafsi nishatoa muongozo wa kimaandishi kisheria,Siku nikifa nizikwe bila Jeneza na kaburi langu lisijengewe wala kusakafiwa!
kWAKO WEWE LAKI 3 NI PESA NDEFU INAONYESHA JINSI ULIVO MASKINI. HIYO HATA HAIFIKI BAJETI YA CHAKULA CHA MBWA WANGU KWA MWEZI ALAFU UNAIITA PESA NDEFU? WAKIJA KWAKO USICHANGE FULL STOP. LAKINI MAISHA NI KUCHAGUA NDO MAANA WENGINE AKIPATA CHUMBA KIMOJA CHA KUISHI KWAKE KINATOSHA, LAKINI WENGINE WANAVYUMBA ZAIDI YA VITATU VYA KULALA KWENYE MOJA. WAKATI UNATEMBEA KWA MGUU MWENzAKO ANAPANDA DALADALA, WAKATI UNAPANDA DALADALA MWENZAKO ANAPANDA BODA BODA, WAKATI UNAPANDA BODA BODA MWENZAKO ANAPANDA TAXI HAYO NDO MAISHA. ISHI YALE UNAYOYAMUDU
 
Sawa Tajiri! But soma Mada uielewe kwa uzuri halafu urudi tena kuchangia kwa herufi ndogo utaeleweka tu Tajiri!
 
Sawa Tajiri! But soma Mada uielewe kwa uzuri halafu urudi tena kuchangia kwa herufi ndogo utaeleweka tu Tajiri!
Ushamba wa kutaka kupangia kila mtu maisha huoni kuna wengine hata baiskeli ya laki na nusu hana, lakini kuna watu wana magari ya milioni 500 mpaka bilioni. Ishi maisha yako na akili zako. Usije na agenda kuhusu familia za watu kwa sababu ya shida zako.
 
Mkuu hebu weka kapicha cha gari yako ya Milioni 500!
 
Kila jamii na utaratibu wake kama wewe umeamua utazikwa kwenye shuka la kufumwa kutokea ujiji kigoma usitake na wengine wafanye hivyo unavyo taka wewe na wala usijione wewe uko sahihi kuliko wao
 
Mambo hya mnayo nyinyi wakristo ata jeneza la laki tu ni gharama sembuse 5M

Ndo mna naupenda uislamu na najifakhari haswaa kuwa Muislamu

Dini ya kweli huku hatulalamiki kuhusu ilo jambo
 
kWAKO WEWE LAKI 3 NI PESA NDEFU INAONYESHA JINSI ULIVO MASKINI. HIYO HATA HAIFIKI BAJETI YA CHAKULA CHA MBWA WANGU KWA MWEZI ALAFU UNAIITA PESA NDEFU? WAKIJA KWAKO USICHANGE FULL STOP. LAKINI MAISHA NI KUCHAGUA NDO MAANA WENGINE AKIPATA CHUMBA KIMOJA CHA KUISHI KWAKE KINATOSHA, LAKINI WENGINE WANAVYUMBA ZAIDI YA VITATU VYA KULALA KWENYE MOJA. WAKATI UNATEMBEA KWA MGUU MWENzAKO ANAPANDA DALADALA, WAKATI UNAPANDA DALADALA MWENZAKO ANAPANDA BODA BODA, WAKATI UNAPANDA BODA BODA MWENZAKO ANAPANDA TAXI HAYO NDO MAISHA. ISHI YALE UNAYOYAMUDU
Punguza kisirani kaka,,Mbona kama umeghafilika?? tuliza akili soma tena,, muelewe mleta thread.
 
Mkuu nani kakashifiwa? Hebu mtag hapa aje aone namna "tulivyo" mkashifu!
Siishi maisha ya show off, lakini pia sijafika hiyo level ya kumiliki gari ya milioni 500 lakini siwezi kutaka kila mtu aishi maisha yangu. Pia zingatia nimeongea kutembea kwa miguu, bodaboda nk
 
Ikiwa pesa hiyo Marehemu hakuitafuta, na mpaka anakufa hakuwa nayo basi upo sawa.

Ila kama MAREHEMU anakufa na kuacha mahela mengi hapa Duniani, basi ni dhulma kubwa kumpumzisha bila kugharamia mazishi yake kwa namna ambayo hata yeye angependa iwe.
 
Ni sherehe yake ya mwisho ya binadamu. Tumefanya hivyo kwa my beloved Mom. Sioni ubaya sababu, tulimpenda akiwa hai na hata baada ya kifo, tunampenda na kumfanyia kwa ukubwa, kama alivyokuwa hai.
Pole mamii
 
Back
Top Bottom