Familia inayomuweka Marehemu kwenye Sanduku/Jeneza la kuanzia laki 3 kwenda Juu,hiyo Familia itakuwa na matatizo ya kiakili

Familia inayomuweka Marehemu kwenye Sanduku/Jeneza la kuanzia laki 3 kwenda Juu,hiyo Familia itakuwa na matatizo ya kiakili

Kwahiyo kama haujafika hiyo levo wewe na familia yako kwa kifupi mko kwenye lindi la umasikini,sasa inakuwaje kama ndivyo ushadadie masikini kuzikwa akiwa ndani ya Jeneza la Milioni 1?
Mimi siwezi kuwaza laki 3 za jeneza siku ukifa nitafute nitanunua hata sita uzikwe kwa heshima acha kuwa na roho ya kimaskini hivo ukizeeka utakuwa mchawi.
Ukiona roho inakuuma kwa sababu mtu fulani kafanya jambo fulani ujuwe hilo jambo si kwa ajili yako.
Kama sina gari ya milioni 500 lakini nikawa nayo ya milioni 20 hadi 30, siwezi kuona mwenye gari ya milioni 500 anaharibu hela.
Kama uwezo wako ni kuzikwa kwenye mkeka au jamvi zika au uzikwe hivo.
Yule ambaye anauwezo wa kuzika kuzikwa kwenye jeneza la dhahabu mwache azikwe hivo. Ishi maisha yako ya watu yatakuumiza tu.
 
Binadamu ana sherehe tatu hapa duniani kuzaliwa, kuoa/kuolewa na kifo... Sasa kama una uwezo au familia ina uwezo hizo sherehe ni haki ya kila binadamu... Marehemu baba, mama na dada yangu niliwazika kwa heshima zote na kuwafanyia sherehe zao za mwisho vizuri kabisa... Na kila mwaka nawafanyia misa na kuchinja ng'ombe tunakula na kunywa kusheherekea maisha yao ya hapa duniani
 
Muandishi akitoka hapa atapinga harusi. Ile ni shughuli na shughuli ni watu, acha watu wachange, pesa si ya marehemu wala familia, ni pesa ya ndugu jamaa na marafiki kwa umoja, ndio ina fanya zoezi lile, halihusiani na pesa za marehemu, Tunachangikiwa tuzikwe, kwanza ni heshima na. Upendo, ukishaona jeneza laki tatu, huyo mtu hakupendwa,
 
Elewa sababu, Hizo gharama ni kwa ajili ya walio hai kuwatambia walio hai wengine kuwa pesa ipo, si kwa ajili ya marehemu.

Binadamu tunapenda sifa na Msiba ni jukwaa la maonyesho la binadamu kutafuta kusifiwa kama ambavyo sehemu za ibada hutumika katika siasa.
 
Ukihitaji salamu kutoka kwangu nenda kwanza kwa CAG ukasome ripoti ya Mwaka uliyopita,Tofauti na hapo utaambulia chuya!


Huwa nashangazwa sana na namna ambavyo Familia nyingi zimekuwa zikihaha,kukabana na kushikana mashati wakati wa Msiba eti kisa tu ipatikane pesa ambayo inatakiwa iende kwenye ununuzi wa Jeneza,na majeneza ambayo unakuta wananunua ni yenye pesa ndefu!

Hivi inawezekanaje maiti ikawekwa kwenye jeneza la milioni 5,Hivi kweli mnakuwa mko Serious?

Hii tabia ipo kwa Wakristo sana sana,nashukuru Waislam wao huwa hawanaga huu ujinga!

Yawezekanaje mtu alikuwa anaumwa na pengine hata pesa tu ya matibabu mlishindwa kumchangia,lakini akifa tu ndo unaona sasa wanafamilia "Viherehere" wanaopendaga show off misibani wakijitolea kununua jeneza la bei chafu,kwanini huyo mtu asizikwe kwenye jeneza tu la kawaida la mbao zisizozidi elfu 50?,Kwanini mnaharibu pesa kwenye Maiti?,Hizo pesa si bora zingefanya shughuli nyingine?

Any way nisiwapangie lakini mimi binafsi nishatoa muongozo wa kimaandishi kisheria,Siku nikifa nizikwe bila Jeneza na kaburi langu lisijengewe wala kusakafiwa!
Mazishi /maziko yana utamaduni ndani yake. Tofauti ya maziko ya kikristo na kiislam na pia kwa dini nyingine imetokana na sehemu dini husika ilipoanzia. Kuzika kwa jeneza au bila jeneza au kwa kusokotwa kwenye ngozi, kuhifadhi maiti ndani au kwenye mapango, kuchoma vyote hivi vilikuepo kabla ya dini zetu ila dini zilifanya kutohoa hizo taratibu kutoka kwenye mila na desturi za watu dini ilipoanzia.

Mwarabu wa jangwani akiona mbao zinatumika kuzikia ataona ni kupoteza rasilimali adimu huku mmatumbi anaeishi kwenye misitu ya tropica akiona sio chochote sio lolote.
 
Usinikumbushe nilikuwa mwanakikundi flani hivi cha kusaidiana muda mrefu kidogo sasa tulikuwa na akiba za kikundi.
Ikatokea mweka hazina alifiwa na mama yake na huyo jamaa eti alivyokuwa lofa alikuta wameandaa jeneza la kawaida kumzikia mama yake akaona sio poa akachukua laki saba na nusu za kikundi na kwenda kumnunulia marehemu mama yake jeneza la hadhi la laki saba na nusu kabla ya kututaarifu sasa alipokuja toa taarifa hizo kwenye kikao wote tulikataa hiyo hoja na tukamkomalia arudishe hiyo hela hiyo ishu ilileta shida hadi kikundi kikafa
 
Mimi binafsi sina hela ila natamani baba yangu alipolala niwekee vigae si kila baada ya miezi kadhaa nabeba jembe kwenda kusafisha ,hii inanikumbusha mbali maana mzazi wangu aliondoka pasipotarajia ,ghafla sana.
 
Jamii zetu zina shida ya kiakili sana mkuu!
Mtu mweusi siku zote ni mtu asiyejielewa na asiyeweza kusimamia jambo lake.

amekuwa wa kuzoa kila kitu kama kilivyo bila hata kukipa tafakuri ni kama asiye na mila na desturi zake mwenyewe.

hata hayo ya kuzika bila jeneza yanayofanywa na baadhi yetu ni ya waarabu maana uko wanazika bila jeneza maana wapo jangwani hakuna chembe ya mti wa kuukata.

hapa hakuna cha mtu mweusi kujivunia km ndo chake. hata hizo nguo kubwakubwa na panapana wanazovaa wameiga ukouko uarabuni maana uko maisha ya jangwani full michanga inabidi wavae ivo kuzuia upepo mkali michanga n.k.

tuombeane heri ifike siku tujitambue turudie asili zetu
 
Sio msiba tu hata harusi, Huwa nashangaa vijana wanawaza mpaka mishipa ya vichwa inawatoka kuwaza na kuomba michango ili waoe. Ni upuuzi mtupu, hv arusi ikiwa na watu 30/40 mbona mambo yameisha kama ndio uwezo wa kamba yako ulipoishia. Anyway mwanzoni ilikuwa inaniumaga Sana lakini nikaja gundua Kwa sababu hiyo pesa nayo haiendi shimoni bali inaenda Kwa wale wenye kuhitaji kama wauza jeneza, maua, magari ya kubebea maiti nk nk na watoto wao wanapata maisha kumbe
 
Mkuu msiba toka lini ikawa sherehe,mkuu uko serious kweli au uenda unatania?

Tangu lini kwenye sherehe watu wakalia?,Au huko kwenu sherehe huwa zina ambatana na Vilio halafu Vilio vina ambatana na Vicheko?
Kama haujatembea usiwe na mdomo wa kuongea yote wakati haujui yote....Kuna kabira flan liko huko Tarime nadhani ni wajaruo...Mtu akifariki wao hawana muda wa kulia ni kukaa na huo msiba siku kadhaa na wanakodisha music system kabsaaa zinapigwa nyimbo zoote unazozijua playlist babu kubwaa.
 
Ikiwa pesa hiyo Marehemu hakuitafuta, na mpaka anakufa hakuwa nayo basi upo sawa.

Ila kama MAREHEMU anakufa na kuacha mahela mengi hapa Duniani, basi ni dhulma kubwa kumpumzisha bila kugharamia mazishi yake kwa namna ambayo hata yeye angependa iwe.
✅ mjadala uishie hapa.
 
Back
Top Bottom