Familia inayomuweka Marehemu kwenye Sanduku/Jeneza la kuanzia laki 3 kwenda Juu,hiyo Familia itakuwa na matatizo ya kiakili

Familia inayomuweka Marehemu kwenye Sanduku/Jeneza la kuanzia laki 3 kwenda Juu,hiyo Familia itakuwa na matatizo ya kiakili

Ni sherehe yake ya mwisho ya binadamu. Tumefanya hivyo kwa my beloved Mom. Sioni ubaya sababu, tulimpenda akiwa hai na hata baada ya kifo, tunampenda na kumfanyia kwa ukubwa, kama alivyokuwa hai.
anajua kama amefanyiwa?
 
Mkuu msiba toka lini ikawa sherehe,mkuu uko serious kweli au uenda unatania?

Tangu lini kwenye sherehe watu wakalia?,Au huko kwenu sherehe huwa zina ambatana na Vilio halafu Vilio vina ambatana na Vicheko?
msiba ni sherehee kama utabaki hapa duniani sawa
 
sasa pole ya nini kama juzi ya eid mnaenda kufanyia usafi makaburi ya ndugu zenu kuwakumbuka.na mda mwengine mnaita watu watu waje wafanye dua na chakula kuombea ujui hiyo ni sheree.
dini ni sehemu ya upofu sana kwa wengi unamcheka mwenzako kumbe na wewe unachekwa
 
Any way nisiwapangie lakini mimi binafsi nishatoa muongozo wa kimaandishi kisheria,Siku nikifa nizikwe bila Jeneza na kaburi langu lisijengewe wala kusakafiwa!

Chukua maua yako ingali bado unaweza kuyaona na kuyanusa yalivyo na harufu nzuri
 
Ukihitaji salamu kutoka kwangu nenda kwanza kwa CAG ukasome ripoti ya Mwaka uliyopita,Tofauti na hapo utaambulia chuya!


Huwa nashangazwa sana na namna ambavyo Familia nyingi zimekuwa zikihaha,kukabana na kushikana mashati wakati wa Msiba eti kisa tu ipatikane pesa ambayo inatakiwa iende kwenye ununuzi wa Jeneza,na majeneza ambayo unakuta wananunua ni yenye pesa ndefu!

Hivi inawezekanaje maiti ikawekwa kwenye jeneza la milioni 5,Hivi kweli mnakuwa mko Serious?

Hii tabia ipo kwa Wakristo sana sana,nashukuru Waislam wao huwa hawanaga huu ujinga!

Yawezekanaje mtu alikuwa anaumwa na pengine hata pesa tu ya matibabu mlishindwa kumchangia,lakini akifa tu ndo unaona sasa wanafamilia "Viherehere" wanaopendaga show off misibani wakijitolea kununua jeneza la bei chafu,kwanini huyo mtu asizikwe kwenye jeneza tu la kawaida la mbao zisizozidi elfu 50?,Kwanini mnaharibu pesa kwenye Maiti?,Hizo pesa si bora zingefanya shughuli nyingine?

Any way nisiwapangie lakini mimi binafsi nishatoa muongozo wa kimaandishi kisheria,Siku nikifa nizikwe bila Jeneza na kaburi langu lisijengewe wala kusakafiwa!
Tafuta hela, kijiba cha roho kitakuua mapema tukuzike kwenye mkeka. Mawazo ya kimasikini huwa yanaamini kila kizuri anachokitumia au kukifanya mwenye hela hakikustahili. Utasikia:-
  • Hayo mavi8 yanamaliza mafuta. MAWAZO YA KIMASKINI
  • Kuzikia jeneza la Laki3 ni kuchezea hela. MAWAZO YA KIMASKINI
  • Unajenga ghorofa ukizeeka utaishi ghorofani>? MAWAZO YA KIMASKINI
  • Unavaaje nguo ya Laki 5. MAWAZO YA KIMASKINI
  • Upande ndege au gari kufika ni kufika tu. MAWAZO YA KIMASIKINI
  • Nk...
 
Siishi maisha ya show off, lakini pia sijafika hiyo level ya kumiliki gari ya milioni 500 lakini siwezi kutaka kila mtu aishi maisha yangu. Pia zingatia nimeongea kutembea kwa miguu, bodaboda nk

Kwahiyo kama haujafika hiyo levo wewe na familia yako kwa kifupi mko kwenye lindi la umasikini,sasa inakuwaje kama ndivyo ushadadie masikini kuzikwa akiwa ndani ya Jeneza la Milioni 1?
 
Tafuta hela, kijiba cha roho kitakuua mapema tukuzike kwenye mkeka. Mawazo ya kimasikini huwa yanaamini kila kizuri anachokitumia au kukifanya mwenye hela hakikustahili. Utasikia:-
  • Hayo mavi8 yanamaliza mafuta. MAWAZO YA KIMASKINI
  • Kuzikia jeneza la Laki3 ni kuchezea hela. MAWAZO YA KIMASKINI
  • Unajenga ghorofa ukizeeka utaishi ghorofani>? MAWAZO YA KIMASKINI
  • Unavaaje nguo ya Laki 5. MAWAZO YA KIMASKINI
  • Upande ndege au gari kufika ni kufika tu. MAWAZO YA KIMASIKINI
  • Nk...

Kwahiyo ukiwa na pesa ndo uzipoteze kwenye Jeneza la Maiti ?
 
Umaskini ni laana aisee. Inafanya hadi mtu amwonee wivu marehemu.


Nani aionee wivu Maiti,Yaani jitu limekufa linanuka na kuoza nalo nila kuonea wivu?

Wivu nilionao ni kwenye familia zilizo hai,Haiwezekani mtumie pesa kubwa kununua Jeneza wakati huo huo familia zinalia na umasikini!
 
Tabia hii imekithiri sana kwa familia za kitajiri.hao ndo wanaopenda sana showcase mbele za watanzania
Familia za kitajiri means wana uwezo, ni namna gani wanatumia pesa zao kwenye misiba hilo ni la kwao, si la kwenu. Kwa hiyo msiokuwa na uwezo msiwapangie wenye nacho
 
Ni kama wewe tu unavyokula dagaa na kuziita dagaa nyama.... Hakuna dagaa nyama kula nyama Kwa uwezo wako...
Karne nyingi sana watu walizikwa kwenye masanduku hasa huko misri ya kale kabla ya kuvamiwa na waarabu.

Hata kuvaa ni anasa . Mtu mwenye pesa zake na familia yake wanaamua wenyewe namna ya kumzika ndugu yao . Wauza majeneza wanashukuru Wale wanaonunua majeneza .
Hata hivyo nakubaliana na wewe kuwa majeneza yanatuka kuharibu mazingira kwa kutumia maelfu ya tani za mbao kuzifukia ardhini na kuacha ziliwe na mchwa.

Panahitaji marekebisho mana mtu akisha kufa anahitaji kurudishwa kwenye udongo kwa namna yoyote kwa gharama ndogo na kwa heshima.

Kupanga ni kuchagua
 
Soma heading yake alafu uone nani aliyeghafilika, Angeongea kuhusu jamii kuhudumia mtu akiwa hai pasipo kusubiri afe ndo watu wachange well and good. Ningeona point yake. Lakini kusema familia inayomuweka marehemu kwenye Jeneza la 3 kwenda juu haina akili hayo ni mawazo ya kimaskini, kufikiria matumizi ya mwenzio na kutamani hiyo hela ungepewa wewe. Kifupi ni Ubinafsi ana uhakika gani kuwa wote wanaotumia majeneza ya hizo gharama hawakuwahudumia wagonjwa wao kabla ya mauti kuwakuta?
Yeye wasio wake wa namna ya kuzikwa apeleke kwenye familia yake yawezekana hapa hata kusoma hawamsomi
Basi Sawa✊✊✊
 
Back
Top Bottom