Familia nyingine ni za ajabu sana

Familia nyingine ni za ajabu sana

Wabibi wa Kanyengereko wanajua wanachokizungumza omwana. Na zaidi kuna siku huyo wa pili almanusura aropoke stori kamili. Alishaanza baba leo tumeenda kwa baba yake na...mama mtu akamuwahi kwa karipio kali na kuipotezea stori.

Inawezekana ndugu yenu anajua sema kanyamaza hajataka kuishirikisha familia kaamua kufa na tai shingoni. Unajua ndoa zina mengi sana
 
Inawezekana ndugu yenu anajua sema kanyamaza hajataka kuishirikisha familia kaamua kufa na tai shingoni. Unajua ndoa zina mengi sana
Wewe unaweza kufanya hivyo yaan kuchanganya damu za wanaume usizae na mwanaume mmoja alafu watoto wote umpe mwanaume mmoja?
 
Inawezekana ndugu yenu anajua sema kanyamaza hajataka kuishirikisha familia kaamua kufa na tai shingoni. Unajua ndoa zina mengi sana
Hahaha. Sisi kama ndugu tulishuazimia mambo haya:
👉 Tutawajali watoto kama wa ndugu yetu japo sio wake. Tutaacha tu siku kuwatambua ikatokea ndugu yetu katangulia duniani. Maana huyo mwanamke ni aina ile ya kuponda na kufanya anasa. Kutafuta hajui, kazoea mume wake analeta. Na uzuri jamaa mfuko yuko njema tu. Ila mwanamke ni kichomi kwelikweli. We fikiria mpaka marafiki zake wamekata mguu. Mwanamke hapendi marafiki, ndugu wa mumewe..mbaya zaidi hata ndugu zake. Ni mwanamke wa ajabu kwelikweli.
 
Wewe unaweza kufanya hivyo yaan kuchanganya damu za wanaume usizae na mwanaume mmoja alafu watoto wote umpe mwanaume mmoja?

Hapo kuna kitu, inawezekana ndugu yao akawa na shida ya uzazi ila wakaamua wafanye hivyo ili kumfichia aibu. Mimi siamini mwanaume uletewe watoto watatu tofauti afu kila mmoja na baba yake na bado usigundue!!!
 
Hapo kuna kitu, inawezekana ndugu yao akawa na shida ya uzazi ila wakaamua wafanye hivyo ili kumfichia aibu. Mimi siamini mwanaume uletewe watoto watatu tofauti afu kila mmoja na baba yake na bado usigundue!!!
Ndio maana nilikueleza kamfanya zuzu. Mwanzoni vitimbi vya mwanamke ndugu alikua tayari kumuacha. Mwanamke kafanya ya kufanya mwamba huyu hapa kanyooka. Mwanamke ndiye mwenye say
 
Hahaha. Sisi kama ndugu tulishuazimia mambo haya:
[emoji117] Tutawajali watoto kama wa ndugu yetu japo sio wake. Tutaacha tu siku kuwatambua ikatokea ndugu yetu katangulia duniani. Maana huyo mwanamke ni aina ile ya kuponda na kufanya anasa. Kutafuta hajui, kazoea mume wake analeta. Na uzuri jamaa mfuko yuko njema tu. Ila mwanamke ni kichomi kwelikweli. We fikiria mpaka marafiki zake wamekata mguu. Mwanamke hapendi marafiki, ndugu wa mumewe..mbaya zaidi hata ndugu zake. Ni mwanamke wa ajabu kwelikweli.

Mhmmm!! Hapo inatakiwa rehema ya Mungu ya hali ya juu. Ni mtihani mzito huo
 
Ndio maana nilikueleza kamfanya zuzu. Mwanzoni vitimbi vya mwanamke ndugu alikua tayari kumuacha. Mwanamke kafanya ya kufanya mwamba huyu hapa kanyooka. Mwanamke ndiye mwenye say

Kabisaa wahaya mmekubali kuzidiwa nguvu na wazaramo??? Unajua bado siamini? Wahaya kwa dawa za mitishamba na kupumbaza wanaume wanazo tena zile konki, hebu rudini kwa mabibi zenu mumsaidie ndugu yenu.

Km imeshindikana pigeni goti kwa Mungu km ni kweli yote yataisha. Mungu hajawahi kushindwa ni kitendo cha muda tu
 
Kuna familia zingine zinashangaza na zinakatisha tamaa sana.

Sisi kwenye familia yetu tumezaliwa watoto 9 wakiume tupo 6 na wakike wa 3 na uzao wetu umekaa hv kuna kaka zangu wakubwa wa 3 waliozaliwa miaka ya 70 then wanafuata dada 3 waliozaliwa miaka ya 80 halafu ndio sisi tena wakiume wa 3 wa mwisho tuliozaliwa miaka ya 90.

Kiukweli tulilelewa vzr sana na atukuwahi kushinda wala kulala njaa japo mzee alikuwa anafanya kazi ya kawaida sana ila alijitahidi kuhakikisha watoto wake tunalelewa vzr japo kwenye swala la kielimu atukufika mbali sana.

Mzee alijitahidi sana kuwekeza nguvu zake kwa hao kaka zetu wakubwa miaka ya 90 kipindi sisi wengine bado tupo wadogo sana ili wao ndio waje kuwa msaada kwetu.

Shida ni kuwa kaka zangu wawili walikuwa ni watu wa starehe na pombe mwisho wa wakafukuzwa kazi. Mmoja aliiba pesa kiac cha sh milioni 2 kazini kwake akakimbilia nchi jirani ya kenya hiyo ni milioni 2 miaka ya 90 haikuwa pesa ndogo, huko alikokwenda pia aliendekeza starehe kama kawaida mwisho pesa zote zilikwisha na mbaya zaidi aliugua sana ikabidi tena mzee aende kumfata huko alipokuwa,

na kaka yangu mwingine alienda mbali zaidi kufikia hatua ya kuingia chumbani kwa mzee na kuiba kiac kikubwa cha pesa na kukimbilia uganda,
Japo nilikuwa mtoto ila sikushindwa kujua maumivu aliokuwa nayo mzee, kwa mara ya kwanza nikamuona mzee akitokwa na machozi mbele yangu aisee niliumia sana.

Mwamba huko uganda akawa mtu wa starehe sana ni mwendo wa pombe na wanawake mwisho pesa zilikwisha akarudi tanzania akawa anakuja nyumbani kwa siri, Siku moja usiku muda wa saa 8 baba aliskia kama mchakacho akachukua panga akakutana na mtu anatoka koridoni mzee akataka kumkata panga akijua kuwa ni mwizi kwa bahati nzuri bro akawahi kutoa sauti ndio mshua akashusha panga.

Kama mjuavyo wazazi ni watu wenye huruma akamsamehe mambo yakaisha japo mshua akuwa na upendo nae tena.

Imepita miaka kadhaa wakaja na project kwa mzee hiyo ilikuwa 2008 mzee akaona sio mbaya akawapa tena mtaji wakiwa wawili rejea nyuma hao wote walishaiba pesa katika vipindi tofauti.

Ila cha kusikitisha hakuna cha maana walichofanya kumbuka hapo nguvu ya mzee katika kufanya kazi imeshaanza kupungua halafu akikumbuka watoto wake wakubwa ambao aliwekeza kwao amna cha maana walichofanya zaidi ya kumtia tu hasara ilifikia stage mpaka sisi wadogo mshua akawa anatuchukia kwa makosa ya kaka zetu wale wakubwa japo sisi bado ni watoto wadogo na tunasoma ila mara nyingi alikuwa anamwambia mama unaona watoto wako hawa wadogo pia wakikua watakuwa kama kaka zao aisee hilo jambo lilikuwa linaniumiza sana.

Ila nachoshukuru kati ya wale kaka zangu wakubwa watatu kuna mmoja yeye alipomaliza shule alienda dar miaka ya 2000 alihustle ila kiac alifanikiwa na ndio huyo akawa anampa mshua back up pale hali inapokuwa mbaya.

Kuna kipindi huyo bro aliyumba kiuchumi na mshua alikuwa mgonjwa na kama mjuavyo familia nyingi za kimaskini ni mpaka mzee atoke ndio familia ipate kula bac mshua baada ya kuwa katika mazingira yale alianza kupata stress akikumbuka nguvu aliyowekeza kwa vijana wake wakubwa ilivyopotea bure mpaka sasa familia aina chakula na yeye ambae ndio mtafutaji yupo chini bac mzee alianza kudhoofu sana hiyo ilikuwa 2011 kipindi hiko mi nipo form2 bac kuyumba kwa mzee vile ilipelekea tukakosa ada bac nikakaa home.

○Mzee maradhi na stress vilimuandama sana mwisho akalazwa hospitali kwa bahati mbaya akafariki. Bac tukaanza namna ya kutafuta mawasiliano ya wale kaka zangu wawili watukutu maana walikuwa wilaya nyingine kipindi hiko tuliwapata aisee jamaa wamekuja msibani hawana hata mia yani wamechakaa kinoma. Bac yule bro ambae yupo dar alijitahidi kwa nguvu zake mwenyewe akamiliza msiba fresh.

○Na ndio anaetoa msaada mkubwa kumlisha mama toka mzee amefariki yeye ndio tegemeo la familia maana dada zangu pia maisha yao ni tabu tu na wote hawajaolewa mpaka sasa.
○Wanaishi kwa kuunga unga tu aisee kuna baadhi ya familia ukizaliwa ni shida sana.

Cha kusikitisha kingine ni kwamba wale kaka zangu wawili mpaka leo hii mmoja ana miaka 50 mwingine ana miaka 45 bado wapo wapo tu wakipata pesa ni pombe na wanawake awana wake wala watoto na mbaya zaidi wao wote wamerudi home wanaishi na mama lakini awajishughulishi na chochote wamekaa tu wanakula kwa mgongo wa bi mkubwa kiukweli kuna familia nyingine zinakera sana.

Ebu fikiria vijana wakubwa wawili miaka 40+ wanashindwa kumlisha mama yao nao wamekaa wanalishwa, just imagine mpaka umeme wa elfu 2 unapigiwa simu dar wakati home kuna vijana wawili wakubwa wao wakipata pesa zao wanaenda kuishi guest mpaka wahakikshe hizo pesa zimeisha ndio wanarudi home halafu wanasubili sisi ndio tuwalishe kifupi tu ni kwamba hao ma bro washakula pesa za watu nyingi na hawajawahi kurudisha.
na kipindi nipo mkoa nilikuwa najaribu kuwashauri ila nilikuwa naishia kukabwa na kutaka kupigwa

Wengine ndio tumepata ajira jana tu hata kujipanga bado lakini simu za mzazi zimekuwa nyingi wakati pale home kuna vijana wakubwa hawataki kujishughulisha na mbaya zaidi mama hata kuwashauri wanae hawezi sometime wanakuja kukaa hapo na wanawake zao halafu bado pesa ya kula sisi ndio tunatafuta ukimtumia mama nae anakaa anakula na wanae, yani wanaenda kuzurura huko wakirudi wanakuta mama kawaachia msosi wanakula wanaondoka tena wanaenda kuzurura wakirudi usiku tena unakuta bi mkubwa kawaachia msosi wanakula wanaenda kulala kesho tena hivohivo jamani halafu fikirieni watu wanaofanya hivo ni watu wenye miaka 40+

Na pesa ya matumizi ikiisha bi mkubwa anawatafuta tena mnaangaika mkipata mnatuma bi mkubwa anaendelea kula na wanae halafu mbaya zaidi nayeye hata awashauri wanae ukimueleza awashauri watoto wake pia wajishughulishe anakwambia sasa kama hawa kaka zako hawana pesa wafanyeje utadhani sisi ndio tunahela wakati tunaangaika ili mama apate kula wengine hata mambo ya wanawake tulishasahau kutokana na majukumu ya kifamilia jinsi yanavyotubana.
Lakini unakuta hapo kuna baadhi ya ndugu zako tena wengine wangeweza hata kukuzaa wao wamekaa wanasubili wewe uhangaike uwatumie pesa wao wale.

Hapa toka jana mama ameshaanza kusumbua anahitaji pesa ya matumizi na sio muda mrefu nilimtumia laki moja na bro school bus yake pia iliangukiwa na mti ipo right off namimi na saiz bado mambo yangu ayajakaa sawa.
Halafu fikiria hapo home kuna wazee wazima ambao hata sio walemavu wamekaa wanasubili uhangaike utume pesa wale.

Aisee kuna familia nyingine zinakatisha tamaa sana kama ni laaana bac hii ya familia yangu imezidi mpaka najuta ni kwanini nilizaliwa na ndugu kama hawa, jamani nimechoka just imagine mpaka umeme wa elfu mbili mama anakupigia simu dar.
Pole sana mdogo wangu... Wakati mwingine hizi huwa ni roho na maagano ambayo hatuwezi kuyang'amua kwa macho ya kawaida. Inahitaji kufanya sana sala/dua na kufunga ili kujikomboa kutoka katika vifungo hivi.
 
Mchukuenj mama mkaishi.nae...ila hawakawii kuuza nyumba Kwa Tabia ulizielezea Mkuu...poleni sana aseee
 
Binadamu wa kawaida hawezi kuishi Maisha Kama hayo unabidi kuelewa Familia yenu hipo Katika nguvu za giza ni swala la kuwaza kuwakomboa hao ndugu zako na dada zako walifungwa kiroho .

Hata Mama yako kafungwa kiroho tafuta watu sahihi wakusaidie.

Ndo maana hawawezi lolote Wapo vifungoni na sifa kuu ya mtu kuwa kifungoni ni ubishi wa Jambo na kutokujua maamuzi au kujali maumivu ya mwenzie.
Shukrani mkuu nitajitahidi kutafuta ufumbuzi
 
Usichokiona kuhusu familia yako ni kikubwa na kigumu zaidi ya kile unachokiona.

Usipotafuta mzizi wa shida ya familia yenu na kuimaliza hata wewe utaishia humohumo. Na dalili ushaziona huwezi save pesa yoyote wala huwezi fanya maendeleo

Mungu akufungue macho uone na kutatua tatizo
Amina amina
 
Ushauri wangu nikikupa kwa lugha laini hutaelewa. Nianze kwa kusema wewe ni mpuuzi unayejibebesha mizigo isiyokuhusu. Unadhani utambadilisha nini mtu wa miaka 50? Acha huo upumbavu. Kama tayari mama anawatetea basi fanya kumtumia hela ambazo unaona ziko ndani ya uwezo wako kisha kausha songa mbele na maisha yako. Pia anza ku-plan familia yako mapema. Yale makosa ya wazazi wetu tusiyarudie. Kuzaa watoto 9 huku kipato duni ni sawa na kujiua taratibu. Zaa unaomudu na hakikisha wanapata elimu bora ya kutosha. Nyie kwenu inaonekana karibu wote vipato duni hali inayochangiwa na elimu ndogo. Kwa sasa pambania maisha yako.
Kabisa umeongea ukweli
 
Ushauri wangu nikikupa kwa lugha laini hutaelewa. Nianze kwa kusema wewe ni mpuuzi unayejibebesha mizigo isiyokuhusu. Unadhani utambadilisha nini mtu wa miaka 50? Acha huo upumbavu. Kama tayari mama anawatetea basi fanya kumtumia hela ambazo unaona ziko ndani ya uwezo wako kisha kausha songa mbele na maisha yako. Pia anza ku-plan familia yako mapema. Yale makosa ya wazazi wetu tusiyarudie. Kuzaa watoto 9 huku kipato duni ni sawa na kujiua taratibu. Zaa unaomudu na hakikisha wanapata elimu bora ya kutosha. Nyie kwenu inaonekana karibu wote vipato duni hali inayochangiwa na elimu ndogo. Kwa sasa pambania maisha yako.
Kabisa umeongea ukweli
 
Hua nasema ndugu yako wa damu ni wewe in another image ( body), kwahyo kama unaona kuna mambo hayako sawa basi unatakiwa umsaidie au umuombee maana kwa kufanya hivyo unakua unajisaidia wewe pia

Lakini kuona kana kwamba umezaliwa bahati mbaya hapo kwa Mungu hakuna bahati mbaya(wala wazee wa mambo ya kiroho wanajua)
Mtoa mada usijaribu kujiona upo hapo kibahati na ukawakosoa au kudhihaki, kwakufanya hivyo utakua unajivua nguo wewe mwenyewe,
Upo hapo kwa sababu
 
Wapo watakaokuona Zuzu eti mlete bimkubwa mpangishie chumba na yeye qummke kuna watu wanachukulia mambo rahisi rahisi tu kisa wanazishika elfu 10 10 bila kutumia nguvu zozote
Watu wanachukulia vitu simple sana😂😂
 
Huna uwezo huo hio ni destiny yao yaan wameshagota wachukulie km walemavu tu akili zao zimeshagota hao ndugu zako hata km utawaona wapo sawa Ila hawapo sawa kiakili, hapo ni kumuachia Mungu tu wapande gari moja wote wapigwe mzinga mkawazike basi ndio pona yenu kinyume na hapo wewe toa msaada tu ahsante zao zitarudi kwenye mikono ya watoto wako watakurudishia wakikua ingawa pia mambo yanabadirika unaweza usaidie na usisaidiwe
Sawa mkuu
 
Nimeshakwambia wapo watakaokuona Zuzu ukisema hivyo wengi wao wanafikiria umepanga apartment na unaishi Masaki huko kumbe jamaa yangu upo zako uswahili chumba cha giza hakina hata umeme na life linasonga
Yani acha mzee watu wanachukulia mambo easy sana
 
Huna uwezo huo hio ni destiny yao yaan wameshagota wachukulie km walemavu tu akili zao zimeshagota hao ndugu zako hata km utawaona wapo sawa Ila hawapo sawa kiakili, hapo ni kumuachia Mungu tu wapande gari moja wote wapigwe mzinga mkawazike basi ndio pona yenu kinyume na hapo wewe toa msaada tu ahsante zao zitarudi kwenye mikono ya watoto wako watakurudishia wakikua ingawa pia mambo yanabadirika unaweza usaidie na usisaidiwe
Sawa mkuu ngoja nifanye yanayonihusu
 
Back
Top Bottom