Accumen Mo
JF-Expert Member
- May 15, 2022
- 18,036
- 39,882
Nadharia ila tambua dunia hapa mambo mengi ya kimaisha hayana uhakika 100% kaka yanaendana na karma .Ameeni hata mimi naunga mkono.
Huenda Baba alikuwa anapata pesa zisizo halali huwezi jua.
Kumbuka kuna watu wanapata pesa kwa kushiriki mauaji, utekaji ujambazi.
Hawa watu hata kama unaona wana hela mwisho wa siku hawana furaha. Kama ambavyo mleta mada ameelezea baba yake alikuwa mtu wa huzuni tu.
Hii ipo sana kwa vile wewe unakuwa na una watoto utakuja kuona ,dunia ina adhibu kwa kosa ambalo hukufanya mfano wewe unaweza kuwa msomi ukazaa watoto wote vilaza na hawataki hata shule tena wezi na wahuni kabisa.
Mambo mengi katika dunia yanasikitisha kwa ujumla ni suala la kuomba Mungu,babu yangu mimi ni imamu wa msikiti tena mtu mkubwa kijijini ila mwanae mmoja ndo mlevi mkubwa na mzinzi hapo kijijini mkubwa ana watoto kila kona wanaletwa tu hapo kwa bib ni chapombe kila kona kazalisha na kakimbia.
Mwalimu wetu mmoja msingi miaka hiyo alikuwa na mumewe anafanya kazi TRA ,walipata mtoto wa kwanza zombi kabisa yaani tahira hata lipelekwe shule za kulipia halielewi na mtoto wao wa pili ni wakiume ni mwizi kabisa na shule hataki ,ni vile wazazi wake ni wachaga so wana wanabars pale town ila watoto waliozaa wote hawana akili.wanazunguka tu kweny biashara za wazazi wao